EACJ: Vyama vya Upinzani vyashinda kesi dhidi ya Tanzania, kuhusu mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Siasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Itakumbukwa kwamba Chadema ilifungua kesi ya kupinga mabadiliko ya sheria za vyama vya siasa nchini Tanzania yaliyopitishwa na bunge bila aibu ili kuua demokrasia na kukandamiza vyama vya upinzani, Kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2020 kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko Arusha.

Leo Hukumu ya kesi hiyo inasomwa, Tayari Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema amekwishafika Mahakamani hapo akiambatana na Wakili wa chama chake John Mallya.

Pia, soma:

1). Vyama vya Upinzani vyafungua kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga Sheria kandamizi ya vyama vya siasa kutumika

UPDATE

‪Mahakama ya haki ya Afrika ya mashariki (The East African Court of Justice - EACJ) katika shauri namba 3 la mwaka 2020 lililofunguliwa na Freeman Mbowe na wenzake, leo, 25/3/2022, imetoa hukumu kwamba Mabadiliko ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2019 (the Political Parties Amendments Act 2019) yanakiuka mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika ya Afrika Mashariki (EAC) sehemu ya 6(9)(72).

Hivyo mahakama ya EACJ imeamuaru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurekebisha sheria ya vyama vya siasa ili iendane na mkataba. Pia, gharama za kesi kwa kila mleta maombi kulipwa na serikali.

Freeman Mbowe na wenzake katika shauri hilo waliwakilishwa kisheria na mawakili John Mally, Jebra Kambole na Sheki Mfinanga.

Vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania vilishtaki serikali ya Tanzania katika mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu haki ya EACJ kufuatia mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa.

Sheria hiyo ambayo ilitiwa saini na Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari na kuchapishwa katika gazeti la serikali siku 10 baadaye, ilizua mjadala mkubwa nchini.
#MMM‬

----
Jaji:
Na kwamba sheria kumpa msajili uhuru wa kuingilia mambo ya ndani ya chama cha siasa!

Na kwamba msajili sio mtu huru kwa kuwa anateuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa.

Ni maoni ya mahakama hii kuwa sheria hii inampa msajili nguvu kubwa dhidi ya vyama vya siasa jambo ambalo ni kinyume cha mkataba wa Jumuiya

Hitimisho

Mahakama hii ina declare kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6d 72 ya Jumuiya ya Afrika

Jamhuri ya Tanzania inaamriwa kurekebisha sheria ya vyama siasa iendane na mkataba.

Gharama za kesi kwa kila mmoja

Jaji anahitmisha

KESI_MAHAKAMA_YA_AFRICA_MASHARIKI%0A%0ASEHEMU_YA_2_%0A%0AHukumu_ipo_tayari%0A%0ANa_itaanza_kus...jpg
 
Mama atafika 2025 amechoka sana. Hii mikwaju huku na kule juu na chini.
Kwa vile 2025, Watanzania wazalendo tumeisha amua twende na mgombea mwanamke, nashauri Mama asichoshwe

P
 
Back
Top Bottom