EACJ: Vyama vya Upinzani vyashinda kesi dhidi ya Tanzania, kuhusu mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Siasa

EACJ: Vyama vya Upinzani vyashinda kesi dhidi ya Tanzania, kuhusu mabadiliko ya Sheria za Vyama vya Siasa

Jaji:
Na kwamba sheria kumpa msajili uhuru wa kuingilia mambo ya ndani ya chama cha siasa!

Na kwamba msajili sio mtu huru kwa kuwa anateuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa.

Ni maoni ya mahakama hii kuwa sheria hii inampa msajili nguvu kubwa dhidi ya vyama vya siasa jambo ambalo ni kinyume cha mkataba wa Jumuiya

Hitimisho

Mahakama hii ina declare kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6d 72 ya Jumuiya ya Afrika

Jamhuri ya Tanzania inaamriwa kurekebisha sheria ya vyama siasa iendane na mkataba.

Gharama za kesi kwa kila mmoja

Jaji anahitmisha
Sasa sijui hit sheria wataifuta au?
 
Enzi za JPM na Kabudi Tz ilijitoa kwenye hii mahakama, sijui kama ilisharudi...
 
Itakumbukwa kwamba Chadema ilifungua kesi ya kupinga mabadiliko ya sheria za vyama vya siasa nchini Tanzania yaliyopitishwa na bunge bila aibu ili kuua demokrasia na kukandamiza vyama vya upinzani, Kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2020 kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko Arusha.

Leo Hukumu ya kesi hiyo inasomwa, Tayari Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema amekwishafika Mahakamani hapo akiambatana na Wakili wa chama chake John Mallya.

Pia, soma:

1). Vyama vya Upinzani vyafungua kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kupinga Sheria kandamizi ya vyama vya siasa kutumika

UPDATE



----


Mbowe saivi ni kama remote tu sio yeye, hakuna tena kitu hapo ni vile moshi unaonekana kufuka tu lakini moto ushamwagiwa maji zamani, kwisha chadema
 
Wazee wakushupaza shingo sijui kama watatekeleza maana hata swala la mgombea binafsi lilipuuzwa wanatakiwa kupigiwa kelele.
Hakuna cha kushupaza shingo. Hakuna sheria ya kuilazimisha nchi yoyote kutekeleza uamuzi wa mahakama hii na ndio maana gharama za kesi hizi kila mmoja anabeba msalaba wake ajijue kuwa ameshinda au ameshindwa na ndio mwisho wake hapo.

Hivyo sheria ya Vyama vya Siasa lazima iheshimiwe na itaendelea kutekelezwa kama ilivyo na Chadema lazima waiheshimu wakiikiuka watawakuta kwa mujibu wa Sheria za Tanzania

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Majaji wetu tume ya uchGuzi, vyama vya siasa ni wazi wanachangia kutupa sheria mbaya unashangaa ujaji wameupataje.

Haya mambo yanaonyesha umuhimu wa katiba mpya.
 
Majaji wetu tume ya uchGuzi, vyama vya siasa ni wazi wanachangia kutupa sheria mbaya unashangaa ujaji wameupataje. Haya mambo yanaonyesha umuhimu wa katiba mpya.
Katiba mpya ni sasa
 
Back
Top Bottom