East African Federation (EAF) public Views


What is his current salary?
 
Kichuguu,
He is paid about $10,000 a month now before allowances.
Had he accepted his salary would have jumped to $30,000 a month.
 
Brothers & Sisters
kuna faida na hasara za kuwepo kwa Shirikisho, kinachotakiwa kufanywa ni kuhakikisha kila nchi inapunguza hasara na kuongeza faida bila kuathiri fursa ya nchi mwanachama. Hatuwezi hata kwa vigezo vya kiuchumi kizifanya nchi hizi zikawa sawa kimaendeleo, wanazuoni watathibithisha hili.

Maoni yangu kwa Tanzania ni kuwa maadamu inajiunga kama Tanzania basi imalize matatizo yake ya Muungano na Zanzibar kwanza ndipo iende EAC isije tumia muda mwingi kushughulikia masuala yake ya ndani wakati UG na KY zikipiga hatua halafu nchi ikaanza ulalamishi kuwa UG na KY wanatuzidi kete.

Hili ya Muungano ni kipimo cha uadilifu wa kujiunga si tu na EAC bali hata shirikisho lingine lolote litakajitokeza.

Viongozi waliopo madarakani wasifiri hali ni shwari Zanzibar na hata Rais wakati akihutubia Bunge katika kikao chake cha Ufunguzi tarehe 30.12.2005 alikiri kuwepo kwa UFA na waswahili walisema usipozipa ufa utajenga ukuta.
 
Na bado, ngoja huo "MUUNGANO"uje!!

Kenya yanyakua sifa za Serengeti kwa utalii

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI dunia inatambua umaarufu na utajiri wa kitalii wa mbuga ya Serengeti na hivi karibuni kutangaza kama moja ya maajabu mapya ya dunia, Tanzania imeendela kuduwaa bila kuitumia nafasi hiyo kwa kutangaza utalii.

Badala yake majirani zake Kenya, ambako mbuga ya Serengeti inaendelea kwenye mipaka yake kwa jina la Masai Mara, imechangamkia umaarufu huo kwa kutangaza kwa nguvu sehemu yao kwenye tovuti na majarida mbalimbali duniani.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kwamba baada ya Serengeti kutangazwa kwamba ni moja ya maajabu mapya saba duniani ikishika nafasi ya saba, wahamasishaji wa utalii wa Kenya wamechukua nafasi hiyo kuitangaza kwa nguvu Masai Mara, ambayo ni sehemu ya mwendelezo wa mbuga ya Serengeti.

Novemba 17 mwaka huu kwa mara ya kwanza, Serengeti ilitangazwa kuwa ni moja ya maajabu hayo mapya na Kituo cha Televisheni cha ABC kupitia kipindi chake cha Good Morning America Tv Show na katika gazeti la USA Today.

Kwa kuwa Masai Mara ni eneo moja na Serengeti lakini likitengenishwa tu na mpaka wa Tanzania na Kenya, watetezi na wahamasishaji wa utalii wa Kenya, wamechangamkia mafaniko hayo kwa kutangaza kwamba maajabu hayo mapya saba ni Masai Mara.

Mbuga ya Serengeti kwa upande wa Tanzania ina ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 wakati Masai Mara ina ukubwa wa kilometa za mrada 1,510 tu.

Juhudi hizi za Kenya zinaiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuvutia utalii kwa upande wa Masai Mara, lakini Serengeti ikiwa na ukubwa mara 9.7 ya Masai Mara bado haijatangazwa vya kutosha kuweza kufaini nafasi hii mpya ya kuwa maajabu ya dunia.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amethibitisha kutambua kupanda chati kwa Serengeti, lakini pia kutambua kwamba kuna njama za kimataifa za kuitangaza kama Masai Mara.

Alisema Tanzania haiwezi kuingia katika malumbano ya 'kihujuma' bali itaudhihirisha ulimwengu kuhusu Serengeti na vivutio vyake vya utalii.

Kauli kama ya Profesa Maghembe pia ilitolewa na Rais wa Kampuni ya Bradford Group ya Marekani, Mira Berman, ambayo imepewa dhamana ya kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania. Alisisitiza kwamba Serengeti ndiyo imekuwa maajabu ya saba mapya ya dunia.

Berman alisema mjini New York wiki iliyopita, kwamba takwimu zinaonyesha kwamba baada ya Serengeti kutangazwa kama maajabu ya saba idadi ya watalii wanaosafiri kuelekea Afrika imeongezeka.

Rais huyo alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni nyingine ambazo ni Miracle Corner of the World na African Travel Association (ATA), zimekubaliana kumeiweka Tanzania katika nafasi nzuri kiutalii.

Hata hivyo, alisema tatizo kubwa linalaoikabili Tanzania ni ukosefu wa miundombinu ya kisasa, ikiwamo mahoteli makubwa na kutaka serikali iongeze bajeti ya utalii.

Wakati Maghembe na Berman wakisema hayo, gazeti hili limebaini mtandao unaonyesha maajabu hayo wa www. new world seven wonders, ukiitaja mbuga iliyoshinda kwamba ni Masai Mara na hakuna eneo ambalo Serengeti imetajwa.

Watangazaji wa vivutio vya utalii wa Kenya, wamechangamka na mafaniko haya mapya ya Serengeti na kwa mujibu wa taarifa za mtandao huo hadi mwishoni mwa wiki hii, zinaitaja Masai Mara kuwa ndiyo imepandishwa hadhi kutokana na kuwa mazingira mazuri ya kuvutia wanyama wa aina tofauti ambao ni twiga, duma, tembo, simba, pundamilia na uwanda mzuri wa makazi ya wanyama.

Ukiacha Serengeti ambayo imeshika nafasi ya saba, jiji la Jerusalem limekuwa la pili kutokana na historia yake ndefu huku majengo ya kifahari ya Potal Palace yaliyopo Tibeti ambayo hufahamika kama majengo ya Malaika kutokana na muundo wake, yakiwa ni ya kwanza.

Maajabu ya tatu ni Polar Ice ambako inapatikana barafu ambayo si ya kawaida, ya nne ni visiwa vya Kaskazini Magharibi vya Hawaii, visiwa vilivyopo Marekani ambayo vimekuwa na viumbe adimu ambavyo ni pamoja na samaki aina tofauti.

Maktaba na ofisi ya mtandao wa Intaneti iliyopo Marekani nayo imechukua nafasi ya sita kati ya maajabu hayo kutokana na kuwa na mfumo na miundombinu ya kutosha ya kupata huduma za mawasiliano ya njia ya kompyuta, vitabu na taarifa mbalimbali za dunia.

Maajabu ya sita ni majengo ya kizamani maarufu kama Mayan Pyramids ambayo nayo yako Marekani na kwamba kura za kuchagua maajabu hayo zilipigwa kwa njia ya kompyuta moja kwa moja na ujumbe mfupi.

Akizungumzia zaidi hilo, Profesa Maghembe alisema hatua ya Tanzania kuanza kupambana na wanaojaribu kuhujumu vivutio vyake vya utalii inaweza kuathiri biashara ya sekta hiyo.

Profesa Maghembe alisema wiki moja iliyopita katika mkutano wa utalii uliofanyika Uingereza ambako alihudhuria, alinadi vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro.

"Tunajua kuna hujuma dhidi yetu, sisi hatuwezi kupamba na wanaoeneza hujuma bali tunaueleza ulimwengu kuhusu vivutio vyetu," alisisitiza Profesa Maghembe.

Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii, Geofrey Tengeneza, alithibitishia gazeti hili ofisini kwake jijini Dares Salaam wiki iliyopita kwamba Serengeti ndiyo imeshinda kuwa moja ya maajabu mapya kati ya hayo saba na bodi itaendelea kuitangaza mbuga hiyo na vivutio vingine.

Wazungu kutoka Ulaya walipofika Serengeti mwaka 1913 walishangaa uzuri wa wanyama, uoto wa asili na walibatiza eneo hilo kuwa ni Peponi, yaani Paradise.

Katika miaka ya 80 mwishoni Tanzania iliamua kufunga mpaka wa Bologonja ambao unatenganisha Masai Mara na Serengeti kwasababu za kiuchumi.

Uamuzi huo ulitokana na uchunguzi uliothibitisha kwamba watalii walikuwa wakiingia Serengeti wakitokea Masai Mara huku malipo yote ya malazi, chakula na kuangalia wanyama yakifanyika upande wa Kenya.

Hatua hiyo ilisababisha mvutano mkubwa kati ya Kenya na Tanzania.
 
Mkereketwa

I very much agree with you. You have made quite an elaborate explanation on your stance of not engaing in creating the EAFU at this moment and have pinpointed very good arguments. While TZ was clinging to the EAC in the 70's, KE deliberately wanted it to go and so it did bringing all the economic consequences.

Some of us who were young men at the time remember. You can see from the boastful posts from our KE neighobours above - that KE is the economic giant in the region. I am quite against this federation as of now. It is a bitter pill to swallow. Political ambitions should be left out.
 
Jamani Watanzania wenzangu mimi ni kati ya wale wanaopinga EAF lakini nimefikiria kwa undani na kugundua kwamba kama tukienda mwendo mzuri na kufanya decision nzuri inaweza kutufaidisha watanzania, hivyo nimekuja na vitu ambayo Tanzania ifanye na vitu ambayo isifanye.

Tanzania ifanye:

1. Barabara na Reli ya Kenda nchi husika ni kitu cha manuhimu hii itatuongezea wala siyo kutupunguzia. Bandari zetu zitaweza kupata tenda na itaongeza biashara kwenye miji ya njiani kama Arusha.

2.Ruhusu wasomi waje lakini kundi mbili tu Walimu na Madaktari, hii itasaidia nchi yetu kwani tunakuwa kwa kasi na hatuna walimu, vilevile kazi ya ualimu hailipi sana hivyo watanzania wamekua wakizimbia kwani masomo na malipo hayalingani. Hatuna walimu wazuri na wazazi wanapoteza pesa nyingi kwenye masomo ya ziada kama "tutions". Madaktari wanakimbia wagonjwa hasa wa ukimwi wamejaza hospitali, vilevile masoma ya udaktari ni ya muda mrefu sana hivyo ruhusu madaktari.

3.Ruhusu Wanachama husika ku invest Tanzania kwenye biashara lakini weka viwango mfano. Kama mwanachama kutoka Kenya anataka kufungua hotel waruhusu kwani hatutakosa chochote badala yake tutapata ajira.

4.Ruhusu na Anzisha michezo ya chuo na sekondari kwa wanajumuia, kama mpira wa miguu n.k hii itaongeza uhusiano mzuri wa baadae kati ya wanajumuia. Vilevile anzisha student exchange kwa mihula ili kuwawezesha wanafunzi kujua wenzio wanasoma nini.

5. Vilevile tufanye mipango ya kuweka ulinzi wa pamoja kama vile rada na askari wa maji.

6. Tanzania inatakiwa kuwapa wananchi wake vitambulisho kabla ya kujiunga na wanajumuia ili tuwe na uhakika je tuko wangapi, tunakaa wapi ili baadaye tuweze kufanya background reference na tuone mwelekeo, lakini kama hata hatuna statistics inakuwa ngumu kujua kama tunarudi nyuma au tunaenda mbele.

Tanzania isifanye na maoni ya

1. Tanzania isitoe tax kwa wanachama hii ni kwa sababu;Hauwezi kuwa na tax free wakati tunatumia pesa tofauti na exchange rate tofauti, hii haimake sense!!.

2.Tusiruhusu watu masikini kuhamia Tanzania maana watu wote masikini watakimbilia Arusha na kuanza kuibia watalii na kufanya ujambazi

3. Ni lazima nchi husika ziwe na sera sawa za rushwa, kama kuna rushwa kenya basi biashara huru haitafanikiwa, ni jambo la aibu kufanya biashara na kufungua border na nchi ambayo imejaa rushwa, hiyo itatuambukiza na sisi tutakuwa watuwa rushwa hata kwenye barabara kama Kenya. Mfano Marekani imefungulia Wacanada kuja free bila visa lakini si mexico kwasababu wana rushwa sana na ni vigumu kuwa control.

4. Tanzania isiruhusu makazi ovyo ya wanajumuia, hii italeta vita kubwa sana.
 
Buddies, as we're now moving into the Federation; I would like to inform all of you that there are so many vacancies in East Africa. These posts are anounced here under Ajira and this' another chance for us online clients to benefit from surfing the net.

Please click here and you will be redirected to the Vacancies section/thread with those posts: Nafasi za Kazi Afrika Mashariki

Regards
 
Tusiogope. Hii itachangia viongozi wetu kuweka mbele maslahi ya taifa dhidi ya maslahi binafsi. Mwendo ni mbele kwa mbele. hakuna kurudi nyuma. Hata kama tukipewa miaka 20 ya maandalizi kwa mwendo huu tulio nao, hiyo miaka 20 itafika na bado tutasema tunaomba miaka 20 mingine.

Cha msingi hapa ni viongozi wa nchi kuweka mikakati sahihi ya mapambano yaliyopo mbele yetu. Maslahi ya taifa dhidi ya mtu binafsi yawe juu ya ajenda. tuchape kazi kwa bidii, tuwekeze kwenye elimu, tuondoe urasimu usio na msingi katika ofisi za serikali. Tujenge displini, tusiwe wababaishaji katika utekelezaji wa majukumu yetu. Wawekezaji wazawa wenye sifa ya kupata mikopo wapewe. Bila shaka tutafika. Hakuna njia ya mkato.

Viongozi wa chama cha mapinduzi wakaribishe michango ya hoja kutoka vyama vya upinzani na waweze kuifanyia kazi.
 
Shirikisho ni zuri kwa Kenya ambao hawana ardhi na wanategemea kuja kuipata Tanzania. tuungane ili iwe nini hasa? kwani tusipoungana tunakosa nini?

Tujaribu kutibu magonjwa yetu nyumbani kabla ya kukimbilia kwa wengine. Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi wana agenda ya kuimaliza bongo kwa shinikizo la nchi za mgharibi ambao kwa muda mrefu walijaribu kuwatumia Tanzania kujineemesha lakini wameshindwa na njia moja ya kuleta ukoloni mamboleo ndio wa kutumia njia hii.
 
Mimi sikubaliani na uharakishwaji wa shirikisho kwani kutasababisha tusiweze angalia mambo ya msingi. Jamani si ilisha semwa "HARAKA HARAKA HAINA BARAKA"?. Kwanza sisi ni waumwa nyoka-EAC iliyovunjika tulipata madhara makubwa ya kiuchumi, lakini cha kushangaza leo tunataka kwenda kasi hiyo bila kuchukua tahadhari.

hakuna aibu kusema wenigne waanze sisi nasi tunakuja kwani wananchi wote wanatakiwa kuridhika na jambo hili. maoni yanayotolewa sasa hayakidhi haja kwani ni watu wachache sana watapata nafasi hiyo. Kwa nini tusipewa nafasi ya kupiga kura ya maoni ili kila mtu apate nafasi ya kufanya maamuzi. Kwanza elimu itolewe kila mmoja ajue tunaenda kufanya nini EAF na tutapata nini. Ndipo tupewe haki yetu ya kikatiba ya kutoa maamuzi kwa njia ya kupiga kura.

Naisihi serikali ya Tanzania iwe makini na uburuzaji unaoweza kutoka kwa nchi nyingine maana hatujui kwa nini haraka iwe kubwa hivyo kwa jambo nyeti kama hili!

Sikubaliani na kuharakisha hili shirikisho kwa kuwanyima wanachi haki yao ya kuamua hatima ya nchi yao.
 
Mwenyekiti Vijana NCCR aenda masomoni



na Happiness Katabazi


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha NCCR-Mageuzi - Taifa, Bahati Tweve, wiki ijayo anatarajiwa kwenda nchini Uingereza kuchukua shahada ya pili katika fani ya sheria.


Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, jana, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo wa NCCR, George Kahangwa, alisema akiwa nchini Uingereza, Tweve atasoma katika Chuo Kikuu cha Coventry, kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Kahangwa alisema, kuondoka kwa mwenyekiti huyo, kunafanya nafasi yake kuwa wazi na Evaristo Haule, ambaye ni Katibu wa Idara ya Itikadi na Mfunzo –Taifa, atakaimu nafasi hiyo.


Mwaka juzi, Tweve, alihitimu shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kuajiriwa na Kampuni ya Uwakili ya Southern Law Chambers.
 
nachukuwa nafsi hii kuwauriza wa tz wenzangu,kuikata rwanda na burundi
hivi kabla ya kuja kwa wakimbizi wa nchi hizo, tanzania hakukuwa na majambazi? mimi nakumbuka kuwa kabla ya watu hao uzambazi ulikuwawepo tz

Mimi binafsi nilifiwa na jamaa zangu kwa sababu ya majambazi , hali hiyo ilitokea baada kuuza pamba, sasa hao warudi na wanyarwada walikuwepo?
jamani tusiwe watafuta sababu, bali tuwe waungwana, acheni kupoteza muda kwa majungu tu . y kama nyinyi hampedi hawo watu, hamuoni aibu?
nyinyi wenyewe mumeowa wanyarwada na warudi sasa leo munawasema tena.

Hivi, mumekosa kazi hadi kujadili hilo swala ambalo sasa naona limekuwa kazi ngumu. sasa nashangaa sana wahangaza sababu wahangaza ni warudi na wanyarwada sasa naomba nao pia warudishwe kwenye nchi zao, nina uhakika kuwa hao watu si watanzania,sababu mimi binafsi nawafahamu sana wahangaza kuwa ni wakorofi na majambazi kwanza walimuuwa padre wa jimbo la Rulenge na hata hivyo wahangaza mimi nawaona tofauti na watanzania wengine ukubali usikubari wahangaza ni wajambazi kabisa neda sokoni kwa kule utaona walivyo wakolofi. sasa neda ukaone kule biharamulo kwenye kijiji cha kasenga waha na wahangaza wanavyo katana mapanga hadi watu wapaita cosovo sababu ya ukolofi wao kama huamini neda kasulu uone waha wanavyo pigana kutukanana kama vichaa je kule msoma ,
bali
 
to the citizens of Uganda,Tanzania who are pushing for the exclusion of Rwanda,Burundi from the EAC i got news for u.Tiny Rwanda has currently the second biggest economy in East Africa after Kenya.Exactly,they Rwandans are up an gone.So Tanzanians u not doing the Rwandans any favour by letting em join the union.

They doing u a favour.Kenyans know this, an that's why Rwanda's main trading partner is Kenya though we don't share a common border.The Tanzanians will keep on hating the Rwandase,the Ugandans wanna play the regional power 2gether with the Ethiopians while the Rwandese an Kenyans do bizness.
 
So if Rwanda and Kenya are far ahead what has that got to do with us. It is good for them and good luck.

We don't want the union period!
 

WEWE NI MRUNDI AU MNYARWANDA, LUGHA YAKO INAONEKANA WAZI. WAWEZA KUSEMA CHOCHOTE NI HAKI YAKO. TUNAWAHESHIMU NA KUWAPENDA KAMA JIRANI ZETU, LAKINI SHIRIKISHO NA NINYI HATUTAKI KWA SASA. KAENI HUKO KWENU NA UKABILA WENU WA UHUTU NA UTUTSI. MTAKAPOMALIZA TOFAUTI ZENU HIZO NJOONI TUTAWAFIKIRIA, LAKINI SI SASA, HATUTAKI MATATIZO YENU MTUAMBUKIZE SISI.
 
Sisi ni Makanda wa jeshi wastaafu tunatoa taazari kwa rais na wananchi wa tanzania hatutaki shirikisho hii kauli haita rudiwa full stop. toeni elimu kwanza hakuna elimu hakuna shirikisho.

Viongozi mumezoeya kuburuza wananchi mimi ninaojua system nzima nimepigana vita dunia nzima, tunaipenda nchi yetu tanzania mungu ibariki tanzania......
 
I am starting by asking questions that will only bring meaning to you when you have perceived the whole concept of the community.Marriage:we tend to admire the succesfull commitments of such people that celebrate 50,25 10 or even 5 aniversaries of those couple that say YES we have achieved these years together, thus the commitment, love patience towards each other containing each others weaknesses.

Do people simply dissolve companies when failure occurs in their commitment toward making a profit or do they struggle toward making it a success.

Who were the major players in the fall of the community? are they alive or was there a foreign intervention toward this break that when these three nations succeed will pose a threat to the region.

The fall of the community was based on differences of peoples opinions in leadership, planted in the peoples minds by the same leaders and causing hate amongst each other.

This fall was so disastrous that it left tanzania behind, kenya economicaly good and uganda politicaly in chaos.

What do we learn from this failed marriage? Alot is being said about how Tanzania is in fears of the past marriage, Uganda and kenya are more than prepared to move forward.This new community is Not a husband and wife situation ,it is a partnership that is here to stay. for the benefit of all the East Africans.

Being prepared is what is required.Competition is what we anticipate seeing in the near future giving a slow runner pace to catch up at what ever time it take he/she will egt there.

Alot is being talked about the education sector leaving Tanzania colleagues not competitive enough to kenyan or Ugandan teachers, But how did these two get where they are today without competing towards each other and what is this going to benefit your children in that context.

The flow of business between these three countries is unmeasurable.The Ugandan clollegues who never wanted to Speak Kiswahili are not only forced to use it in order to negotiate discounts and other services but even taught in schools , hopefully very soon will be a compulsory subject.

The leadership of the Failed community was then in the hand of the lofty hands of the greedy leaders but now i would like the people to have more power in the leadership of the community.The represatation of bodies that govern general bodies in business health and other areas of interest be given a seat at the community level, because those bodies deal directly with the people and they present views that are sent in by the people themselves.

May i say to you all fellow East African that anniversies of or community will only be celebrated if we look only at positive achievements of the future and not to entangle our selves with the past failures giving us a slack, slow start of the community with a single currency like the euro for the European Union for the Europeans, The USA for the north Americans and anyother sort of comunity you might be knowing that i havent mentioned .
May god bless President. J. M. Kikwete, President Y. K. Museveni and President M. Kibaki and i strongly pray for the success of this community, preside over East Africa.God Bless you all

Baptist J Mutesasira
East African
+447944268259
 

Kwa uliyosema mh Kabwe (au bwana mdogo Zitto kama nilivyokuwa nikikuita pale Mlimani UDSM) nakubaliana na wewe kuhusu shirikisho la kiuchumi, na ninaweka msisitizo huo huo wa kwako kwenye MASOKO. Lakini kwenye shirikisho la kisiasa NAKATAA kabisa na sitaki kuona kwa sasa nikiwa chini ya serikali moja na hawa jamaa, ni balaa tupu.

Hawa jamaa kina Kony wa Uganda na wale waasi wa DRC vita yao haijaenea kwetu kwa sababu kuna mipaka ya kiutawala na kisiasa ya hizo serikali wanazopinga. Ingekuwa tuko katika utawala mmoja na hao jamaa pangechimbika hapa na pasingekalika, ni nuksi kabisa hao jamaa. Tufanye nao biashara, inatosha, lakini shirikisho la kisiasa NO!
 

Mawazo mazuri, nami nakubaliana nawe. Tumewashika mkono siku nyingi, tuliwapokea wakimbizi miaka mingi, wameishi Uganda, Tanzania (kwa wingi sana) na hata Kenya. Tumewafanyia hisani ya kutosha, na huu naamini ndio ujirani mwema. Lakini viumbe wazito hawa, hawabebeki! Wajirekebishe kwanza kasoro zao hizo za ubaguzi waishi kama binadamu, hapo itafaa kuishi nao kwenye shirikisho.

Kwa sasa msaada tunaowapa wa makambi ya wakimbizi unatosha. Haifai kuwaruhusu watu hawa kutembea nchini kama raia, fujo zote watatuletea. Wakae huko kwenye makambi tutawadhibiti huko. Wakishapata amani nchini kwao warudi, wakajenge umoja wa taifa lao kwanza ndipo watapata sifa ya kujiunga na mataifa mengine yenye umoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…