Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
BURIANI TANZANIA ... AU KILA LA HERI AFRIKA MASHARIKI?
Na Mlenge Fanuel
"Mtu akikushauri jambo la kijinga, huku anajua jambo hilo analokushauri ni la kijinga, na wewe ukakubali, basi atakuona, wewe zuzu!"
-- Mwalimu Julius K. Nyerere, 1994/5
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali isome barua hii ya wazi ya kukufikishia ujumbe kwamba Tanzania haiko tayari kujiunga na Shirikisho la Afrika Mashariki (East African Federation, EAF) wala Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, na kwamba Watanzania hatutaki Tanzania ijiunge na Shirikisho hilo.. Yatakuwa ni maafa makubwa kwa Tanzania na Watanzania iwapo Tanzania itajiunga na EAF hasa kwa mpangilio ulioko wa fast track. Ndiyo maana nimeanza na nukuu ya Mwalimu Nyerere, ambaye tayari baadhi ya watu, hasa wa nchi MIMI NAONA HUU NI UOGA WA KUTOINGIA HII JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI HAWA JAMAA WAKENYA WAGANDA NA WARUNDI WATATUCHEKA TUNAWAOGOPA KWANI SISI NI MBUMBUMBU KIASI GANI TUNYANG`ANYWE ARDHI? HUU NI UOGA WA KUSHINDANA TU NA HAWA JAMAA KINGEREZA KINATUPIGA CHENGA NA HAYA MAJAMAA MAKENYA MAGANDA NA MATUSI YAMESOMA SANA KULIKO MAMBUMBUMBU MENGI YA KITANZANIA. SASA UOGA UMEZIDI INATUBIDI TUJIFUE NA SISI TUHIMIZE WATOTO WETU WENGI WAINGIE SHULE, HUU MUUNGANO NI BORA UFANYIKE MAPEMA ILI KUTUWEZESHA SISI WATANZANIA KUWA NA USHINDANI KIBIASHARA NA KIELIMU PIA. KUJI ISOLATE HAKUTO TUSAIDIA KITU KWANZA TUNA EXPERIANCE KUBWA YA MUUNGANO HIVYO HAWA JAMAA WATATUTEGEMEA SANA KATIKA MAMBO MUHIMU. KIKWETE HALAKISHA HUU MUUNGANO IKIBIDI KABLA YA MWAKA UJAO TUWE NCHI MOJA...KWANZA WATU WENGI WATAFANIKIWA KUSOMA UGANDA AMA KENYA KWENYE ELIMU POA NA WENGINE KUJIFUNZA KIFARANSA NA KUWA MAKINI KATIKA BIASHARA KAMA HAYA MATUSI THEN KESHO TUNAWEZA KUICHUKUA NA SISI NCHI YA MALAWI ILIYO DOLORA KAMA SISIjirani za Kenya, Uganda na Rwanda, wameanza kumsingizia kwamba kwa kujiunga na EAF tutakuwa "tunamuenzi" Mwalimu Nyerere, huku wakijua fika ushauri wanaotupa wa kujiunga na Shirikisho na Soko la Pamoja la Afrika Mashariki hauna manufaa yoyote kwa Tanzania, wakidhania sisi Watanzania ni mazuzu tunaoendekeza wema wa mshumaa kuwaangazia wengine huku wenyewe unateketea, kwa minajil ya kupata misifa isiyo na tija.
Ni kweli Mheshimiwa Rais umeunda Tume ya Kupokea Maoni kuhusu Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini inatia mashaka iwapo huo siyo tu ni utaratibu uliouweka kuhalalisha maamuzi yaliyokwishafikiwa ya kuidumbukiza Tanzania kwenye EAF. Hii inatokana na muonekano kwamba Tanzania kujiunga na EAF kumeshaamuliwa tayari -- kutaka watu tujadili siyo kiinimacho tu? Mheshimiwa Rais, palikuwa na muswada uliopelekwa Bungeni wa Tanzania kujiunga na EAF, ambao Waheshimiwa Wabunge waliukataa, na serikali ikabidi iuondoe. Lakini mchakato wa Tanzania kujiunga na EAF ukaendelea tu, na kupuuza maoni ya Wabunge wetu tuliowachagua watuwakilishe. Ikiwa sikusikiliza vibaya, katika Bunge la Bajeti 2006/2007, Mheshimiwa Waziri wa Afrika Mashariki aliliambia Bunge kwamba patakuwa na KURA YA MAONI kuhusu Afrika Mashariki. Matokeo yake tumeletewa Tume badala ya kura ya maoni! Kana kwamba hiyo haitoshi, iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa wewe Mheshimiwa Rais wetu, ulimhakikishia Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwamba utafanya kila unaloweza kuhakikisha kufanikiwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki, kwenye mkutano wenu uliofanyika Mwanza. Je, maoni tunayotoa Watanzania kukataa kujiunga na shirikisho si "kilio cha samaki -- machozi yanakwenda na maji?" Wenyewe "wenye nchi" mshaamua mloamua?
Pana maswali mengi mheshimiwa Rais ambayo ukitupatia majibu utakuwa umetuwezesha Watanzania tulio wengi kuelewa kuhusu mustakabala wa maisha yetu na Tanzania yetu:
* Je, Ni sera ya CCM Tanzania kujiunga na EAF au Soko la Pamoja la Afrika Mashariki?
* Je, Ilikuwa kwenye ilani ya Uchaguzi 2005 ya Chama Tawala CCM Tanzania kujiunga na EAF?
* Je, Nani aliyependekeza Tanzania ijiunge na EAF? (Inabidi tumfahamu ili tuweze kumpamba maua iwapo Tanzania itafanya tunalodhani ni kosa la maisha la kujiunga EAF kumbe ikathibitika EAF ni manufaa tele kwa Tanzania ; vinginevyo inabidi tumfahamu ili tuweze kumzomea na kumuimbia nyimbo za kumsimanga pindi machungu ya EAF yatakapoanza kudhihirika muda si muda iwapo Tanzania itafanya kosa la maisha kujitumbukiza kwenye EAF. Vinginevyo itakuwa kama mikataba ya madini -- hatuelezwi nani aliwaalika na kuingia mikataba na 'wawekezaji' kwenye migodi.)
* Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshajitangaza kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki -- ikiwa na maana yote mengine yanayojitokeza sasa ni kuhalalisha na kusafisha njia ya Museveni kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki, hasa ukitilia maanani Rais wa Kenya na wewe Rais wetu mko kimya, ikielekea mmekubaliana na matamshi ya Museveni. Si hivyo?
* Kutokana na maneno yanayosemwa na Wakenya na Waganda, Wanyarwanda na Warundi, inaonekana kama vile serikali ya Tanzania HAINA UBAVU wa kusema HAPANA kwa EAF -- kila mara Tanzania inazomewa inapohoji maslahi yake kwenye EAF -- au inapotaka kutumia uhuru wake ISIJIUNGE na EAF. Hivi karibuni Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania alisemwa kwenye vyombo vya habari kwamba hahudhurii vikao vya Afrika Mashariki -- na kumfanya Mheshimiwa Waziri Mkuu ajitokeze kumtetea -- na baadaye Waziri yule akaondoshwa toka Wizara ya Afrika Mashariki kwenye mabadiliko ya Baraza la Mawaziri uliyoyafanya hivi karibuni Mheshimiwa Rais. Ina maana Tanzania ni kama mbwa anayeelekea kwenye mdomo wa chatu EAF -- amefyata mkia, anatoa kilio cha mwisho, na hana la kufanya zaidi ya kufanywa asusa na kumezwa -- au si hivyo?
* Ni kwa nini Kiswahili SIYO lugha rasmi EAC, na badala yake ni kiingereza?
* Kama shida ni ushirikiano, kwa nini Tanzania isijiunge na Msumbiji na Zambia , na kutengeneza shirikisho?
* Kwa nini EAF inaharakishwa namna hii?
* Ni nini Tanzania inahitaji kwenye EAF ambacho haiwezi kukipata bila kuwemo kwenye shirikisho hilo ? (Mbali na ngonjera za kisiasa, pengine na watu fulani kupata posho za vikao vya EAC na baadhi kuandikwa kwenye vitabu vya historia, vitu ambavyo havimsaidii Mtanzania mpiga kura wako anayesubiri neema tele na maisha bora...)
* Pana bidhaa zipi za Tanzania hazifiki kwenye soko Kenya au Uganda , ambazo EAF itazifanya zifike sokoni?
* Nani atakuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Afrika Mashariki, na ni upi mchango wa EAF kwenye uvamizi dhidi ya DRC?
* Mheshimiwa Rais, hivi "Usalama wa Taifa" wa Tanzania una majukumu gani makubwa zaidi ya kulinda (uhuru) "Sovereignty" ya nchi yetu? Kwa nini "Usalama wa Taifa" haukupi picha kamili ambayo itakufanya usijisumbue hata kuja kutuuliza iwapo tunataka uhuru wa nchi yetu uondoke kupitia "soko la pamoja" na "Shirikisho la Afrika Mashariki", badala yake tukaendelea kulijenga taifa "letu changa" na kuulizana maswala ya maendeleo kama vile tutanufaikaje na maliasili tulizojaaliwa nchini m
MIMI NAONA HUU NI UOGA WA KUTOINGIA HII JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI HAWA JAMAA WAKENYA WAGANDA NA WARUNDI WATATUCHEKA TUNAWAOGOPA KWANI SISI NI MBUMBUMBU KIASI GANI TUNYANG`ANYWE ARDHI? HUU NI UOGA WA KUSHINDANA TU NA HAWA JAMAA KINGEREZA KINATUPIGA CHENGA NA HAYA MAJAMAA MAKENYA MAGANDA NA MATUSI YAMESOMA SANA KULIKO MAMBUMBUMBU MENGI YA KITANZANIA. SASA UOGA UMEZIDI INATUBIDI TUJIFUE NA SISI TUHIMIZE WATOTO WETU WENGI WAINGIE SHULE, HUU MUUNGANO NI BORA UFANYIKE MAPEMA ILI KUTUWEZESHA SISI WATANZANIA KUWA NA USHINDANI KIBIASHARA NA KIELIMU PIA. KUJI ISOLATE HAKUTO TUSAIDIA KITU KWANZA TUNA EXPERIANCE KUBWA YA MUUNGANO HIVYO HAWA JAMAA WATATUTEGEMEA SANA KATIKA MAMBO MUHIMU. KIKWETE HALAKISHA HUU MUUNGANO IKIBIDI KABLA YA MWAKA UJAO TUWE NCHI MOJA...KWANZA WATU WENGI WATAFANIKIWA KUSOMA UGANDA AMA KENYA KWENYE ELIMU POA NA WENGINE KUJIFUNZA KIFARANSA NA KUWA MAKINI KATIKA BIASHARA KAMA HAYA MATUSI THEN KESHO TUNAWEZA KUICHUKUA NA SISI NCHI YA MALAWI ILIYO DOLORA KAMA SISI