Alionekana kuwa na mengi ya kuzungumza, lakini alifikia mahali akazidiwa na jazba, akakatiza maoni yake kwa hasira.
Butiama: Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, yeye alikuwa na maoni yake.
Dk. Kamala alipata fursa ya kwenda kusalimiana naye, akianzia kanisani alikoshiriki naye misa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Butiama.
Baadaye alikwenda nyumbani, na kabla ya mazungumzo, Dk. Kamala alipata fursa ya kwenda kuhani katika kaburi la Mwalimu
Katika mazungumzo yao, Mama Maria alishauri Burundi na Rwanda zikubaliwe kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Msimamo huo wa Mama Maria ni mwendelezo wa filosofia ya Mwalimu aliyeamini katika umoja wa Afrika.
Mama Maria alisema ni jambo la busara kwa nchi wanachama wa EAC, kuzipa uanachama Rwanda na Burundi.
Amesema matatizo ya ukabila na mapigano yanayojitokeza katika mataifa hayo, yanaweza kupunguzwa au kumalizwa kwa kuziruhusu nchi hizo kujiunga katika jumuiya hiyo.
"Nadhani Rwanda na Burundi zikiingia kwenye jumuiya, zitaweza kupunguzwa matatizo ya ukabila na vita.
"Watajifunza kutoka kwetu na wataweza kuishi kwa amani, hawa tuwakubali kwa sababu bila hiyo wataendelea na vurugu na hivyo sisi tutaendelea kuwa na mzigo wa wakimbizi? Alisema.
Hata hivyo alisema suala la kuzikubali nchi hizo kuwa wanachama linapaswa kushulikiwa na taratibu zilizopo zikiwamo kama hizo za kukusanya maoni ya wananchi.
Sirari: Maoni katika miji ya sirari na tarime, mkoani Mara hayakuwa tofauti na sehemu nyingine. Wapo waliopendekeza nchi hizo zikubaliwe kujiunga EAC, lakini wengine walipinga kwa nguvu zote.
Katika mkutano wa hadhara mjini Sirari, Daniel Marwa alisema "Hawa watu (warundi na wanyarwanda) wakubaliwe kuingia, kama ni wakorofi waache waje, watajifunza kutoka kwetu"
Kuhusu shirikisho wengi walichagia walitaka kwanza elimu itolewe kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba wapo wasiojua hata maana ya shirikisho, faida na hasara zake.
Walipendekeza kwamba katika kuelekea kwenye shirikisho nchi wanachama wa EAC hazina budi kwenda hatua kwa hatua.
Kuhusu Rwanda na Burundi kukaribishwa EAC, wengi walipinga, wakisema bado zimegubikwa na Uhutu na Ututsi. Wengi walichagia walipendeza utolewe muda na masharti kwa nchi hizo kabla ya kukubaliwa uanachama.
Mjini Musoma, Dr. Kamala alifanya mkutano, na viongozi wa vyama vya siasa, madhehebu ya dini, mashirika yasioyo ya serikali, asasi na wadau mbalimbali.
Miongozi mwa wachangiaji alikuwa ni Moses Zefania, ambaye alisema kama Rwanda na Burundi zina sifa zikaribishe kwenye jumuiya.
"Afrika sasa ifikirie kuungana, tusiangalie tofauti zetu," alisema Zefania.
Naye Kalaine Kunei alipendekeza mipango ifanywe ili shirikisho la Afrika mashariki lianze haraka.
Mwanza: Mkoani mwanza Dr. Kamala alifanya mkutano katika Ukumbi wa Halmashauri wa jiji hilo. Kama iliyokuwa Musoma, mkutano wa Mwanza ulihudhuriwa na wadau wa kada mbalimbali, wakiwemo wanasiasa wa vyama mbalimbali, wakiwamo wanasiasa wa vyama mbalimbali, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wafanyabiashara, viongozi wa asasi na kadhalika.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema "Shirikisho hatuwezi kulikataa, lakini kwanza Watanzania watambuliwe, wapewe vitambulisho, nchi hii yeyote anaingia tu"
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Hassan Ferej, pamoja na mambo mengine mengi aliyozungumza alisema huu ndio wakati wa kuungana.
"Wakati huu ndiyo wa kuungana, watanzania pekee hatutafika popote," alisema.
Moses Methew alitadharisha kwa kusema tunapaswa kuwa macho kwenye shirikisho ili ajira zisitishie kwa wageni tuu.
"Tumejiandaa vipi kulindaa ajira? Tuangalie tusiwe wasindikizaji tuu," alisema.
Rusumo: Rusumo ni mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Ni sehemu ya wilaya ya Ngara.
Waliozungumza walionekana kupinga Rwanda na Burundi kukaribishwa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Jumuiya yoyote lazima iwe na maslahi kwa wananchi, Hawa tunawakaribisha tutapata nini kwao? Sijaona bidhaa zao, isipokuwa vyuma vichakavu na viazi kutoka Rwanda. Hakuna tunachoweza kupata kutoka kwao?
"Tanzania iwe ya Watanzania, Tusiwe kama Kosovo ambao waliruhusu wageni, kisha wageni wakaanzisha himaya yao", alisema mchangiaji.
Wananchi wanashaka na Rwanda na Burundi, wanasema Wananchi katika nchi hizo hawajatulia, wana mifugo mingi, tukiungana si tutamezwa? Shaka kubwa ni hali ya Kisiasa?
Katibu tawala wa wilaya ya Ngara, naye alikuwa na maswali kadhaa.
"Jumuiya itahusishwa maeneo gain? Kama Tanzania, Kenya na Uganda kuna kutoelewana, kuna sababu ya kukaribishwa Rwanda na Burundi?
Sisi tungesubiri kwanza hadi sisi tuwe tumeelewana?
"Tukiungana hivi hivi, tunaweza kuwa daraja la wengine kujinufaisha," alisema
Mrongo: Eneo la Mrongo ni maarufu. Lipo wilayani karagwe Hapa ni mpakani mwa Tanzania na Uganda miongozni mwa mambo yanayolifanya eneo hili liwe maarufu ni ukweli kwamba hapa ndipo Yoweri Museveni alipoishi wakati wote wa harakati za uasisi, na hatimaye kwenda kumngoa nduli Idi Amini.
Katika kijiji cha mrongo Rais Museveni alitoa fedha ili ijengwe shule kijijini hapo. Walaji wa Kitanzania wakazitafuna. Hakukata taama. Katoa fedha nyingine alichofanya sasa ni kuleta mafundi na wasimamizi wake. Shule inajengwa na ni ya kisasa.
Dr. kamala alifanya mkutano katika eneo hili kuzungumzia EAC.
Mwananchi wa kwanza kutoa maoni alikuwa ni Daud Karoli. Aliyesema "Ingawa Rwanda na Burundi ni ndugu zetu, tusubiri, bado wana matatizo makubwa. Wana vita na ukablia, Wakitulia ndipo tuwaingize kaitka Jumuiya."
Mwananchi mwingine ambaye jina lake halikupatikana alitetea kwa kusema Rwanda na burundi wanapaswa kuingizwa sasa.
"Tusiwe na wasiwasi, kila nchi itaendelea kuwa nchi na mipaka yake, udhibiti ule ule, hatuwezi kuwaacha wanagambana, wanapigana na kuuana, ni vizuri tuwaingize kuna sababu za wao kujiunga.
Ni ndugu zetu. Waafrika wenzetu, sheria zitabaki zile zile" alisema.
Ofisa Mifugo aliyejitambulisha kwa jina la Charles, alisema "Hapa tunahukumiwa na historia Watawala wa Rwanda na Burundi alikuwa tofauti na watawala wa Tanzania, Kenya na Uganda.
‘Tuwascreen tutaona matatizo yao, ikiwezekana ndipo twakaribishe," alisema
Mhifadhi wa Wanyamapori, Francis Chuwa, alisema "tunaruhusu wajumuike kwenye muungano, vita vya majirani zetu hawa inawezekana ni subject, bora waingizwe.
"Tukiungana nao, wataona aibu kuona wenzao hawagombanim turudie Uafrika wetu. Hii mipaka ni ya kikoloni, tukae pamoja," alisema Chuwa.
Jackson John, naye alikuwa na maoni yake. "tukiwaruhusu waingie, lakini serikali yetu iongeze bajeti ya ulinzi hasa baada ya kuwaingiza Rwanda na Burundi."
"tumeingia dhamana kutokana na mitafaruku yao,"
Dr. Kamala pia alipata fursa ya kukusanya maoni ya Wananchi wa kata ya Isingiro, wilayani karagwe, kwenye mkutano wa hadhara.
Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Sweatbet, alisema "Rwanda na Burundi zisingizwe, wana vita hawajui Kiswahili, wakiingizwa wataleta migogoro.'
Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Paul, alisema "Burundi na Rwanda wasishirikishe, ni watu wa vita na kuuanna, akiungana na sisi watafundisha watoto wetu vita, tutakuwa na umwagaji damu."
Maoni kama haya yalitolewa na Deogratius Maiko" Naomba Rwanda na Burundi wasiingine kwenye jumuiya, ni wakabila, wanajali Ututsi na Uhutu, kazi yao ni kushitakiana arusha."
Hata hivyo felisa Chrysostom, ambaye alionekana kuwa na asili ya Rwanda alikuwa na maoni tofauti.
"tuwashirikishe kwenye jumuiya, tumezaa nao, ni wenzetu wana shida. Tukiwakaribisha tutawafundisha," alisema na kuzomewa na umati uliohudhuria mkutano huo mkubwa.
Kasulu: Mmoja wa maofisa wa JWTZ, alimweleza Dk. Kamala kuwa suala la Burundi kukaribishwa kwenye jumuiya, linapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu.
Yeye anapendekeza Rwanda waruhusiwe lakini Burundi wapewe muda kwanza
"Hawa wasubiri, vinginevyo tutabeba mzigo wao," anasema
Maoni kama haya yaliyotolewa na Freddy Baraza, kwa kusema "Tuziache Rwanda na Burundi, "wamalizana kwanza" (wachinjane)."
Mchangiaji mwingine Thobias, alisema "Tuwapime kabla ya kujiunga EAC, tuhakikishe kwanza wana amani ya kudumu, tukiwaruhusu sasa. Tutaleta matatizo."
Na HabariTanzania.com -
http://www.habaritanzania.com/articles/1837/1/