East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

"Now my TZ bros and sisters, ask yourselves, why is the entire region unhappy with your 'unfriendly' behaviour? Although on face to face you deceptively project a differrent picture;
A POLITE REQUEST PLEASE: DO NOT USE ABUSIVE LANGUAGE WHILE RESPONDING TO THIS ARTICLE. E.G MJINGA, NYANGAU, MSHENZI "


Is it true that the entire region is unhappy with the so called 'unfriendly behaviour' by Tanzanians? By the way who started all this? So, the behaviour of the Kenyans towards Tanzanians is friendly and is smelling rose!

See this, "Do not use abusive language while responding to this article e.g. mjinga, nyang'au, mshenzi". Hahaha.aaaaaaah. Oh God, this is the invisible man. Just hear his language...mjinga, nyang'au, mshenzi. What a resemblance to one posting in this forum? Ameshindwa au amesahau kujificha.

Mtoto akililia wembe mpe. Mlianza matusi, mumejibiwa kwa matusi, sasa mnalalamika. Ndiyo maana sisi watanzania tunasema uungwana na utu ni mambo muhimu na yanayotakiwa katika eneo hili la Afrika Mashariki. Tushindane kwa hoja na siyo kwa "arrogance" ambayo nyinyi eti mnaiita "confidence". Mwishowe wizi mtaita kuazima.
 
Asante ndugu yangu kaka/dada Un-registered. Kwakuwa uhuru wa kuchangia bila kujisajili ndo unapelekea kudharauliana nadhani kwa sasa tusitishe kwa wasiojisajili kuchangia humu

Lugha yoyote ya KEJELI, MATUSI, DHIHAKA, KASHFA ISIYO NA UTHIBITISHO, na vingine vyote vyenye dhamira ya kumdhalilisha mwenzako havitovumilika.

Mimi ni Mtanzania (Tena nipo Bagamoyo). Siwezi kuandika matusi yote kwani mengine kuyaandika hayapendezi kabisa kwa mtu mwenye heshima yako. Mi binafsi kumwita mwafrika mwenzangu Nyang'au au idiot au matusi ya aina hii siwezi... Naona aibu kabisa! Si desturi yangu!
 
Unregistered said:
As a Kenyan i'm glad the Tanzanians are anti-EAF though it's sad they think we're shyt piled several feet high.An EAF is one step closer to global gorvernance coz somehow it gonna be easier to incorporate the fed into the New Age agenda.Yeah,i'm a cospiracy nut.Big deal.The hell i wanna be an East African Federation citizen nor an African Unionist crap nor Global citizen.Rather be Kenyan,Kenyan,Kenyan all through with all the shyt it's associated with,including Kibera.Bongo is cool though, with all the music and stuff.Music capital of East Africa,but do they say.Wish i could speak some bongo Swahili so i could get a leg up on the ladies.Economic union is fine but political
union????wtf???Wabongo nawasihi wacha matusi.Waganda stop bombing our Karamoja citizens pronto.Na hiyo ni maendeleo.Meanwhile Kenyans we got monster fish to fry when it comes to Somalia BS and them Ethiopians who invade Marsabit whenever they feel like.But then,What do i say?

Hakuna noma.


LOL... but kijana; the federation will still happen with or without the fightings etc.....I have not heard the tanzanian intellectuals (proffesors, doctors etc)saying that they do not want EAF.... If anything they have been silent knowing that it is a good thing to have EAF.
Balozi
 
TzPride said:
I hate no body, but I hate ignoring some vital facts. EAF will not work, especially if Tz and Ke will be the members. Alot have been said in here, so let's forget this idea. I swear, if our leaders will force us into EAF with Ke a member, I will lead a group of wazalendos to regain Tz freedom. Tz and Ke are incompatible completely, civil unrest is inevitable.

Hivi kweli mwaweza ungana kama hamuelewani? Ati tutaelewana mbele kwa mbele. Sitaki sikia hadithi za akina Mangungo wa Musovero enzi hizi.Period! JK upo mkuu wetu? Changamoto hiyo.


TZPride
You are being ignorant in the sense that remember each of the three countries will remain as a sovereign state... the only thing that we shall have in common is that we can now trade more freely between the three countries and moreover there will be a parliament comprised of both KE, TZ and UG and all your views no matter which country you come from will be heard in the said parliament.
Balozi
 
Kwa kuwa wakenya wanahitaji TZ kuliko TZ inavyowataka na kwa kuwa walituibia mwaka 1977, kwa nini tusiwawekee masharti kwamba kabla hatujaingia kwenye federation lazima wao wafanye reparations. Yaani warudishe zile mali walizoziiba kwa nguvu kabla ya community kufa halafu ndiyo tuanzae upya?

Halafu watuombe msamaha na waruhusu TZ ikalie bandari ya mombasa na kukusanya ushuru mpaka zile mali walizozidhulumu zilipwe kabisa na hasara ambayo Tanzania iliipata iweze kusawazishwa?
 
Asante kwa wazo lako zuri la reparations. but i think it wont work coz kenyans have already paid for the collapse of old eac. Not for 'wizi' as you would like to call it but for compensation of infrastructure some of which tz REFUSED to be put up.. eg earth satellite station. dont get me wrong, i believe tz is the richest of all eac countries & the super power, if you would like to call it, and do not need to be compensated..its kinda demeaning...

As we speak the you may be aware that tume flani mwaka ya thamanini ili kadiria pesa ambazo kenya ililipa Tz kama reparations. Sasa hivi bado terms of trade kati ya tz na ke yako lopsided sana in favor of tz. je wajua tz waweza export chochote kenya bila kutozwa kodi? ilhali kenyan goods are still taxed. Even traders wadogo wadogo bado taxes wanalipia katika border crossing.

As regards the debate, i think the masses have spoken..the decision is unanimous..no to EAC or EAF or EA Customs Union. Lets remain separate, watu warejee mwakwao, all investments zirejeshwe (or nationalised as the case may be). we shall all remain in peace otherwise itakuwa vita.

asante
 
"LOL... but kijana; the federation will still happen with or without the fightings etc.....I have not heard the tanzanian intellectuals (proffesors, doctors etc)saying that they do not want EAF.... If anything they have been silent knowing that it is a good thing to have EAF.
Balozi"

Bwana Balozi, I am also among the intellectuals (najifagilia mwenyewe). I don't like this monster political federation. No...No. No. Haiwezekani tuungane. What for? Hatuwezi kufanya kosa tena. Nimesoma mtanzania mmoja akisema kuwa ikitokea tukaungana ataanzisha kikundi cha wazalendo cha kupigania uhuru wa Tanzania. Mimi siyapuuzi mawazo ya aina hiyo. Tunakaribisha machafuko katika eneo hili la AFRIKA. Shirikisho la kisiasa BIG NO. HUwezi kuungana na watu wanaokuona wewe ni takataka. Haiwezekani. Kila mtu abaki kwake katika nchi yake.
 
Kutokana na watu kutumia vibaya nafasi ya kuweza kutuma maoni yao bila kujisajili tumeonelea ni vema wanaochangia wakubali kuwa members wa hii Forum. Tunapata wakati mgumu kufuta threads zenye matusi au kashfa. Wanachama wetu hawana jadi hii hivyo ukijiunga nasi utakuwa unakubaliana na kanuni zetu.

Haturuhusu kashfa, usajili wa majina mabaya, matumizi ya lugha za matusi n.k. It's easy... Just click on Register and get registered.

Your registration needs no REAL DETAILS but you better remember your password. We value you!

Now click here to register (1min action):- https://www.jamiiforums.com/register.php?
 
Wananchi wengi, hata wasiotarajiwa, wana mawazo kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ni chombo kinachoihusu mikoa ya kaskazini mwa nchi yetu.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Mara, Mwanza na Kagera. Kwa nini dhana hiyo imejengwa? Dhana hiyo imejengwa kutokana na imani kwamba wanaopakana na Kenya na Uganda, ndio wanaohusika na EAC.

Ndiyo maana katika mazungumuzo, wengi wamekadiri kuhoji uhalali wa viongozi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufanya ziara katika mikoa ya kati. Nyanda za Juu Kusini, au mikoa ya Kusini mwa Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Hawana habari kwamba athari au faida za EAC, ni athari kwa nchi nzima. Kwa sababu hiyo, ziara ya kuwaelimisha wananchi kuhusu EAC, ni jambo lisiloepukika, kama kweli serikali imenunia kuwashirikisha wananchi katika mchakato mzima.

Katika ziara hiyo, mambo mengi mno yalijitokeza, lakini lilikuwa na mvuto, pengine kuliko wengi, ni la Rwanda na Burundi kupewa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wananchi wengi walitoa maoni yao, na kwa hakika, wengi hawakupendelea sana nchi hizo zikaribishwe.

Katika maeneo yote, karibu asilimia 95 ya walitoa maoni, wamepinga Rwanda na Burundi kupewa uanachama EAC kwa sasa.

Kimsingi, wanataka nchi hizo zipewe uanachama baada ya kutekeleza masharti kadhaa muhimu.

Msingi mkuu wa hoja zao umejengwa juu ya hali ya ukabila, vita na mauaji, si tu yayoendeshwa sasa nchini Burundi, bali hata nchini Tanzania ambako ujambazi, uporaji na mauaji, yamekuwa matukio ya kutisha.

Katika mapori ya Buringi, Buhiramulo, Nyakanazi, Kibondo, Kasulu na maeneo mengi ya magharibi mwa Tanzania, magari sasa yanasindikizwa na askari wenye bunduki, wakiwa tayari kwa mpambano na majambazi ambao wanadhaniwa kuwa wanatoka Rwanda na Burundi.

Mauaji, uporaji na uhalifu mwingine, vimewafanya Watanzania waishio mipakani, wawachukie mno Wanyaruanda na Wanarundi.

Hali hiyo, ikichangiwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambayo Watanzania walio mipakani walishuhudia maelfu ya maiti, yanawafanya Watanzania wakose imani kabisa na Rwanda na Burundi.

Karibu wananchi wote walizungumuza, isipokuwa wachache, wameonyesha wazi kutaka umoja, lakini msititizo umekuwa kwamba lazima kwanza nchi hizo zitelekeze masharti muhimu.

Watanzania wanajua vizuri zaidi athari za wakimbizi kutoka nchi hizo, pengine kuliko Waganda na Wakenya, kwa kuwa wapo mbali kijiografia.

Kwa msimamo unaoonyeshwa na wananchi hao, inawezekana Wakenya na Waganda wakawashtumu Watanzania kwa kutaka kuwachelewesha mambo.

Kwa wananchi hao, suala la ujambazi na uhalifu mwingine nchini, limesababishwa na wakibmizi kutoka Rwanda na Burundi.

Mjini Kasulu, Dk. Kamala alipokea maoni kutoka kwa wawakilishi wa wananchi kutoka kata zote za wilaya hiyo.

Mwananchi aliyetushambulia kwa jina la Fred Baraza, “ Tuziache Rwanada na Burundi, tuwaaache wamalizane kwanza ndipo tuwakubali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

Maulidi Hassan alisema: “Tukiungana nao, tukaoleana nao, tutaleta kizazi cha ubakaji, wataleta chuki. Kuhusu Shirikisho, twende hatua kwa hatua, tuache haraka”

Venance Sigwa, alisema “ Warundi na Wanyaruanda hawana tabia nzuri, wana tabia za kugeuka geuka, hii tabia ya ukigeugeu itaisha lini tuwapokee?

“Nimekubali waingie lakini watatuhakikishia vipi kuwa hawatakuwa vegeugeu?” alihoji

Katika mji wa Manyovu, Dk. Kamala alifanya mkutano wa ndani ambao uliwashirikisha viongozi wa idara zote muhimu serikalini zilizo mpakani. Eneo hilo lipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi.

Waliozungumuza, wengi walipinga Rwanda na Burundi kupewa uanachama, kwa maelezo kwamba watu wake hawaaminiki.

Moses Msuruzya, alidokeza kuwa duru za uchunguzi zinaonyesha kwamba mwaka 1996, mkakati wa kuanzisha himaya ya Bahima, ulianza kujadiliwa katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.

“Wizara hailioni hilo? Tukiwaruhusu tunajenga daraja, ipo haja ya kusubiri tuone tunakwenda wapi , kwani tangu mwaka 1959 hawajatulia.

“Tunataka ujirani gani na asiye na amani? Tuwape muda wajirekebishe, sasa hivi tunapoteza muda mwingi kuhangaika na athari za vita yao ya ukabila,” alisema

Ofisa Uhamiaji aliyetambulisha kwa jina la Samuel, alisema kwamba Warundi si watu wanaotaka umoja na Watanzania.

Alitoa mfano kwamba wakati Tanzania inapokea Warundi na kuwapa viza siku 30 kuwapo nchini, kwa gharama ya dola tatu za Marekani, wao hudai kiasi kama hicho kwa siku tatu pekee za Mtanzania kuwapo Burundi.

“Sasa hivi tuna wahamiaji haramu wengi sana, halafu kuna mpango wa serikali yetu kutoa uraia wa nchi mbili. Hawa wahamiaji haramu itakuwaje?” alisema

Mjini Kigoma, Dk. Kamala alikutana na baadhi ya viongozi wa CCM ambao walikuwa na kikao chao cha kawaida. Alitumia fursa hiyo kupata maoni ya wananchi.

Kimsingi, wengi wa waliochangia walipinga nchi hizo kukaribishwa kwenye jumuiya kwa sasa. Pia walitaka shirikisho lisiharakishwe mno, badala yake, mambo yaende hatua kwa hatua.

Manju Msambya alisema: “ Sikubaliani kabisa na Rwanda na Burundi kujiunga EAC. Sisi ndio tunapokaa nao hawa, sisi ndio tunawajua wana ukabila na ugomvi wao, chanzo chake kikuu ni mgawo wa rasilimali.

“ Tukiwakaribisha watahamisha matatizo yao kwetu, hatuwezi ku-import matatizo. Tusiharibu maisha bora kwa kuwakaribisha matatizo wake huko huko, wakitaka waunde jumuiya yao”, alisema

Kuhusu Shirikisho, anasema anaungana wazo hilo, lakini kusiwe na haraka kwani hata jumuiya, maana hata Ulaya wanaungana, lakini tuwape muda kwanza wamalize migogoro yao,” alisema

Mchungaji mwingine, Musa Chowo, alisema : Rwanda na Burundi ni vizuri waingizwe kwenye jumuiya, maana hata Ulaya wanaungana, lakini tuwape muda kwana wamalize migogoro yao.

“Tukiwaacha tutakuwa hatujawasaidia wakiwa na amani ndio tuwakaribishe, waje wajifunze kutoka kwetu na tuwe tayari kuwapelekea wataalamu wawafundishe utawala bora,” alisema

Asha Juma yeye anasema matatizo ya wananchi katika nchi hizo ni makubwa, na akapendekeza wapewe masharti, wakiyatekeleza wakubaliwe kujiunga baada ya miaka mitano.
 
Mchungaji mwignine aliyejitambulisha kwa jina la Musa, alisema Warundi wana asili ya ukorofi, kwani hata migogoro kwenye madhehebu ya dini hapa nchini, inasumbuliwa na Warundi waliolowea nchini kujipachika Utanzania.

Aliwataja baadhi ya wakorofi hao ( majina tunayahifadhi kwa sasa), akisema wanafanya vurugu na uchochezi kwa kivuli cha dini, lakini ukweli ni kwamba vurugu zao ziko kwenye damu kwa sababu ni Warundi.

Hata hivyo Christopher Kika, yeye alikuwa na maoni tofouti, Anaamini kuwa kwa kuzikaribisha nchi hizo katika EAC, vurugu, vita na mauaji yatapungua.

Maoni kama hayo yalitolewa na Lazaro Samuel, ambaye alisema Rwanda na Burundi zimeanza kuonyesha uhai katika suala zima la demokrasia.

" Burundi imeingia kwenye uchaguzi wa kidemokrasia, vita imepungua, tukiwakataa hawa kwa sababu ya vita, mbona tunakubali Uganda ambao kuna vita kaskazini mwa nchi?

"Tukiwaingiza katika Jumuiya , wakileta matatizo ni rahisi kuwadhibiti wakiwa ndani, tuwavute waje wajiunge, vita yao itakoma wakiwa EAC," alisema

Msimamo huo uliungwa mkono na Joseph Kadoa Kisina, ambaye alisema " Umoja ni nguvu, hawa tuwakaribishe alimradi tu EAC iweke ulinzi mzuri na iandae bajeti ya ulinzi."

"Luteni Hassan wa Jeshi la Polisi Tanzania (JWTZ), yeye anaunga mkono Warundi na Wanyaruanda kujiunga EAC, akisema hawatasababisha matatizo kwa vile vitaundwa vyombo maalumu.

"Tukiwaacha haitasaidia, tukiwakaribisha hata mataifa yanaoingiza silaha tutaweza kuyadhibiti," alisema

"Kuhusu Shirikisho, twende taratibu, ghafla, mbio mbio, mchaka mchaka katika shirikisho, hapana.

Mwingine aliyejitambulisha kuwa ni Mzee Fernandi: alisema wananchi wa Rwanda na Burundi ni wastarabu, isipokuwa matatizo yapo kwa viongozi wao.

" Tuwakubalie wajiunge, wabaya ni viongozi, kama ni wabaya wanaweza kuongozwa na viongozi wetu vizuri, wasipojiunga wataendeleza ubaya.

"Ikumbukwe kuwa mawazo ya dunia yote ni umoja, iwe moja hata Baba wa Taifa alisema. Tukiwakataa watatuelewa vibaya, nakubali wajiunge, lakini si sasa hivi, iwe baada ya miaka miwili, mitatu au mitano.

"Tuwape muda huo wa masharti ili wajute kidogo, wajue amani ni kitu muhimu," alisema

Mchungaji mwingine ambaye Tanzania Daima haikufanikiwa kupata jina lake alisema: " Nyinyi (Watanzania walio mbali na mipaka ya pembezoni), mnajua Rwanda na Burundi kwa kule. Si tunawajua, kwanza wasomeshwe, wale katika lugha yao hawana neno "tafadhali" tuwape hata miaka, maana vita ikianza nyingi mtakuwa mbali.

"Wakiana na hapa kwetu ( Kigoma), wakipiga yataanguka Kigoma au Bukoba. Mimi nakubali umoja, lakini wapewe muda kwanza, wajirekebishe," alisema

Dk.Kamala, anapokea maoni mengi ya aina hiyo katika mikutano ya ndani na ya nje katika maeneo ya Tarimu, Sota, Shirati, Musoma mjini, Mwanza, Ngara, Rusomo, Kabanga, Karagwe, Mrongo, Isingiro, Ishunju, Mtukula, Mabamba (Kibondo), Manyovu, Kasulu, na Kigoma

Kibondo: Wananchi wa Kibondo, kama wenzao waliotoa maoni, waliendeleza kauli za kuwakataa Warundi na Wanyaruanda.

Hata maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Polisi na Uhamiaji ambao walipata fursa ya kutoa maoni yao mbele ya Naibu Waziri kwa uhuru kabisa, walieleza bayana dukuduku lao na hatari ya kutakaribisha majirani hao.

Mkutano katika wilaya hii ulifanyika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zilizopo eneo la Mabamba. Eneo hilo linapakana na Burundi. Hapa ndipo Watanzania waliposimama kushuhudia Warundi wakipigan risasi miaka kadhaa iliyopita.

Warundi walikimbia katika eneo hilo, lakini baada ya mambo kuanza kuwa shwari, wamerejea na kujenga nyumba nyingi za kuezeka kwa mabati. Kwa hiyo ni eneo linalong'arishwa na mabati baada ya miaka mingi ya umwagaji damu.

Hapa Mabamba ni kilometa 20 hiyi kutoka mjini Kibondo. Sifa kuu ya Mabamba, ni nyumba zilizojengwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kama mfano wa nyumba nzuri na za kisasa zinazopaswa kujengwa na wananchi vijijini. Alifanya kazi hivyo miaka ya 1960.

Katika mkutano, mmoja wa wazungumuzaji, alikuwa ni Kapteni Saleh, ambaye ni kiongozi wa JWTZ katika eneo hilo, Alisema Rwanda na Burundi hazijatulia kisiasa , hivyo si vema zikingizwa EAC.

Tukiruhusu kujiunga tutachukua matatizo yao, wapewe muda wajijenge kwanza," Alisema

Ofisa Uhamiaji, aliyejitambulisha kwa jina Obado, alisema" Muda niliokaa na hawa watu nimeona bado sana, tusiwakaribishe sasa, tuna tofouti zao, na sisi tumetawaliwa na Waingereza, wao wametawaliwa na wakoloni wengine.

Alipinga wazo la kuwaingiza katika jumuiya ambako wanaweka kupewa hati ya kusafiri na vibali vya kuishi nchini kwa miezi sita.

"Kama sasa wanaingia kama wahamiaji haramu, itakuwaje baada ya kuwapa pasipoti?", Alihoji Obado.


Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kibondo, SSP Twaha Ramadhan, aliungana na wazungumzaji wengine, kupinga Rwanda na Burundi kujiunga EAC.

Alisema kama ni uanachama, nchi hizo lazima zipewe masharti na ziyatekeleze.

"Wapewe masharti, kwanza wakusanye silaha zote zilizozagaa, kwa sababu makosa mengi yanayotokea huku, yanafanywa na wakimbizi na wahamiaji haramu wa Burundi," alisema.

Alimweleza Dk. Kamala kuhusu mauaji yanayofanywa, na akampeleka hadi kwenye maeneo ya tukio ambako Watanzania wamekuwa wakipigwa risasi na kuuawa na maharamia wanaodhaniwa kuwa wanatoka Burundi ambayo Isingiro, Mrongo, Rusumo, Kabanga (kagera), na Mwanza mjini.

Oktoba 13, mwaka huu, Rais Kayaka Kikwete, alitangaza kamati maalumu ya kukusanya maoni ya wananchi katika wilaya zote nchini, kuhusu muundo na hatua za kuelekea kwenye Shirikisho.
 
Ngara: Sehemu iliyokuwa na michango ya wananchi iliyojaa mvuto na vionjo, ni walatani Ngara. Itakumbukwa kuwa kwa wakati Fulani, idadi ya wakimbizi wilayani Ngara, ilizidi idadi ya watanzania zaidi ya 200,000 katika wilaya hiyo.

Wananchi wa Ngara, walionyesha kuwa wanajua mambo mengi sana, na kwa hakika michango yao ilikuwa ya umakini mno. Hata wazee wasiodhaniwa, walitoa hoja zilizofanya mkutano uzizime.

Hawa walipinga waziwazi Rwanda na Burundi kukaribishwa EAC. Sababu kuu ni vita na ukabila katika nchi hizo; hali ambayo wanasema ikikaribishwa, itavuruga amani, umoja, mshikamano na utulivu wa Watanzania.

Akiwa katika Kijiji cha Kabanga, wilayani Ngara, mpakani mwa Tanzania na Burudni, wananchi walitoa maoni yao kwa uwazi na kupinga kwa nguvu zote, Burundi na Rwanda kupewa uanachama kwenye Jumuiya ya Africa Mashariki.

Aliyeanza kutoa maoni yake ni Suleiman Minani, na akasema: "kujiunga kunahitaji muda, hawa wamekuwa katika mapigano kwa muda mrefu, wametuletea uhalifu, hasa ujambazi. Hapa Ngara ujambazi umeletwa na wakimbizi hawa.

"Sisi Watanzania, Kiswahili ndicho kitambulisho, Warundi na Wanyarwanda sasa wakizungumza Kiswahili, wanaonekana ni Watanzania.

"Kwa nini serikali inachelewa kutoa vitambulisho kwa raia wake?" alihoji.

Mwananchi huyo alitoa mfano kwa kusema wakati Fulani alisafiri na Wanyarwanda kwenda Mwanza walifika kwenye kizuizi, na akastaajabu kuona wakitoa kadi za uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuruhusiwa kuendelea na safari.

"Mimi nilipitakwa kitambulisho cha gazeti, hatuna vitambulisho na viwango vya kuoleana ni vikubwa, kule (ng'ambo upande wa Burundi) tuna wajomba, mimi nashauri wasubiri kujiunga kwenye jumuiya, wakiruhusiwa sasa, usalama. Wetu utayumba," alisema.

Mwananchi mwingine, Seleman Senduka, alisema, "Kabla ya kuwakaribisha Rwanda na Burundi, kwanza tujue sisi (Kenya, Uganda na Tanzania), tumefaidika vipi na Jumuiya yetu."

Naye Jason Bahina alisema: "Sisi Watanzania hatuna matatizo ya ukabila na vita; wenzetu wanamalizana kwa kuuana. Wanahukumiana kwa kuangaliana pua.

"Kabla ya kuwakaribisha, CCM ifanye kwanza kazi ya kisiasa, ijiridhishe kama kweli kujiunga kwao hakutaleta mgogoro. Kilichodambaratisha Jumuiya ya kwanza ni tofauti za kisiasa, kwa hiyo kabla ya kuwakaribisha Rwanda na Burundi, lazima mataifa haya yaeleweke siasa zao."

Mwananchi mwingine, Joseph Balindie, alisema wananchi wana wasiwasi mkubwa kuona Rwanda na Burundi, zinataka kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Tuna wasiwasi na tabia za wenzetu. Kuwashirikisha ni ngumu, wale wanauana hovyo, kuwashirikisha si rahisi," alisema.

Naye Gideon Ruvulahenda (66), alisema: " Kuungana ni jambo zuri, sasa kama Rwanda na Burundi nao wanataka kuungana na sisi, kwanza wapewe masharti ya kuumaliza ukabila wao."

Aliendelea kusema: "Kwanza wazungukie ndugu zao, wafute ukanda na ukabila wao, kuungana ni kuzuri, lakini kwanza wafute ukabila wao, wakikubaliana kufuta ukabila, ndipo wakubaliwe kuingia kwenye jumuiya."

Japhet Israel (62) alisema kwa umri wake huo, hajawahi kusikia Rwanda na Burundi kuna amani.

Alisema wananchi katika nchi hizo ni ndugu zetu, na kwamba hata baadhi yao wanafanana na watanzania, lakini kwa suala la kuwakaribisha kwenye jumuiya kwa sasa haliafiki.

"Tukiungana tutaharibu usalama wetu, kwanza wajirekebishe, wajue sote tu Waafrika, wajue watusi na wahutu wote ni Waafrika – wajue weupe (watusi) na weusi (wahutu), ni Waafrika, wakijua hivyo, sasa ndipo wakaribishwe kujiunga," alisema Israel.

Ofisa Uhamiaji Mkuu wa Kituo cha Kabanga, Harride Mwaipyana, alitumia fursa ya mkutano huo wa hadhara kutoa maoni yake.

"Nipo hapa kuanzia mwaka 1999, nimesoma tabia za pande zote. Tusikurupukie kitu bila kukijua. Sisi Tanzania, Kenya na Uganda tunajuanatabia zetu.

"Tabia za hawa wenzetu ( Rwanda na Burundi) ni mbaya. Hawana amani, wanabaguana, kuna vikao vya usiku vya kujadiliana. Wanakutana kwa mambo ya siri wakitumia vijisherehe, wanaalikana.

"Ukiwaingiza hawa, nchi itaharibika, wanapenda kutawala, wanajiona bora kuliko mtu yeyote duniani, tusiwakaribishe kabisa. Tuchukue muda mrefu sana.

"Mheshimiwa naibu waziri, naomba ilichukue hili kwa umuhimu wa kipekee. Wameleta ujambazi hawa….," alisema Mwaipyana, akionekana dhahiri kuchukizwa na Rwanda na Burundi kujadiliwa kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Alionekana kuwa na mengi ya kuzungumza, lakini alifikia mahali akazidiwa na jazba, akakatiza maoni yake kwa hasira.

Butiama: Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, yeye alikuwa na maoni yake.

Dk. Kamala alipata fursa ya kwenda kusalimiana naye, akianzia kanisani alikoshiriki naye misa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Butiama.

Baadaye alikwenda nyumbani, na kabla ya mazungumzo, Dk. Kamala alipata fursa ya kwenda kuhani katika kaburi la Mwalimu

Katika mazungumzo yao, Mama Maria alishauri Burundi na Rwanda zikubaliwe kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Msimamo huo wa Mama Maria ni mwendelezo wa filosofia ya Mwalimu aliyeamini katika umoja wa Afrika.

Mama Maria alisema ni jambo la busara kwa nchi wanachama wa EAC, kuzipa uanachama Rwanda na Burundi.

Amesema matatizo ya ukabila na mapigano yanayojitokeza katika mataifa hayo, yanaweza kupunguzwa au kumalizwa kwa kuziruhusu nchi hizo kujiunga katika jumuiya hiyo.

"Nadhani Rwanda na Burundi zikiingia kwenye jumuiya, zitaweza kupunguzwa matatizo ya ukabila na vita.

"Watajifunza kutoka kwetu na wataweza kuishi kwa amani, hawa tuwakubali kwa sababu bila hiyo wataendelea na vurugu na hivyo sisi tutaendelea kuwa na mzigo wa wakimbizi? Alisema.

Hata hivyo alisema suala la kuzikubali nchi hizo kuwa wanachama linapaswa kushulikiwa na taratibu zilizopo zikiwamo kama hizo za kukusanya maoni ya wananchi.

Sirari: Maoni katika miji ya sirari na tarime, mkoani Mara hayakuwa tofauti na sehemu nyingine. Wapo waliopendekeza nchi hizo zikubaliwe kujiunga EAC, lakini wengine walipinga kwa nguvu zote.

Katika mkutano wa hadhara mjini Sirari, Daniel Marwa alisema "Hawa watu (warundi na wanyarwanda) wakubaliwe kuingia, kama ni wakorofi waache waje, watajifunza kutoka kwetu"

Kuhusu shirikisho wengi walichagia walitaka kwanza elimu itolewe kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba wapo wasiojua hata maana ya shirikisho, faida na hasara zake.

Walipendekeza kwamba katika kuelekea kwenye shirikisho nchi wanachama wa EAC hazina budi kwenda hatua kwa hatua.

Kuhusu Rwanda na Burundi kukaribishwa EAC, wengi walipinga, wakisema bado zimegubikwa na Uhutu na Ututsi. Wengi walichagia walipendeza utolewe muda na masharti kwa nchi hizo kabla ya kukubaliwa uanachama.

Mjini Musoma, Dr. Kamala alifanya mkutano, na viongozi wa vyama vya siasa, madhehebu ya dini, mashirika yasioyo ya serikali, asasi na wadau mbalimbali.

Miongozi mwa wachangiaji alikuwa ni Moses Zefania, ambaye alisema kama Rwanda na Burundi zina sifa zikaribishe kwenye jumuiya.

"Afrika sasa ifikirie kuungana, tusiangalie tofauti zetu," alisema Zefania.

Naye Kalaine Kunei alipendekeza mipango ifanywe ili shirikisho la Afrika mashariki lianze haraka.

Mwanza: Mkoani mwanza Dr. Kamala alifanya mkutano katika Ukumbi wa Halmashauri wa jiji hilo. Kama iliyokuwa Musoma, mkutano wa Mwanza ulihudhuriwa na wadau wa kada mbalimbali, wakiwemo wanasiasa wa vyama mbalimbali, wakiwamo wanasiasa wa vyama mbalimbali, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, wafanyabiashara, viongozi wa asasi na kadhalika.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema "Shirikisho hatuwezi kulikataa, lakini kwanza Watanzania watambuliwe, wapewe vitambulisho, nchi hii yeyote anaingia tu"

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Salum Hassan Ferej, pamoja na mambo mengine mengi aliyozungumza alisema huu ndio wakati wa kuungana.

"Wakati huu ndiyo wa kuungana, watanzania pekee hatutafika popote," alisema.

Moses Methew alitadharisha kwa kusema tunapaswa kuwa macho kwenye shirikisho ili ajira zisitishie kwa wageni tuu.

"Tumejiandaa vipi kulindaa ajira? Tuangalie tusiwe wasindikizaji tuu," alisema.

Rusumo: Rusumo ni mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Ni sehemu ya wilaya ya Ngara.

Waliozungumza walionekana kupinga Rwanda na Burundi kukaribishwa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Jumuiya yoyote lazima iwe na maslahi kwa wananchi, Hawa tunawakaribisha tutapata nini kwao? Sijaona bidhaa zao, isipokuwa vyuma vichakavu na viazi kutoka Rwanda. Hakuna tunachoweza kupata kutoka kwao?

"Tanzania iwe ya Watanzania, Tusiwe kama Kosovo ambao waliruhusu wageni, kisha wageni wakaanzisha himaya yao", alisema mchangiaji.

Wananchi wanashaka na Rwanda na Burundi, wanasema Wananchi katika nchi hizo hawajatulia, wana mifugo mingi, tukiungana si tutamezwa? Shaka kubwa ni hali ya Kisiasa?

Katibu tawala wa wilaya ya Ngara, naye alikuwa na maswali kadhaa.

"Jumuiya itahusishwa maeneo gain? Kama Tanzania, Kenya na Uganda kuna kutoelewana, kuna sababu ya kukaribishwa Rwanda na Burundi?

Sisi tungesubiri kwanza hadi sisi tuwe tumeelewana?

"Tukiungana hivi hivi, tunaweza kuwa daraja la wengine kujinufaisha," alisema

Mrongo: Eneo la Mrongo ni maarufu. Lipo wilayani karagwe Hapa ni mpakani mwa Tanzania na Uganda miongozni mwa mambo yanayolifanya eneo hili liwe maarufu ni ukweli kwamba hapa ndipo Yoweri Museveni alipoishi wakati wote wa harakati za uasisi, na hatimaye kwenda kumngoa nduli Idi Amini.

Katika kijiji cha mrongo Rais Museveni alitoa fedha ili ijengwe shule kijijini hapo. Walaji wa Kitanzania wakazitafuna. Hakukata taama. Katoa fedha nyingine alichofanya sasa ni kuleta mafundi na wasimamizi wake. Shule inajengwa na ni ya kisasa.

Dr. kamala alifanya mkutano katika eneo hili kuzungumzia EAC.

Mwananchi wa kwanza kutoa maoni alikuwa ni Daud Karoli. Aliyesema "Ingawa Rwanda na Burundi ni ndugu zetu, tusubiri, bado wana matatizo makubwa. Wana vita na ukablia, Wakitulia ndipo tuwaingize kaitka Jumuiya."

Mwananchi mwingine ambaye jina lake halikupatikana alitetea kwa kusema Rwanda na burundi wanapaswa kuingizwa sasa.

"Tusiwe na wasiwasi, kila nchi itaendelea kuwa nchi na mipaka yake, udhibiti ule ule, hatuwezi kuwaacha wanagambana, wanapigana na kuuana, ni vizuri tuwaingize kuna sababu za wao kujiunga.

Ni ndugu zetu. Waafrika wenzetu, sheria zitabaki zile zile" alisema.

Ofisa Mifugo aliyejitambulisha kwa jina la Charles, alisema "Hapa tunahukumiwa na historia Watawala wa Rwanda na Burundi alikuwa tofauti na watawala wa Tanzania, Kenya na Uganda.

‘Tuwascreen tutaona matatizo yao, ikiwezekana ndipo twakaribishe," alisema

Mhifadhi wa Wanyamapori, Francis Chuwa, alisema "tunaruhusu wajumuike kwenye muungano, vita vya majirani zetu hawa inawezekana ni subject, bora waingizwe.

"Tukiungana nao, wataona aibu kuona wenzao hawagombanim turudie Uafrika wetu. Hii mipaka ni ya kikoloni, tukae pamoja," alisema Chuwa.

Jackson John, naye alikuwa na maoni yake. "tukiwaruhusu waingie, lakini serikali yetu iongeze bajeti ya ulinzi hasa baada ya kuwaingiza Rwanda na Burundi."

"tumeingia dhamana kutokana na mitafaruku yao,"

Dr. Kamala pia alipata fursa ya kukusanya maoni ya Wananchi wa kata ya Isingiro, wilayani karagwe, kwenye mkutano wa hadhara.

Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Sweatbet, alisema "Rwanda na Burundi zisingizwe, wana vita hawajui Kiswahili, wakiingizwa wataleta migogoro.'

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Paul, alisema "Burundi na Rwanda wasishirikishe, ni watu wa vita na kuuanna, akiungana na sisi watafundisha watoto wetu vita, tutakuwa na umwagaji damu."

Maoni kama haya yalitolewa na Deogratius Maiko" Naomba Rwanda na Burundi wasiingine kwenye jumuiya, ni wakabila, wanajali Ututsi na Uhutu, kazi yao ni kushitakiana arusha."

Hata hivyo felisa Chrysostom, ambaye alionekana kuwa na asili ya Rwanda alikuwa na maoni tofauti.

"tuwashirikishe kwenye jumuiya, tumezaa nao, ni wenzetu wana shida. Tukiwakaribisha tutawafundisha," alisema na kuzomewa na umati uliohudhuria mkutano huo mkubwa.

Kasulu: Mmoja wa maofisa wa JWTZ, alimweleza Dk. Kamala kuwa suala la Burundi kukaribishwa kwenye jumuiya, linapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu.

Yeye anapendekeza Rwanda waruhusiwe lakini Burundi wapewe muda kwanza

"Hawa wasubiri, vinginevyo tutabeba mzigo wao," anasema

Maoni kama haya yaliyotolewa na Freddy Baraza, kwa kusema "Tuziache Rwanda na Burundi, "wamalizana kwanza" (wachinjane)."

Mchangiaji mwingine Thobias, alisema "Tuwapime kabla ya kujiunga EAC, tuhakikishe kwanza wana amani ya kudumu, tukiwaruhusu sasa. Tutaleta matatizo."

Na HabariTanzania.com - http://www.habaritanzania.com/articles/1837/1/
 
Na HabariTanzania.com

NIMEJITAHIDI kutafuta maneno murua, ninayoweza kuyatumia kuufikisha ujumbe huu kwa Watanzania, lakini nikiri kuwa nimeshindwa.

Sijui nitumie maneno au vionjo gani, ambavyo vitawapa picha halisi wananchi wanaoishi nje ya mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na hata Rukwa, ili waelewe ninachotaka kusema.

Nia yangu ni kutaka wananchi wenzangu wajue jinsi Watanzania wenzetu, katika mikoa ya magharibi, walivyopoteza uhuru, utu na amani ndani ya nchi yao.

Baada ya kufika katika Mkoa ya Kagera, hasa katika wilaya za Biharamulo, Ngara, na Karagwe, sikuamini kama niko Tanzania.

Nilipofika Kibondo, Kasulu, na nilipotoka Kigoma kwenda Tabora, kupitia eneo la kambi za wakimbizi za Lufufu I na Lufufu II, sikuamini asilani kama kweli hii ndiyo nchi yangu.

Sikuamini kama hii ni sehemu ya Tanzania, nchi inayosifika kwa amani, utulivu, umoja na mshikamano. Nasema sikuamini kabisa. Sikuamini kwa sababu hakuna siku nimeomba polisi wanisindikize kutoka Mbezi kwenda Kariakoo.

Huku magharibi, hata kwenda sokoni, karibu wenzetu hawa watahitaji polisi wa kuwasindikiza!

Maisha gani haya? Je, kweli serikali iko makini? Inasikiliza kilio cha haki cha wabunge wa mikoa hii? Kwa nini tumelala kiasi hiki wakati Tanzania imechukuliwa na wageni majambazi?

Katika maisha yangu, sijawahi kuona polisi wakiwa na bunduki zilizofungwa magazine tatu, nne, hadi sita! Sikuwahi kuona kituko hiki. Kwa anayeona hali hii kwa siku ya kwanza, kama ilivyokuwa kwangu, anaweza kudhani anachoshuhudia ni maigizo.

Kutoka Buselesele hadi Nyakanazi, wapo waliotushangaa, kwamba tumewezaje kupita katika pori bila ulinzi wa polisi. Kutoka Nyakanazi, tulikwenda moja kwa moja hadi Rusumo wilayani Ngara.

Barabara ni nzuri. Ni barabara ya lami iliyojengwa. Inapita katika milima na mabonde ya kuvutia.

Barabara yote hii ni hatari. Majambazi ni wengi. Wanafanya unyama wa kila aina. Wanateka magari asubuhi, mchana, jioni na usiku. Ujambazi ni kwa saa zote 24!

Mwezi uliopita, majambazi walimuua mpiga debe katika stendi ya mabasi Ngara, siku iliyofuata, waliingia Karugawe, siku tano wakarejea tena na kuua watu wawili, na wengine kama hao walifia hospitalini.

Kutoka Ngara, tukawa na safari ya kwenda Karagwe. Usafiri kati ya sehemu hizi mbili ni wa matatizo makubwa mno kwa wananchi.

Kutoka Benako, unaingia katika pori la Kyamisi. Hili ni pori kubwa, refu, na pana. Kwa gari aina ya Land Cruiser tulilokuwa tukisafiria, tulitumia muda wa saa nne hivi kukatiza pori hili. Barabara ni nzuri, na kwa muda wote huo, na kwa aina ya gari tulilokuwa tukitumia, bila shaka msomaji anaweza kujiuliza kuhusu ‘uzito’ wa pori hilo.

Tulipita tukiwa tunasindikizwa na polisi wawili wenye silaha na magazine zisizo na idadi, maana wanasema majambazi wengine huwa na risasi hata zaidi ya 600; kwa maana hiyo, wingi wa risasi ni jambo linalozingatiwa mno na polisi.

Majambazi katika pori hili, wengi wanadaiwa kuwa ni wakimbizi kutoka Rwanda, lakini kuna habari kwamba wanashirikiana na Watanzania; ambao bila shaka yoyote, wana asili ya huko huko.

Ndani ya pori hili, maeneo hatari zaidi ni yake yanayopatikana mtandao wa simu selula.

Katika eneo hilo, wananchi wanajua wazi nafasi ya simu katika suala zima la ujambazi. Majambazi huwasiliana kirahisi. Hawa ni wale wanaoingia kwenye magari ya abiria, na wengine wanaokuwa maporini.

Siku za Alhamisi na Ijumaa ndizo mbaya na hatari zaidi, kwani ni siku za minada. Majambazi huteka magari na kupora abiria mali zao. Mauaji au kujeruhiwa katika matukio ya aina hiyo, si mambo ya kuulizwa.

Polisi wanaeleza wazi kuwa wamechoshwa na kazi ya kusindikiza magari, yawe ya abiria, mizigo au ya viongozi. Wenzao wamepiga kambi katikati ya pori hili. Hawa wanaishi maisha kama ya nguchiro! Hawana huduma muhimu, japo za mawasiliano. Wengine hawana redio za mawasiliano, eti wakipewa wanaweza kuporwa na majambazi, kisha wanazitumia kuendeleza uhalifu!

Katika pori hili la Kyamisi, suluhisho la kumaliza ujambazi ni kuendesha operesheni ya kijeshi katika wilaya za Karagwe, Ngara, Biharamulo, Kibondo, Kasulu na Kigoma kwa jumla.

Hili si jambo la kuepukwa. Tuna makamanda na wapiganaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanafanya nini wakati huu ambao hatuna ugomvi na majirani zetu?

Nani anayedanganya kuwa kazi hii inaweza kufanywa na polisi hawa wawili, watatu waliopo hapa Ngara, Karagwe, au Biharamulo? Helikopta za jeshi zinafanya nini? Vifaru na mizinga, ni kwa ajili ya nani?

Tuna haki ya kutamba kwamba Tanzania ni nchi ya amani, ilhali kuna Watanzania wenzetu wanaogopa hata kwenda kuteka maji kwa kuhofia kutekwa na kutendewa vibaya?

Kuna sababu gani zinazokwamisha serikali kuweka vituo vingi kwenye mapori ya wanyama?

Leo hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu kuona kuwa majambazi wameanzisha jamhuri yao ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mfano, hakuna anayeweza kupita katika barabara kuu ya lami kuanzia Burigi Game Reserve-Ngazi Saba-Karugete-Mgodini. Eneo hili ni jamhuri ya majambazi.

Matatizo mengine yako katika pori linaloanzia Muleba hadi Biharamulo. Kwa gari tulilokuwa nalo, ilituchukua muda wa saa tatu hivi kukatiza pori hili. Barabara ni nzuri sana.

Hii ni ngome imara sana kwa majambazi. Kuna majambazi kutoka nchi jirani, walioingia na kujichimbia, wakiendesha vitendo vya kinyama kwa Watanzania.

Wanawapiga risasi wananchi wetu, wanawapora mali, na kuwafanyia vitendo vya kipuuzi, vikiwamo vya kuwavua nguo na kuwaacha kama walivyozaliwa.

Hivi karibuni majambazi hao walivamia basi, lakini polisi walimuua mmoja wa majambazi hao.

Kuna Nyakanazi kwenda Kibondo; na kutoka Kibondo kwenda Kasulu, ujambazi ni mambo ya kawaida kabisa. Watanzania wanasafiri katika nchi yao wakiwa na hofu kubwa. Wanavamiwa, wanaporwa, wanajeruhiwa kwa risasi, wengine wanauawa, na wanadhalilishwa.

Sehemu zote hizo, lazima magari yasindikizwe na polisi wenye silaha. Maisha ya aina hii, yataendelea hadi lini? Kwa nini wenzetu waishi katika maisha haya ya hofu?

Mwezi uliopita majambazi wenye silaha, nusura wamteke Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, ndani ya pori la Lugufu mkoani Kigoma.

Tukio hilo lilitokea asubuhi, wakati Dk. Kamala alipokuwa akisafiri kwa gari akitoka Kigoma kwenda Tabora.

Watuhumiwa ni wakimbizi wanaoishi katika kambi za Lugufu I na Lugufu II.

Waliweka mawe barabarani, kilometa chache kutoka katika kambi hizo.

Kilichomnusuru Dk. Kamala na ujumbe wake ni lori la mizigo ambalo liliwahi kufika eneo la tukio. Lori hilo lilitekwa. Mali zikaporwa. Dereva na msaidizi wake walipigwa na kudhalilishwa.

Kila palipo na kambi ya wakimbizi, matukio ya utekaji nyara ni mengi. Kuna wakimbizi wanaotoroka kambini, wanakwenda kufaya uhalifu na kisha wanarudi.

Cha kusikitisha ni kwamba polisi katika eneo hilo hawana usafiri wa aina yoyote, zaidi ya kutegemea miguu.

Gari moja walilokuwa nalo lilipata ajali, lakini baada ya kutengenezwa, limebaki mjini Kigoma.

Tuliwashuhudia polisi zaidi ya 10 wenye silaha wakiwa na watuhumiwa wawili wa tukio hilo, lakini wakiwa hawana usafiri japo wa baiskeli.

Jamani, hivi kweli viongozi wa serikali wako makini na mambo mazito katika nchi hii? Pori la Lugufu, unaweza kuwatuma polisi wapambane na majambazi bila kuwa na usafiri na zana nyingine za kisasa?

Polisi sehemu zote hizi ni watu wa kudhalilika. Wanasindikiza mabasi au malori, wakishafika mwisho wa safari, suala la kurudi walikotoka, ni shauri lao!

Nimeshuhudia polisi wakirejea maeneo yao kwa kuomba lifti kutoka kwa wananchi.

“Tunaomba lifti za baiskeli, safari ni ndefu sana, mwenye baiskeli anaendesha, akichoka, ananipa naendesha -tunapokezana hivyo hivyo,” aliniambia polisi mjini Kibondo.

Hivi kweli serikali inashindwa kununua pikipiki? Kama magari ni ghali, hata pikipiki kwa mashujaa hawa ni vitu visivyowezekana? Tanzania ni maskini kiasi hiki?
 
Tukiwa Kibondo, tulionyeshwa mahali ambako ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) aliuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika eneo la Mabamba.

Kabla yake, dereva teksi na abiria kadhaa walipigwa risasi na kuuawa katika eneo hilo.

Polisi hao wanafanya kazi katika mazingira magumu mno. Wanapigwa vumbi kiasi kwamba hata afya zao ziko hatarini.

Hali ya ujambazi iliyopo Kagera na Kigoma, inahitaji nguvu mpya za serikali. Kuna mambo kadhaa ya kufanya.

Mosi, kwanza kabisa serikali itambue kuwa ukanda wa magharibi kwa nchi yetu, ni ukanda uliochukuliwa na majambazi. Ni ukanda wa wageni walioamua kuwafukuza Watanzania. Ikiri kuwapo kwa tatizo hilo kwanza. Na ijue wazi kwamba nchi hii haina amani hata kidogo.

Pili, kuwepo na kikosi maalumu cha polisi wengi waliofunzwa kupambana na majambazi misituni. Polisi hao wapewe zana za kisasa kabisa.

Malipo kwa polisi hao, yawe tofauti na polisi waliopo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza au sehemu nyingine za mijini. Polisi wa Ngara, Karagwe, Kibondo, Kasulu, Kigoma, na Biharamulo, wapate malipo maalumu kama sehemu ya motisha kwa kazi kubwa na nzito ya kulinda raia wa nchi hii.

Tatu, kwa hali ilivyo sasa, na kwa kutotaka kuchelewesha mambo kwa kuanza kuwafundisha polisi maalumu wa kupambana na uhalifu katika eneo hili, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), liingie kazini.

Makamanda na wapiganaji mabingwa katika medani za kivita, waende eneo hili, waone ni nini cha kufanya ili kurejesha heshima ya Mtanzania.

Wana vifaa vingi vya kijeshi. Vifaa hivyo havitakuwa na maana kama vitatunzwa tu. Hali iliyopo mikoa ya magharibi mwa nchi, ni ya kivita. Jeshi liingie eneo hili kivita.

Kuna helikopta, kuna magari ya delaya, kuna vifaa vya kisasa, kuna askari waliofunzwa kuyamudu mazingira haya ya misitu na mapori- kazi ianze sasa.

Jeshi haliwezi kukaa na kustarehe, wakati kuna upande wa nchi umetwaliwa na majambazi kutoka nchi jirani, wanaoshirikiana na wenyeji wachache.

Ijulikane wazi kuwa kilichopo sasa Ngara, Bihalamuro, Kibondo, Kasulu, Lugufu, Karagwe na kwingineko, ni vita.

Polisi pekee hawaiwezi kazi hii. Majambazi yaliyopo, yana mbinu za kivita, na huenda hawa ni masalia ya askari wa kawaida na makomandoo waliotoroka Rwanda, Burundi na DRC.

Hawa saizi yao ni askari wenzao shupavu wa JWTZ, ambao wameapa kulinda mipaka ya nchi hii kwa gharama yoyote, na wanachosubiri sasa ni amri ya kuwateketeza mabazazi hawa.

Nihitimishe tu kwa kusema suala la ujambazi katika mikoa ya magharibi mwa nchi yetu, ni kubwa na la hatari. Tanzania imemezwa upande wote wa magharibi.

Siasa iwekwe kando katika suala hili. Tuelezane ukweli. Tuingie vitani kuirejesha Tanzania iliyochukuliwa na majambazi wageni.

Kwa pamoja, tunaweza kuwafanya Watanzania wenzetu wajione kuwa wako salama katika nchi yao.

Kutumia kigezo cha kupungua kwa ujambazi Dar es Salaam, kama kipimo cha nchi nzima, ni kujidanganya.

Tanzania si salama kama wengi wanavyodhani. Magharibi, kumetwaliwa. Kunahitaji kurejeshwa.

manyerere@habaritanzania.com
selula: 0787 335469
 
Unregistered said:
TZPride
You are being ignorant in the sense that remember each of the three countries will remain as a sovereign state... the only thing that we shall have in common is that we can now trade more freely between the three countries and moreover there will be a parliament comprised of both KE, TZ and UG and all your views no matter which country you come from will be heard in the said parliament.
Balozi[/QUOT
-----------------------
Balozi,
You are absolutely right, by virtual of being TZN, I'm ignorant!. Tell me, M7 has anounced to be the 1st president of EAF, will you have Tz , Ke or Ug as countries? or you mean you will be having Tanzania, Kenya and Uganda as states in EAF, their heads being governers under M7.mmmh..if that's the case, there wont be sovereignity my dear clever boy.
Parliament? No, no noooooooooooooo... I dont want to see my dear Tzs MPs turned into punching bags by experienced Kenyan counterparts. Wana muda mrefu wanapigana masumbwi bungeni, wao hutumia " Hoja ya Nguvu" badala ya "Nguvu ya Hoja"-That's Kenyan parliament reputation!
 
Unregistered said:
Kwa kuwa wakenya wanahitaji TZ kuliko TZ inavyowataka na kwa kuwa walituibia mwaka 1977, kwa nini tusiwawekee masharti kwamba kabla hatujaingia kwenye federation lazima wao wafanye reparations. Yaani warudishe zile mali walizoziiba kwa nguvu kabla ya community kufa halafu ndiyo tuanzae upya?
Halafu watuombe msamaha na waruhusu TZ ikalie bandari ya mombasa na kukusanya ushuru mpaka zile mali walizozidhulumu zilipwe kabisa na hasara ambayo Tanzania iliipata iweze kusawazishwa?


Siyo wazo baya kwa kuanzishia mjadala! Lakini zaidi ya hayo, hivi tujiulize kwa nini katika EU kuna wengine wako jnyuma akini kwa kuwa kwao nyuma kuna marekebisho fulani yanafanyika jkuwa-accomodate wengine?

Inawezekana hapa! Tuamzie hapo!
 
Kenya na nchi jirani ndio walivyo maji yamewafika shingoni, wakenya wameitwa ni Manyang’au, uliza kwa nini waitwe nyang’au? Wamemchora rais wa Tanzania ati analambwa miguu na waandishi wa habari mithili yeye ni muumba. Sisi Tanzania hatuna tabia na maadili haya kwa viongozi wetu.

Vile vile wamemsuta rais eti anaongelea nchi yao pale alipokwenda Marekani, Sasa kwa sababu waandishi wengi wa Tanzania hawakujibu mapigo hayo sisi kama watanzania tumeamua kujibu.

Tunafahamu fika wenzetu walizoea tangu enzi walipopata uhuru kuwatukuza viongozi wao kila wakati wa taarifa ya habari, sijui ni mara mia ngapi hivi kwa siku na hawajaacha tabia yao chafu ya kuweka vinyesi kwenye mifuko ya Rambo. Haya sio matusi ni ukweli wa mambo hebu kaangalie maana ya nyang’au.

Tukumbuke ya wahenga, waliosema ‘ukiwasha moto kuuzima si jambo rahisi’, sasa leo hii wanaomba samahani kwa mlango wa nyuma ya kwamba matusi yaachwe; hebu uliza nani alianza? Sio hivyo tu wanaendelea kututukani wanasema hatukusoma, sisi ni maskini wakutupwa n.k. sisi hatuwezi kukaa kimya tu kama waandishi wa habari walivyofanya – ukweli unauma.

Ukweli wa mambo ni kwamba hii federation inaletwa sio kuwanufaisha watanzania wote; ni wale ambao tayari wanafaidika hivyo wanahitaji kujiongezea maslahi yao. Tunao wakenya, waganda, warundi n.k. ambao wamejaa kama utitili, nakumbuka wale wliokuja kwanza kwanza miaka ya 1980 wakati wa kumuondoa nduli, tuliambiwa ni wakimbizi na tuwasaidie, walikuwa hawana kitu masikini, leo hii ni matajiri wa kutupwa na wanatamba; hata kwao hawataki kurudi tena na wanawakaribisha wenzao waje kufaidi. Kulikoni Tanzania? Political Liberation of Africa finished!

Tumewakaribisha hawa jamaa sebuleni sasa wanataka kuingia chumbani tena sio kwa amani bali fujo (fast track).

Watanzania wenzetu wameisha sema tena sio siri itabidi waanzishe kikosi cha wazalendo kupigania uhuru wa nchi hii? Hili si la mzaa tukumbuke 1998 wakati yule jamaa aliyejificha tora bora alivyowaonya nchi za magharibi na wakampuuza, leo mapigano yanaendelea. Hivi sio vitisho ‘mwenye macho haambiwi atazame’.

Uongozi wa CCM ulipiga kampeni wakati wa uchaguzi kuwapatia wananchi kazi na wale wageni wote ambao kazi zao zinaweza kufanywa na watanzania itabidi warudi makwao hususani hawa wageni kutoka Kenya, Uganda na nchi jirani. Haya ni mambo yanayofanyika diniani pote si Tanzania tu kazi ambazo wazawa tunaziweza lazima tuzifanye. Sasa kibao kinageuzwa ati tuwe na federation. Jamani tusipuuze ya wahenga ‘mwamba ngozi huvutia kwake’.

Hivi watu waliopewa dhamana ya nchi hii pamoja na usalama wa taifa wako wapi? Nchi inauzwa hivi hivi tu bure bure. Viongozi tuliowachagua wako wapi kuwaelimisha wananchi kuhusu huu uvundo.

Hata ‘generation’ haijaisha tayari wale wote ambao walikuwa wanashirikiana na nchi za magharibi kutukandamiza sasa wanataka eti sisi tuungane na askari kanzu wao waliokuwa wakiwatumia. Iweje leo hii tuwe tumesahau yaliyotokea Congo, Kenya, Uganda, Somalia n.k. Hii federation ni njia nyingine ya kuanzisha vita ambavyo havitaisha ndani ya nchi yetu, ni mwanya wa kutaka kutuingilia chumbani. Waliokuwa wanatukandamiza bado wapo na wanaendelea na juhudi zao kwa njia tofauti tofauti.

Nchi zinazoandikwa vizuri leo hii katika nchi za magharibi – Kenya, Malawi n.k. ukisoma habari ya bongo basi ni mambo mabaya ya kutudhalilisha ambayo hayaandikwi kama ya wenzetu. (Utakumbuka serikali ya waingereza walivyoilalamikia BBC kuhusu habari ya kimbunga kule Florida hawakupenda habari ziandikwe zilivyokuwa lakini kwa sisi ni sawasawa). Kenya wataendelea kutumiwa na marafiki zao tu hawana ujanja. Ujanja wao ni wa alinacha. Mtoto wa chui leo hawezi kuwa paka.

Kenya wanataka hadi kesho na mtondogoo kudominate East Africa na hii ni strategy tu wameisha kubaliana wamtumie M7 ambaye ana uloho wa madaraka.

Hivi leo kweli Watanzania tumelewa amani na tunadiriki na kufikiria nchi zote hizi zilizotuzunguka ambao wanauana kila siku wanafurahia amani yetu? Wana lao jambo na ni vyema kujiweka tayari kwa ufisadi wowote maana lazima kuna mkono wa mtu. Hii ajenda sio ya Kenya, Uganda wala Warundi na kibaraka wao M7.

Wametafuta sababu na wanaona jinsi tulivyoshindwa kumiliki mali zetu na kuwaachia wafanye wanavyotaka kwenye mikoa ya Mwanza, Kagera, shinyanga, Kigoma, na ukanda wote wa mpaka na Kenya ambako njia za panya zimeshamiri.

Turudishe heshima yetu. Please do not play around with this stability built.


Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Unregistered said:
Kenyans Ignore This Forum> Dont Reply>
I cant believe what I'm reading.. The reason why Africa will remain poor, will be always associated with Diseases, Hunger and poverty is due to this kind of websites and racists, hatiful insults towards fellow africans.

If you have happen to have lived in the west it does not matter you are tanzanian, kenyan, ugandan, Nigerian white people see you as black African. Genocide in Rwanda, femine in Ethiopia and other misgiving in africa reflects to failures of africa as a continent.. How long do you have to wait for white people to solve african problems? we expect USA/Europeans to send miltary and food aid to help other africans when other fellow africans ignores it is happening ? That why I see African president running to western coutries for AID/investors.... We need to wake up, Most African problems will only be solve by African. If you are waiting the help from the west, they will use you to enrich themselves. They have been doing so for years

The single most problem of Black man is self hate, selfishness and not supporting each other. Not only between nations, Just among us..
Instead of spending numerous hours figuring out what is wrong with you neighbouring countries, can you come up with ideas how to solve our problems.

We dont even have our own cars, we barely export anything to the west, we have only factories to produce sugar,salt,water,bread etc
The only way out of poverty is Business among us, education for our people, technology...

Kenya, uganda, Tanzania we are all third world coutries , where most people live on less than a dollar a month.. Non is better than the other!!!!!!!
Each country has it good and bad sides..
 
Unregistered said:
..............The single most problem of Black man is self hate, selfishness and not supporting each other. Not only between nations, Just among us...............


HOW TRUE!!!

Africans have been a victim of abuse for a long time, being told they are useless, and somehow that has gone into there brains. They are unsure of themselves. We need to urgently correct this if we are to become relevant as a people.

Debate among Africans, including this one, even through vitriols, should be viewed as efforts to find peace with ourselves, build confidence among ourselves, not enhace hate. This will however develop slowly!

I do not therefore support the Kenyan call to ignore, it is useful.
 
Back
Top Bottom