Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
kinyang'anyiro hicho.CHADEMA na mgombea kwa pamoja walifanikiwa kuweka bayana kwamba katika masuala ya kitaifa, utanzania unakuwa kitu cha kwanza kabla ya vyama na tofauti za kiitikadi chini ya kauli ya kampeni „SIASA SI UADUI-TANZANIA NA AFRIKA KWANZA". Hivyo, timu inapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wabunge wachache waliotambua ubora huu na kumpigia kura Profesa Mwesiga Baregu bila kutanguliza kwanza maslahi ya chama chao.
b) TUMEBAINISHA MAPUNGUFU YALIYOMO KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI NA TABIA YA WENGI YA WABUNGE KATIKA KUPIGA KURA: kwa ujumla mapungufu mbalimbali katika kanuni na taratibu za uchaguzi yameweza kubainika. Kwa upande mwingine tabia ya wabunge katika kupiga kura imebanika kama ambavyo imedokezwa katika mapungufu yaliyotajwa hapo juu. Hii ni hatua muhimu katika kuboresha mchakato wa uchaguzi wa bunge la Afrika katika chaguzi zijazo.
MAPENDEKEZO NA MWELEKEO:
(i) UCHAMBUZI UFANYIKE KUBAINI KIASI NA ATHARI ZA „SIASA ZA UNDUGU KWA MUSTAKABALI WA TAIFA: Suala la kuongezeka kwa viongozi wanaochaguliwa wenye uhusiano wa kindugu na wale waliokatika nafasi mbalimbali linapaswa kufanyiwa uchambuzi. Zipo hisia kwamba kama mtindo huu ukiendelea kutajengeka tabaka la nasaba za watawala(royal classes) na watawaliwa. Kama hali hii ikitokea ni hatari kwa umoja wa Taifa. Ni vyema wakati wote mfumo wa uchaguzi na kisiasa ukatoa haki na uhuru kwa watanzania wote.
(ii) UANGALIZI NA UTAZAMAJI WA UCHAGUZI UFANYIKE KATIKA CHAGUZI ZOTE KATIKA HATUA ZOTE: Uchaguzi wa bunge la Afrika Mashariki kama zilivyo chaguzi nyingine ni mchakato unaopaswa kuwa huru na haki katika ngazi na hatua zote. Kwa mantiki hiyo suala la haki kutendeka ni la muhimu lakini suala la haki kuonekana ikitendeka ni la muhimu zaidi. Hivyo jitahada za makusudi zifanywe na wote wanahusika kuhakikisha kuwa chaguzi zijazo za bunge la Afrika Mashariki zinakuwa na waangalizi(monitors) na watazamaji(observers). Hii ni muhimu hususani wakati huu ambapo jumuia ya Afrika Mashariki inaelekea kuchukua nafasi ya pekee katika maisha ya wananchi wa nchi wanachama.
(iii) KAMATI ZA VYAMA(PARTY CAUCUS) ZISITUMIKE KUBAKA DEMOKRASIA: Katika mazingira ya sasa kamati za vyama(party caucus) zimekuwa zikitumiwa vibaya na chama tawala. Suala la kuwa na kamati za vyama ama kambi(party/camp caucus) ni suala la kawaida katika demokrasia ya mfumo wa vyama vingi kote duniani. Hata hivyo katika mabunge yanayoheshimu haki na uhuru wa mawazo na maamuzi kamati za vyama/kambi ni fursa ya serikali ama mamlaka kutoa UFAFANUZI na KUSHAWISHI. Lakini hapa kwetu chama tawala kimekuwa kikitumia kamati ya chama kutoa SHINIKIZO na MAELEKEZO kwa wabunge. Na wabunge wengi kwa upande wao wamekuwa wakisukumwa na mashinikizo hayo na kufanya maamuzi kwa kuzingatia kile wanachokiita MSIMAMO WA CHAMA. Tunachukua fursa hii kuwakumbusha wabunge kwamba ninyi ni WAWAKILISHI WA WANANCHI hivyo mnapaswa kuweka mbele MASLAHI YA UMMA kabla ya maslahi ya chama ama maslahi binafsi. Kumbukeni kuwa mmechaguliwa na wapiga kura wa vyama mbalimbali na wasio wanachama wa chama chochote hivyo ni muhimu kwenu kuweka mbele maslahi ya Taifa.
(iv) UWAKILISHI WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI UPANULIWE NA MFUMO WA UPATIKANAJI WA WABUNGE WAKE UBORESHWE: Idadi ya wabunge wa sasa(tisa kwa kila nchi) ni ndogo ukilinganisha na maslahi yanayojadiliwa katika bunge la Afrika ya Mashariki hususani wakati huu ambao tunaelekea katika soko la pamoja na hatimaye baadae shirikisho la kisiasa. Katika hali kama hiyo kuna haja ya kujadili suala la kupanua uwakilishi lakini pia kutengeneza daraja mwafaka baina ya bunge la Afrika ya mashariki na mabunge ya nchi husika. Aina mbalimbali za uwakilishi zitafakariwe ikiwemo suala la kuwa na sehemu ya wawakilishi ambao watapigiwa kura za moja kwa moja na wananchi wa nchi husika hususani katika hatua ya shirikisho. Pia kuna haja ya kuzifanyia marekebisho kanuni za bunge ili kuzingatia pia uwiano wa kura kwa upande wa Zanzibar pamoja na kutumia kura za ujumla badala ya kutumia idadi ya viti bungeni kama kigezo pekee.
(v) WANANCHI WAYAJADILI MASUALA YALIYOIBULIWA NA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUTOA MAONI YAO KUHUSU MCHAKATO KUUNDA SHIRIKISHO LA AFRIKA YA MASHARIKI: Katika uchaguzi huu masuala mbalimbali yaliibuliwa kuhusu mambo ya kuzingatiwa katika muktadha wa uundwaji wa shirikisho la Afrika ya Mashariki. Ni wakati mwafaka sasa wa kuyajadili kwa kina masuala haya na kutoa maoni katika kamati iliyoundwa ya kukusanya maoni. Baadhi ya mambo hayo yamedokezwa katika sehemu ya mafanikio. Aidha tunatoa mwito kwa wote waliokuwa wagombea pamoja na vyama vyao kuendeleza mjadala wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa kwa maslahi ya watanzania, Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla. Hakuna kulala, Mpaka Kieleweke.
CHADEMA: Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli
Imetolewa na:
John Mnyika
Aliyekuwa Mratibu wa timu ya kampeni
Na Mkurugenzi wa Vijana Taifa
0754 694 553
www.chadema.net
18/11/2006