East African Federation (EAF) public Views

East African Federation (EAF) public Views

Mikael
kama wabunge 15 kati ya mamia wa CCM hiyo ni fair, ni sawa na shule kuna walimu wanafundisha si ajabu kuona kuna ndugu zao. mmoja au wawili.
sasa katika wabunge 11 wa chadema halafu tizama wenye ujamaa na viongozi au watoto wao karibu 95%.na huo ndio mwanzo tu.

nakubali Chadema kuwa na urafiki na conservative party sababu sera zao zinafanana kwani conservative wanapalilia ubaguzi similar 2 Chadema ambao nao wanapalilia ubaguzi wa kimajimbo na ukabila.
kwa mtaji huo ndoa yao itakuwa na nguvu kubwa sana.

kuna sehemu bwana Mnyika anadai kuwa tayari mwenyekiti wa chadema atakayemfuatia Mbowe anajulikana kwa wale wanaoifuatilia chadema. kwa kauli hiyo inaonyesha kuwa demokrasia haipo huko, sababu tayari mwenyekiti

watu wanaye mfukoni.hata kabla ya uchaguzi ndani ya chama. kinachosubiriwa kwenye uchaguzi ni mchezo wa kuigiza kama kesi ya saddam ambapo hukumu imeshatolewa.

chukulia mfano mwezi wa nne mwaka jana hakuna aliyejua nani atakuwa mgombea wa ccm hadi ulipokwisha uchaguzi ndio akajulikana nani atakuwa mgombea. jifunzeni demokrasia ndogo kama hizo kama kweli mna claim mna chama cha siasa otherwise nazidi kuamini ni NGO ya Mzee Mtei.

Mheshimiwa Mnyika pole na safari na wala usipoteze kujibu tena hoja zangu kwani wapambe wako hawataki tujue zaidi juu ya chadema ndio unaona tunaambiwa hatuna fikra na tumetumwa na makamba.
jifunze siasa za ulaya ambapo kila jambo linajadiliwa kwa uwazi na viongozi wako tayari kukosolewa na kupingwa.

kuna mtu ameuliza kazi ya kanisa naomba pitia mwanakijiji.podomatic.com kwenye mahojiano murua aliyofanya mwanakijiji na DR.Njozi kwenye kitabu chake kuna facts nyingi sana kuhusiana na hujuma za kanisa katoliki na elimu tanzania.

Mnyika
uhuru wa kweli unadai mbona hata kuhoji tunazuiwa na kuambiwa tumetumwa na makamba?

kingine jitahidi upate maoni ya weusi UK juu ya siasa za conservative party hata kama mnakula mlungula wao ila mjue vipi sera zao. huo nao ushauri wa bure kwenye NGO ya mzee Mtei.
 
Buddies.

Sidhanikama tunahitaji kujiuliza twice kuhusu huyu Chinga, and we aint get nowhere with this "Chinga", yaani kaanza kuleta hoja za akina Nchimbi, Kamala et al.............

Tahadhari
1 Nungwi (Ngw) is the quantity of stupidity in 1000 mature people who have lost 63.3% or (1-exp(-1)) of their reasoning power. The level of stupidity in a normal person is between 2 to 10 microNungwis and it is normally unnoticeable. People start showing abnormal behavior when their stupidity level reaches abot 100 microNungwis and it becames alarming when it reaches 1 milliNungwi.

It is advised to stay away from whoever records stupidity level of above 1 milliNungwi. Sporadically people with stupidity levels of up to 1 full Nungwi have been observed but they are very rare, appearing once in about 100 years per continent. (Kichuguu, 2006)

Wazee jibuni hoja kwa wakati wenu, asiwaendeshe huyu kijana
 
Mzee Chinga,

Damn! Ulikuwa wapi siku zote bro? Hii forum inahitaji watu kama wewe BOLD! na Strong! I mean all the respect kwa JJ na supporters, lakini do not dis-miss this kid Chinga, bravo! let JJ ajibu maswali fair kutoka kwa mwana-forum hii ambayo hata JJ anaiheshimu siku zote kuwa ina watu wanaoelewa ndio maana hajaenda darhotwire,

I mean, please let the kid aulize yanayomkera na Chadema jamani, hapa hakuna free pass, unataka kuwepo hapa lazima upewe joto we all go through this kila siku, acheni mambo ya golden glove hapa,

Mzee O,

Muache kijana aulize maswali, and more respect kwa JJ, so far hajakasirika maana anaelewa kwa wale tulioko bongo na siasa, haya ni mambo ya kawaida, sasa mtatisha vijana waogope kuuliza maswali hapa WHY? No Chinga endeleea na maswali, kuna nisiyoafiki kati ya maswali yake lakini I like the attitude ambayo ni mawe tu!
 
Chinga ,naomba take time ku study namna uongozi ndani ya ccm unavyojeuka wa kifalme...sio unabisha tu wakati facts zipo...
 
Chinga,

endelea tu kuuliza ni haki yako.

Ila uliza with logic na tumia takwimu with research mathalani:

1. Umesema asilimia 95+ ya wabunge 11 wa CHADEMA wanaundugu na viongozi wengine? What a mockery! Hebu tutajie nani ana undugu na nani kati ya hao 11, orodha yao inapatikana kwenye website ya chama!

2. Umesema kwamba nimesema mimi ndiye nitakuwa mwenyekiti wa CHADEMA. Hebu tuonyeshe ni katika post ipi hapa nimesema maneno hayo?

Otherwise, endelea kuuliza-ila uliza maswali makini ili usije ukajivunia heshima kwa watu mahiri katika Forum hii!

Endelea kuuliza, Endelea kuuliza. Nitajibu yote nikifika nyumbani. Na wengine-endeleeni kuuliza na pengine kujibu mkipenda.

'This is grassroot, netroot and the rise of people powered politics'!

JJ
 
Mnyika
samahani mimi si CCM, nilikuwa natoa maoni yangu kwenu raha ni hoja kujibiwa na hoja na si kunishtumu.kauli mbiu yako ya uhuru wa kweli ni theory tu?

Mwanasiasa
unashangaa nini kuona wabunge wa chadema wanalala bungeni?sababu wengi waliokwenda huko ni familia ya vigogo wa chadema na hawakuwa na mdadi wa siasa, unategemea nini toka kwao zaidi ya kuupiga usingizi tu.hamuoni Chifupa anavyoweka vitu sawa! wajifunze kwake.
 
Mzee JJ,

Hebu tu-switch the subject kidogo, ni nini msimamo wa Chademna kuhusu suala zima la Richmond? Chadema ina altarnetive zipi as far as suala zima la umeme is concerned? Je tutaendelea kuishi kwenye giza mpaka lini? Mbona mnakuwa bubu saana kwenye hizi issue muhimu at the time,

maana binadamu tunaoishi kwenye giza tutafanya mambo gani ya maana kwa maendeleo? Maji hatuna, umeme hatuna, usafiir ndio hivyo Mungu nisaidie, sasa upinzani mnayo platform nationally, as opposed to sisi hapa froum, ni nini hasa msimamo wa Chadema na hizi kero? au mpaka wakati wa uchaguzi wa rais ndio mtaziongelea?
 
Mzee Es,

Nashukuru....

1. We can't switch subject mpaka nijibu hoja za Chinga. Umeme ni suala moja kubwa, uhai wa oppossition ni suala moja kubwa zaidi. Kwa kuwa kama hoja tenge za watu kama chinga zikiachwa zikaelea zitachafua upinzani na hivyo kuukosesha hata uhalali wa kusema hoja mbadala kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuhusu umeme!. Kuwa na siasa chafu na uongozi mbovu ni root cause, kwa hiyo lazima tuijadili katika sekta zote. Hata behind Richmond ni hili tatizo mzizi, Richmond ni matokeo tu na hata kukosa umeme ni athari tu za matokeo

2. That withstanding, CHADEMA tumezungumza kuhusu Richmond na hata IPTL. Oktoba Mbowe aliipa serikali terms, majibu ya karamagi yamejibu baadhi ya hizo terms. Sasa tutakwenda hatua nyingine mbele. Tunatambua ukubwa wa tatizo na umuhimu wa umeme. Hatupaswi kuingia kwenye band wagon ya kutoa short term solutions to a long term challenge. tarajia kutusikia soon on this regard, sitaki kusema mengi nitatoa habari za ndani za chama kwa swala ambalo liko 'karibu kupakuliwa'

Jamani nitachelewa ndege....

I miss home!

JJ
 
Mnyika
nyinyi mnataka kutuongoza watu milioni 40 huku maswali ya msingi hamtaki kujibu. narudia tena Mbowe na Mtei na ujamaa gani?
pia fuatilia kwa sana siasa za Michael Howard,Anne Widescombe,na hasa wakati wa uongozi wa William hague.

nahofia ndoa yenu na conservative mmeingia tu kichwakichwa bila kujua msimamo wa hicho chama?ni sawa kipindi cha kutafuta uhuru wa South Africa then kije chama toka nchi nyingine ya africa let say Zambia kikajiunga na makaburu huku kikidai kinakuza demokrasia, mfano huo ndio ndoa ya chadema na David Cameron.

natoa mfano mzuri na wa wazi. hivi karibuni David cameron ametangaza nia yake kwamba akiingia madarakani Human rights Law ataiondoa ili kuona Immigrants hawapati loop hole ya kuishi U.K

pia fuatilia sana siasa zao na hata sera uone zina mlengo gani? ubaguzi tu. pia hatuna historia ya hicho chama kuwa na interest nje ya nchi yao.
BLAIR na vuruga zake zote lakini ana moyo fulani na wafrica.
alipoingia tu madarakani aliwapa ukazi wa kudumu watu 56,000 na kabla ya hapo ilikuwa Major John NA Magret thatcher wanawaweka tu watu na hata makazini wanafuata wageni na kuwa deported.

1997 blair na Labour wameingia madarakani na mwaka mmoja tu Human rights law ikapitishwa na kuwa officially enforced on 2-10-00.
hapo bwana Mnyika utaona kabisa chama mlichofunga nacho ndoa kimejaa uovu.

2003-Labour wakatangaza Family amnesty kuwafikilia watu ambao hawana vibali ambapo watu karibu laki na nusu wakapewa ukazi.
sasa Cameroon amesema akiingia tu kazi ya kwanza ni kuondoa human rights act 1998.

jiulize katika africa wapi viongozi wakuu wa chama hicho wamefanya kweli?
Labour ni chama cha wanyonge na cons ni watu wenye nacho hawataki wengine wapande juu na kama kupanda wawe waingereza na si mgeni au mweusi.

najua zaidi ya gea ya siasa kuna kitu kati ya Chadema na conservative deal za diamond na mabwanyenye ya conservative. fuatilia utakuja kuniambia usiwe na jazba tu.jj
 
Chinga,
Mshikaji unazo point zako kwa Chadema kama chama lakini huyu JJ Mnyika sidhani kama yeye ni issue hapa zaidi ya kuwa na mama kutoka Kaskazini. Afadhali JJ Mnyika mara mia na kabila lake kwani anatuonyesha mavitu hapa... ukabila ama udini huja pale waliochaguliwa hawana uwezo kabisa na wanatumia madaraka hayo kueneza Ukabila ama dini zao. . Sasa kama wewe wampima yeye kwa kabila lake hali sioni maoni yake ya Kikaskazini hapa utakuwa wewe Mkabila.

Hao wengine ambao umedai kuwa wamepewa madaraka kwa sababu ya Ukabila na dini zao nadhani tunahitaji majina zaidi. Tutapima uwezo wao ktk nafasi walizopewa na sio lazima iwe kulingana na elimu zao ama division. Freeman na Mtei limefika na ujumbe huu sii mpya. Tupe zaidi kwani Mtei na Free sio wanaoitengeneza Chadema.

Swala la kuwa conservative nadhani wewe ndiye umelielewa vibaya. hao conservative wa UK watahifadhi culture zao za Kizungu kwa hiyo mtu mweusi ni mgeni. Chadema ipo TZ na wanaweza kabisa kutumia mfumo huo kupigania hifadhi ya culture zetu na hao wazungu ndio wakawa wageni. Kwa hiyo mfumo na sera zinaweza kuwa sawa ama kufanana kabisa lakini wahusika ndani wakatofautiana.

Unaposema Wazawa haina maana ni kwa wazungu tu tukifuata mfano wa UK... bali wazawa kwa TZ ni wewe na mimi.
 
Mkandara
sijamshambulia Mnyika kama mnyika ni kutokana na Tamko alilolitoa ndio nikawa najaribu kudadisi na kuona hali halisi kati ya chadema na Ccm.
Kama umesema suala la Mbowe na Mtei sio jipya basi hata karume naye amechukua urais toka 2000 iweje liletwe leo?

Mkandara usiwe na jazba, na kupenda tu kitu bila kufanya tathmini ya maana mie nina huruma zaidi kwa Mnyika kwani ni mtoto mdogo ambaye angekuwa shule muda huu ila kundi alilonalo linampotezea muda.kwani hata pata kitu pale zaidi ya kupoteza muda yeye hivi sasa priority kwake ni kupata digrii ya uhakika. hivi vi allowance vya safari wanavyomdanganya navyo akina Mbowe havitamsadia.

chukua mfano mwingine CCM ndio karume tukubali karithi kwa baba yake na hata kukiwa na kifo warithi huwa ni ndugu wa karibu kama watoto wa marehemu, kaka au dada.

lakini kichekesho cha chadema wamempa kiti MKWE.
hivi wewe mkandara ukijaza fomu yeyote unaulizwa ndugu zangu jee umewahi kuona sehemu ya mkwe? hapo hata mnyika alitakiwa ajiulize.

kumbuka kuwa Mtei alipokuwa gavana benki kuu, makani alikuwa naibu wake na Mbowe alikuwa karani pale, ukafanyika usanii nakuondoka na mlungula heavy.
halafu ndio ikaja deal ya kuanzisha NGO YAO (Chadema),
sasa Mnyika hajui hapo pana game tu,inatakiwa yeye akasome muda huu then arudi 2010 lakini hivi sasa kupoteza muda wake kujibu au kutoa matamko ni kupoteza muda wake.
kama wanampenda wampeleke naye Hull University.

Mkandara sijakulielewa kuhusu conservative lakini chukua mfano huyu kiongozi wao mkuu katangaza kufuta haki za binadamu(human rights act)jee unao uwezo wa kumtetea mtu huyu anayeshirikia na chadema?nilidhani chadema wanasimamia haki za binadamu sasa iweje mshirika wao mkuu aseme hatotambua haki hizo akiingia madarakani,
iwe zitanigusa mimi au laa lakini haki za binadamu duniani kote zikivunjwa mtu makini lazima ataguswa tu.

Mnyika rudi shule huu ni ushauri wangu wa bure hao wanajuana toka benki kuu ni kama NGO au saccoss fulani, sasa usipoteze muda wako hawa wenzako wako kwenye biashara,kama pesa tutakuchangia ukasome hata uganda, najua Mbowe hana elimu hivyo hawezi kukupa huu ushauri. anataka wajinga muwe wengi ndani ya chama.tizama mwenzako Zitto kakamilisha mambo ya shule ndio kaja hapo. na kama nilivyokuusia huko nyuma uenyekiti chadema atachukua mtoto wa Mbowe kumbuka atakuwa na referees wawili.

Babu(mtei) na mbowe mwenyewe,jiulize mjukuu wa mtei atakosa vipi ikiwa Mkwe kapata huyu mjukuu atakuwa na nguvu zaidi atasema baba yangu alikuwa mwenyekiti na babu yangu alikuwa mwenyekiti, nani atapinga?wakati huo watakutupa wewe lakini ukiwa na elimu yako unasonga mbele.kumbuka Kaburu kapata misukosuko mingi ndani ya chadema na wakampiga pande,alikuja kugundua kuwa yuko kwenye saccoss na si chama,

Chadema kwa sera ilizo nazo haina ubavu kwa kuchukua nchi.hadi ibadilike toka kwenye saccoss,ngo NA kuwa chama kama Taasisi si kikundi cha mzee fulani mjanja aliyempata mkwe wake.
 
Chinga,
Wala sina Jazba kabisa... labda hujanikuta nikipandisha..
Mimi nimependezewa na baadhi ya maswali yako, ni kibano safi na lazima watu washtuke lakini lugha uliyotumia ndio hiyo ya ushabiki wa YANGA na SIMBA. Watu kama mimi sina U -CCM wala CHADEMA kwa hiyo mnapoanza kulinganisha kati ya CCM na CHADEMA ni sawa na kunambia tuyakubali mapungufu ya vyama hivi kwa kuzingatia nani nafuu.

Jambo jingine ambalo kidogo limenitoa handasi ni kuipaka tope elimu ya JJ ambaye nina hakika hakusema mahala popote juu ya elimu za viongozi wa CCM na division zao kulinganisha na yake.. JJ ni mtu wa Vijana kama alivyo Amina Chifupa sasa hapa tukianza kutumia darasa la mtu na pass zake sijui kama tutafika. Issue inakuwa watu badala ya majukumu aliyopewa.

Amina Chifupa anafanya mavitu kuliko hata baadhi ya wasomi CCM, huyu mtoto kweli mtoto loto...linajua kuongea na hakika ni tamasha la watoto/vijana kwa hiyo sifa zake zinamtosha. J.J naye ni ngoma tofauti kabisa. Sidhani kama ni ligi moja kwani michezo yao tofauti kabisa.
Freeman na Karume ni issue za ushabiki. Tuzungumzie malengo ya kuwepo mtu huyo ktk nafasi ile. Freeman kaonyesha kuwa kiongozi bora kuliko hata Mtei na Karume pia ana uwezo mzuri kuliko marehemu baba yake ktk Uongozi kutokana na wakati. Sii dhambi kufuata nyayo za mzazi na nijuavyo mimi watoto wengi hujifunza mengi toka kwa wazazi wao ama wakwe!..

Wee nambie kama Mtei kamweka Freeman ili wapate KULA hapo mshikaji nitakuskia sana na hao watu wa Chadema kama wataweza kutupa ushahidi kuwa Karume kapachikwa ili familia ya marehemu ipate KULA.
Udini na Ukabila vilevile iwe ktk kutpa sisi picha kwamba wanachaguana kwa madhumuni ya kutetea/kuendeleza makabila yao ama dini zao.

Samahani lakini nadhani nimeeleweka na wala sii kusudio langu kukuondoa ktk mada hii, isipokuwa ningependa kuona hoja zenye upeo mkubwa zaidi kama vile ulivyouliza mwanzo kuhusu uongozi wa Chadema.
 
Mkandara
mie si CCM kama ninavyopakaziwa ila tamko la chadema lilikuwa linaelezea undugu na kujuana kwenye ccm na aliyetoa ni Mnyika, nikaona nimfahamishe kwake kulivyo, na kama angetaja vyama vingine navyo ningevitizama kwa kina sana.

Mknadara kuna watu waliwafuata akina Mabere marando. lamwai, fundikira, mzee Mapalala na hadi kudiriki kuandamana na wengine kufukuzwa masomo bila kufanya utafiti wa kutosha toka kwa watu hao. temeke vijana wengi wameumia kwa kumsikiliza Hiza Tambwe, sasa Mnyika na wengine wajiulize kwanza kwao kabla ya kwenda kwingine,nikitiza mtandao wa akina MTEI.MAKANI NA MBOWE(TRIPLLE M) napata shaka kubwa, kumbuka hawa watu wamefanikiwa sana leo hii kutokana na utawala au chama wanachosema hakifai, jee kweli wako serious?kama ulifuatilia mchezo wa Lamwai alipokuwa anamkingia kifua Mrema temeke. mara akawa ccm damu.

fundisho hawa watu walioneemeka ndani ya mfumo wa ccm hawawezi kuwa wapinzani halisi, wapo kwenye ajira tu.Mbowe hajawahi kupata tabu yeyote maishani leo awe mpinzani? majengo yale ya bilicanas yalipatikana bila mkono wa ccm?

ndio maana nikasema natoa ushauri wa bure, mtaochukia chukieni najua ukweli unauma ndiyo maana kila mtu akija anaweza jina langu.
Elimu na uongozi ni vitu viwili tofauti. na wala siamini elimu inatoa kiongozi bora au mfanyabiashara bora.wapo akina Bill gates wamefika mbali bila digrii na elimu aliyonayo Mnyika inatosha kuongoza chama kwani mwenyekiti wake hana hata elimu ya mnyika na hata makamba. ila mjadala wa elimu ulikuwa na hiojo tofauti, eilikuwa inahusu wakristu kupendelewa kielimu, ndio jina la mnyika likatajwa humu.unaweza kuifutilia hiyo story kwa mwanakijiji.podomatic.com.
 
Mkandara umesema kweli. Tuna uhuru wa kusema, lakini maneno mengi ya Chinga si mazuri. Sitaki kusema ni mabaya. Watu wanajadili hoja yeye anawalazimisha ukabila, uhusiano n.k. Anamkejeli JJ bila sababu. Anataka kumjengea chuki na wenzake. JJ ameshasema huko juu kwamba hawa wanaomshambulia wakaacha hoja, ni wachovu, wanamchukia kwa sababu amewakataliwa kwenda CCM. Nashangaa Chinga kuona kama Kaburu ni mtu wa maana.

Ni hivi, watu hawa aliokuwa nao walikuwa waungwana kutomuumbua. Na ingawa hawakusemwa hadharani (hawakutaka kumwaga mtama barabarani maana ya NCCR hayajasahaulika) sisi tulio nje tulikuwa tunawaonea huruma...tulimjua kuwa alikuwa mzigo kwao. Unakumbuka lo lote alilowahi kufanya likasikika kitaifa? Chama chao kimesikika baada ya akina Kaburu kuondoka....kilidumaa hadi walipofanya mabadiliko ya uongozi. Na inaonekana mabadiliko hayo yaliyomtema Kaburu ndiyo yaliyomfanya awe msaliti wa wazi hata sisi tulio nje tukagundua.

Huyu huwezi kumwona wa maana kuliko vijana wanaoibukua kina JJ. Wala hatuwezi kumuunga mkono binadamu mwenzetu anayewakatisha tamaa wanaofanya vizuri...Chinha jirudi bwana!
 
Eeeh bwana wee! yes, Chinga ngoma nyingine kabisa.
Mzee nimepoa mwenyewe sina hoja zaidi! wewe kiboko bob inabidi CCM wakutafute. Duuuh!
 
MKANDARA
Ccm wanitafute kwa shughuli gani? nimeuliza na kutoa hoja kwa fikra zangu nadhani zinahitaji kupata majibu makini.
ninakumbukumbu nzuri ya vyama vya siasa, nakumbuka Mapalala alikuwa akiwatorosha vijana shuleni na kufanya mkutano kinondoni kwa wiki mata tatu. vijana wengi wakakosa mwelekeo na kusahau elimu wakitajia kupata chochote kwa Mapalala leo wanajuta.
 
Kichwamaji
hakuna nukta yeyote niliyosema Kaburu ni kiongozi makini, naomba nionyeshe, kuondoka kwake chadema haina maana kuwa ni makini.
unadai nina nia mbaya? kwanini niwe na nia mbaya? ninachojadili kama mtu mtu mwingine
 
Chinga,
Sikuwa na maana mbaya... nina maana kama wewe sii mwanachama basi Wanatakiwa watu kama wewe huko CCM. Nimegundua kwamba Chadema na CUF wana watu ambao wanaweza lugha kama hii lakini CCM siku zote wao hubaki na kiswahili cha kisomi kuita watu wapumbavu ama wanaona wivu na kadhalika. Trust me ni mara ya kwanza kuona mtu akiingia ndani kiasi hiki kwa viongozi wapinzani... utamwacha mtu uchi, bob taratibu...haya unayotupa ni madongo.
 
Mkandara
sio kama napiga madongo, Mnyika anatakiwa aende Tumaini university akachukue Law, Mass-com au b.com kwa maksi zake Tumaini watamchukua.
atizame akina Mbatia walipotezewa muda wao na walifika wapi? sina hakika kama mbatia ana degree yeyote hadi sasa.

Professor Kighoma Malima aliposaidia kupatikana uhuru wa Tanzania akiwa na Tanu then aliahidiwa kupewa ukuu wa wilaya lakini akaomba akasome na tizama alipofika

Mnyika kuna akina guninita John walipoteza muda kwenye hiyo saccoss, leo wako wapi?

huu si muda wa wewe kutoa semina,kongamano au tamko vitu hivyo kwenye NGO au saccoss ni maisha ya kila siku, huu ni wakati wa kuchukua elimu, nasikia ulijiandikisha part time-BBA wawasi wangu huna muda wa kusoma na kwanini usome part time? na muda gani utasoma na wewe uko busy na semina na makongamano ya NGO YA MZEE mtei?

Nina uchungu na kipaji chako naogopa kisije kupotea tu,
Mnyika ukitulia unaweza kula hata phd,tizama wanaokupotezea muda wako watoto wao wako U.K na Marekani wanakula kitabu ili waje kukuongoza hapo,
wewe ni mshika mapembe kwani wakamua maziwa wapo akina Mbowe na mkwewe Mtei.
 
Back
Top Bottom