Ukweli jamani tuseme, sasa kwa wale mnaompinga Chinga kwenye hii mada, mnaonekana kupwaya katika hoja, kama the issue ni ELIMU ya JJJ, Chinga's man is hitting hard, I mean jamaa is going NUCLEAR, au kisiasa siku hizi anayoyafanya yanaitwa Shock and Awe!
Ningewashauri mumuachie JJ mwenyewe ayajibu mapigo, au akubali yaishe aende apate elimu kwanza halafu aje hapa. Chinga anawapiga knockout punch pale anaposema kuwa nyinyi wote mnaomtetea mna elimu, tena kubwa sana, sasa iweje mumwambie mwenzenu kuwa kutokuwa na elimu sio tatizo hata CCM hawana elimu? Wakati Keeenja wa CCM moja ya sababu ya kumshinda ubunge JJ, ilikuwa ni pamoja na elimu kubwa aliyonayo?
On this kwakweli, kubalini yaishe maana sisi forum hatuwezi kutetea viongozi wasiokuwa na elimu eti kwa sababu taifa tuna viongozi wenye elimu lakini wanaonekana kama hawana kutokana na maamuzi yao, nafikir ni the lowest excuse kifikira iliyowahi kutamkwa na mwana forum hii toka ianzishwe, na we katika hii forum we are not about kuikubali kama authority against moja ya maadui wakubwa wa taifa letu yaani, ujinga.
Matajiri kina Mike Tyson, kutojua namna ya kuutumia utajiri wao haiwezi kuwa kinga kwa wengine kutotafuta utajiri, NONESENSE! Bahkressa ana hela kuliko Mengi, lakini siku zote Mengi anaonekana kuwa na hela zaidi kuliko Bakhress, WHY? Elimu!
Kuna issues nyingi ambazo zitajadiliwa katika kipindi cha hawa viongozi wa Chadema kuwepo hapa, mojawapo ni elimu yao ndogo kulinganisha na dunia tuliyonayo sasa hivi, asiyekubali kushindwa sio mpinzani. Kwenye mchezo wa ngumi kuna raundi 12, kwa kawaida mabondia hugawana raundi ingawa hatimaye mmojawapo hushinda, sasa ndugu zangu maapologists wa Chadema kubalini tu kuwa raundi ya elimu kwa viongozi wenu wa juu, siyo yenu na mmeshindwa ili tuangalie raundi zingine tusije tukakwama kwenye raundi ya kwanza, ni lazima tu-move on na raundi nyingine, ila kwa elimu ya viongozi wenu wa juu ni lazima mkubali kuwa ni ndogo mno, katika ulimwengu huu wa teknologia, ni the right thing to do!
Na Chinga boy, bravo kwa kusimamia hoja yako ki-forum hiii style, yaani MAWE tu, yaani wewe ndiye kumkoma nyani giladi mwenyewe bro, ninakuvulia kofia,
ahsante ndugu zangu na tuvuke kwenye mjadala mwingine sasa! kama watu wazima!