1. Mfumo wa sebule kukaa kati kati na kufanya isiwe na madirisha ya pembeni inafanya mzunguko wa hewa uwe mdogo na pia kutoruhusu mwanga wa kutosha, kipindi cha kiangazi utakuwa huwezi kukaa tena sebleni kutokana na joto
2. Kuna bedrooms mbili ambazo mtu hawezi kutoka nje ya nyumba bila kupitia sebleni japo bedroom moja kati ya hizo ina option nyingine ya kutoka kipitia store>>kitchen (kitu ambacho sio vizuri pia)
3. Mlango wa kuingilia jikoni kukaa kati kati kunazuia nafasi isitumike ipasavyo (mlango siku zote huwa unakaa pembeni ili kuruhusu nafasi ya upande mwingine kutumika bila kuzuiwa na ufunguaji/ufungaji wa mlango)
4. Mpishi akitaka kwenda toilet ni lazima apitie sebleni vinginevyo inabidi atoke nje ya nyumba aje kutumia choo cha nje (hiki ambacho kimetengwa kama choo cha master bedroom)
Nakiita master bedroom ili tuelewane lakini hakistahili kuitwa master bedroom kutokana na contents zake
5. Ukiangalia vizuri utagundua kwamba store ni kubwa kuliko hata jiko lenyewe
6. Bedroom ambayo imelengwa itumike kama Master bedroom ina dirisha moja tu tena dirisha lenyewe ni la upana wa futi 4 (hii ramani inaweza ikaua watu kwa suffocation)
7. Vyumba vingi lakini vyote ni single bedrooms (mtu yeyote akitaka kwenda toilet ni lazima atoke nje ya chumba, kwa maana hata self bedroom moja hakuna)
8. Bedrooms zote, milango yake imegeuzwa (ilipaswa ifungukie upande tofauti na huu uliowekwa ili mtu akifungua mlango wakati wa kuingia au kutoka, sehemu kubwa ya chumba iwe imezibwa na mlango)
Hapo jinsi milango ilivyowekwa, hata mtu akifungua mlango wa chumba kwa nyuzi 45 tu basi anaona kila kitu ndani ya chumba lakini kama ingegeuzwa, hata mtu afungue mlango kwa nyuzi 90 bado ataona sehemu ndogo sana ya chumba (ni kama strip tu yenye upana unaolingana na upana wa mlango)
9. Choo cha chumba cha master bedroom ni kidogo kuliko vyoo vyote, ikumbukwe kuwa choo cha master bedroom kinatakiwa kiwe kikubwa kwa kuwa sometimes unakuta partners wanataka wakaoge wote pamoja (hasa mishahara ikiingia, natania), achilia mbali mambo ya kuogeshana kuna vitu kama sehemu ya kupiga mswaki, kubadilishia nguo n.k
Nimeelezea hayo machache, wengine wataongezea.
Imekuwa heri upande wako kugundua baadhi ya makosa kabla ya kuanza ujenzi, maana kuna boss mwingine ukimpatia ramani haelewi chochote kwa hivyo yeye akipatiwa tu ramani anaanza ujenzi hapo hapo (atakuja kugundua makosa baada ya nyumba kukamilika)
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane