Ebu tuichambue hii ramani ya nyumba, kwanza sijapenda dining kuambatana na choo, kipi kingine umekiona?

Ebu tuichambue hii ramani ya nyumba, kwanza sijapenda dining kuambatana na choo, kipi kingine umekiona?

Ramani ya hovyo sanaa. Vyoo vitatu vyote ni public, na kimoja kuingia hadi utoke nje! Bora bedroom 2 zingekuwa na choo ndani, choo kilichobaki kiwe public. Jiko linalingana ukubwa na store yake? We uliskia wapi? Punguza ukubwa wa store, ongeza jiko. Halafu store ya jiko ina mlango wa kutokea chumbani, wa nini? Punguza dead spaces (lobby, corridor), ongeza usable spaces e.g. dressing room; gross floor area ya nyumba ni kubwa; but very poorly designed floor plan!
Mchoraji wa hii ramani kafeli pakubwa mno, mwenyewe nilijuuliza pia, mtu anatokaje chumbani,Kisha apitie stoo, atokee jikoni, Kisha aende sebleni. SIKUPATA majibu kabisa
 
Raman yoyote ya nyumba mm huwa naangalia sewage system.
inapendeza sana sewage ikawa inapita pande mbili. au moja.

sewage haitakiw ionekane unavyoingia mbele ya nyumba.

ila hapo naona iko pande tatu.
na inaonekana.

kwa kigezo hiko. kwangu mm hiyo sio raman nzur.
Upo sahihi, kitaalambr residential bouses, sewage inatakiwa one side, ikizidi 2 side,
Sababu kubwaa mi Kwa aniro ya easy installation na icho ulichokise.
 
Au hii ndo ramani ya vita? 🤔
Ha ha ha...mi nahs atakua mwanachuo.
Engineer ata fundi mchundo au yyt mwenye uzoeefu WA ujenzi, kamwe hawez toa raman mbovu kiasi hiki.

Hii ramani ata kuipaua ni ngumu Sana, Kuna Kona hazipauliki, vinginevyo litatoka PAA kituko
 
Kiukweli Hii ramani ya mtoa mada, ina makosa mengi mno, haijazingatia kabisa kanuni za ujenzi.

Kafanya jambo la busara sana kuilta jf, kabla ya kuzamisha pesa, kutoa nyumba kituko
Hapo unakuta ameshapata malipo yake, sasa muambie habari za marekebisho uone kama mtaelewana. Atakuambia hiyo ni kazi nyingine, tunabargain upya
 
Hapo unakuta ameshapata malipo yake, sasa muambie habari za marekebisho uone kama mtaelewana. Atakuambia hiyo ni kazi nyingine, tunabargain upya
Ndo hizi ramani, ukiipeleka saiti, unaishia kugombana na fundi, kumbe fundi Kazi yake kujenga tu, na sio kukosoa ramani
 
Ndo hizi ramani, ukiipeleka saiti, unaishia kugombana na fundi, kumbe fundi Kazi yake kujenga tu, na sio kukosoa ramani
Ni mafundi wachache wenye moyo wa kubeba hayo majukumu, fundi mwingine anakuambia hela ya kuchora ramani ale mwingine mimi huku site nipate shida ya kuumiza kichwa kwa faida gani, najenga kama ilivyo tusisumbuane akili[emoji846][emoji846][emoji846]. Ila ukimuahidi kumnunulia msosi na maji/sigara sijui energy, analegeza msimamo
 
Ndo maana Kampuni makubwa(hasa ya nje),kabla ya ramani kulipiwa au kujengwa, inaletwa mezani

Structural Engineer wanaijadili contractors wanaijadili,
Quantity surveyors wanaijadili,
Wataalam WA mifumo ya umeme wanaijadili,
Wataalam WA mifumo ya maji wanaijadili,
Wataalam WA sayansi ya ardhi wanaijadili,
Mipango miji nao wanaijadili,

Ikionekana Iko sawa, inapitishwa ndo mchoraji analipwa 75% ya malipo husika.

Na mchoraji ramani anapaswa kua active muda wote WA ujenzi, akifanya kazi Kwa kushauriana na wataalam wote WA ujenzi.

Saiti ikikamilika, analipwa 25% yake iliyobaki
 
1. Mfumo wa sebule kukaa kati kati na kufanya isiwe na madirisha ya pembeni inafanya mzunguko wa hewa uwe mdogo na pia kutoruhusu mwanga wa kutosha, kipindi cha kiangazi utakuwa huwezi kukaa tena sebleni kutokana na joto

2. Kuna bedrooms mbili ambazo mtu hawezi kutoka nje ya nyumba bila kupitia sebleni japo bedroom moja kati ya hizo ina option nyingine ya kutoka kipitia store>>kitchen (kitu ambacho sio vizuri pia)

3. Mlango wa kuingilia jikoni kukaa kati kati kunazuia nafasi isitumike ipasavyo (mlango siku zote huwa unakaa pembeni ili kuruhusu nafasi ya upande mwingine kutumika bila kuzuiwa na ufunguaji/ufungaji wa mlango)

4. Mpishi akitaka kwenda toilet ni lazima apitie sebleni vinginevyo inabidi atoke nje ya nyumba aje kutumia choo cha nje (hiki ambacho kimetengwa kama choo cha master bedroom)

Nakiita master bedroom ili tuelewane lakini hakistahili kuitwa master bedroom kutokana na contents zake

5. Ukiangalia vizuri utagundua kwamba store ni kubwa kuliko hata jiko lenyewe

6. Bedroom ambayo imelengwa itumike kama Master bedroom ina dirisha moja tu tena dirisha lenyewe ni la upana wa futi 4 (hii ramani inaweza ikaua watu kwa suffocation)

7. Vyumba vingi lakini vyote ni single bedrooms (mtu yeyote akitaka kwenda toilet ni lazima atoke nje ya chumba, kwa maana hata self bedroom moja hakuna)

8. Bedrooms zote, milango yake imegeuzwa (ilipaswa ifungukie upande tofauti na huu uliowekwa ili mtu akifungua mlango wakati wa kuingia au kutoka, sehemu kubwa ya chumba iwe imezibwa na mlango)

Hapo jinsi milango ilivyowekwa, hata mtu akifungua mlango wa chumba kwa nyuzi 45 tu basi anaona kila kitu ndani ya chumba lakini kama ingegeuzwa, hata mtu afungue mlango kwa nyuzi 90 bado ataona sehemu ndogo sana ya chumba (ni kama strip tu yenye upana unaolingana na upana wa mlango)

9. Choo cha chumba cha master bedroom ni kidogo kuliko vyoo vyote, ikumbukwe kuwa choo cha master bedroom kinatakiwa kiwe kikubwa kwa kuwa sometimes unakuta partners wanataka wakaoge wote pamoja (hasa mishahara ikiingia, natania), achilia mbali mambo ya kuogeshana kuna vitu kama sehemu ya kupiga mswaki, kubadilishia nguo n.k

Nimeelezea hayo machache, wengine wataongezea.

Imekuwa heri upande wako kugundua baadhi ya makosa kabla ya kuanza ujenzi, maana kuna boss mwingine ukimpatia ramani haelewi chochote kwa hivyo yeye akipatiwa tu ramani anaanza ujenzi hapo hapo (atakuja kugundua makosa baada ya nyumba kukamilika)

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
Naomba namba yako ya simu ili tuwasiliane kuhusu ramani.
 
Huu mpangilio ni mtu anataka kujenga ramani ya ghorofa kwenye flat au?
 
Ya hovyoo bna kuna nyumba nkakuta dirsha la choo linageukia kwenye veranda doh nikachoka asee
 
Yaani hapo kuna vyumba huwezi kutoka mpaka upite sebuleni. Mtu mwenye aibu atakaa chumbani siku nzima kama sebuleni kuna wageni.
 
Ndo maana Kampuni makubwa(hasa ya nje),kabla ya ramani kulipiwa au kujengwa, inaletwa mezani

Structural Engineer wanaijadili contractors wanaijadili,
Quantity surveyors wanaijadili,
Wataalam WA mifumo ya umeme wanaijadili,
Wataalam WA mifumo ya maji wanaijadili,
Wataalam WA sayansi ya ardhi wanaijadili,
Mipango miji nao wanaijadili,

Ikionekana Iko sawa, inapitishwa ndo mchoraji analipwa 75% ya malipo husika.

Na mchoraji ramani anapaswa kua active muda wote WA ujenzi, akifanya kazi Kwa kushauriana na wataalam wote WA ujenzi.

Saiti ikikamilika, analipwa 25% yake iliyobaki
Nakuaminia sana mkuu DeepPond njoo unichambulie na haka kamchoro kama kataonekana
 

Attachments

  • IMG_20250819_144517.jpg
    IMG_20250819_144517.jpg
    1.3 MB · Views: 33
Ni mafundi wachache wenye moyo wa kubeba hayo majukumu, fundi mwingine anakuambia hela ya kuchora ramani ale mwingine mimi huku site nipate shida ya kuumiza kichwa kwa faida gani, najenga kama ilivyo tusisumbuane akili[emoji846][emoji846][emoji846]. Ila ukimuahidi kumnunulia msosi na maji/sigara sijui energy, analegeza msimamo
Hii ni dharau kubwa sana kwa mafundi.
Kwahiyo sisi level zetu ni energy drink na sigara na sahani ya ubwabwa sio?
 
Kingine pia,
Umefanya kosa Kama la mtoa mada,
Masterbedroom umeiweka eneo Moja imepakana na public toilet, halijakaa vizuri. PUBLIC TOILET INGEKAA UPANDE MWINGINE MBALI KABISA NA CHUMBANI KWAKO
Nakuaminia sana mkuu DeepPond njoo unichambulie na haka kamchoro kama kataonekana
 
Back
Top Bottom