Ebu tuichambue hii ramani ya nyumba, kwanza sijapenda dining kuambatana na choo, kipi kingine umekiona?

Afu Nmeona ukitoka KITCHEN,
Kuna milango unaingia STORE,
Afu Kisha Kuna milango unaingia EXIT

Pia hapo hapo,
Hicho kichumba Cha exit,
Kina uwazi unaoingia Moja Kwa Moja (bila mlango) kwenye bedroom ya nyuma, upande wa kulia.

Naomba kujua Hicho kichumba kdg ((kilichoandikwa exit), ndo kina Kazi gani mkuu?

Kwamba Kuna mtu atapaswa kua anaaamka asbh, Moja Kwa Moja anatokea stoo,Kisha anaingia jikoni Hadi anafika sebleni? Au vipi?

Ushauri wangu,
Hicho Chumba Cha EXIT kingekufa,

Kilipaswa kua ni choo Cha self ya hiyo bedroom iliyopakana nayo.
 
Bado Sijaelewa mchoraji wa ramani Hii, hii design yake Kama aliwaza tv itakaa wapi na makochi yatakaa vipi
Upande wa kushoto kuna kodro, mbele kuna dinning na tv, kulia kuna mlango wa kutokea.

Pia sioni kama kuna master bedroom pamoja na kwamba kuna vyoo vitatu
 
Kutokana na ramani ya mtoa mada,

Naona kabisa masterbedroom itakua ni hiyo ya kushoto Kwa mbele
(Naona Ndo bedroom kubwa kuliko zote, na pia ndio Ina choo self, tofauti na zote)

Kosa nnaloliona ni hiyo public toilet kuangaliana face to face na mlango WA kuingilia kwenye masterbedroom ya mshua.

Kikawaida,
Nyumba ya familia inakosa adabu pale choo Cha wageni kinapoangaliana face to face na mlango WA FATHERHOUSE.

Imagine,
-unapiga shoo, afu unaskia mlango WA pili, mgeni anaharisha
Au
-umemtembelea mtu, unamsubiria sebleni, afu unakaribishwa msalani, unaskia miguno Yuko na mkewe masterbedroom WANAPIGA SHOW.

Kiuhalisia,
Masterbedroom inapaswa kujitenga na vyumba vya kawaida au public toilet.

Masterbedroom haitakiwi kua pamoja na vyumba au korido zenye traffic kubwa ya watu, Kwa sababu ya usiri.
 
Madirisha ya bedroom kamwe hayatakiwi kutizamana na vibaraza,

Haiingii akilini, mtu Yuko na privacy yake bedroom afu aanze kuwaza ni nani atakua kakaa kibarazani Kwa MDA huo.

MDA WA joto Kuna watu upenda kukaa uchi bedroom, afu uanze kuwaza watoto wanaocheza kibarazani au wanawake watakaokua wanasogoa kibarazani.
 
Naunga MKONO hoja
Raman yoyote ya nyumba mm huwa naangalia sewage system.
inapendeza sana sewage ikawa inapita pande mbili. au moja.

sewage haitakiw ionekane unavyoingia mbele ya nyumba.

ila hapo naona iko pande tatu.
na inaonekana.

kwa kigezo hiko. kwangu mm hiyo sio raman nzur.
Upande wa kushoto kuna kodro, mbele kuna dinning na tv, kulia kuna mlango wa kutokea.

Pia sioni kama kuna master bedroom pamoja na kwamba kuna vyoo vitatu
Master Itakua ni hiyo ya bedroom ya kushoto Kwa mbele, angalia design ya choo chake
 
1. Mfumo wa sebule kukaa kati kati na kufanya isiwe na madirisha ya pembeni inafanya mzunguko wa hewa uwe mdogo na pia kutoruhusu mwanga wa kutosha, kipindi cha kiangazi utakuwa huwezi kukaa tena sebleni kutokana na joto

2. Kuna bedrooms mbili ambazo mtu hawezi kutoka nje ya nyumba bila kupitia sebleni japo bedroom moja kati ya hizo ina option nyingine ya kutoka kipitia store>>kitchen (kitu ambacho sio vizuri pia)

3. Mlango wa kuingilia jikoni kukaa kati kati kunazuia nafasi isitumike ipasavyo (mlango siku zote huwa unakaa pembeni ili kuruhusu nafasi ya upande mwingine kutumika bila kuzuiwa na ufunguaji/ufungaji wa mlango)

Nimeelezea hayo machache, wengine wataongezea.

Imekuwa heri upande wako kugundua baadhi ya makosa kabla ya kuanza ujenzi, maana kuna boss mwingine ukimpatia ramani haelewi chochote kwa hivyo yeye akipatiwa tu ramani anaanza ujenzi hapo hapo (atakuja kugundua makosa baada ya nyumba kukamilika)

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝🤝
 
Kutokana na ramani ya mtoa mada,

Naona kabisa masterbedroom itakua ni hiyo ya kushoto Kwa mbele
(Naona Ndo bedroom kubwa kuliko zote, na pia ndio Ina choo self, tofauti na zote)

Kosa nnaloliona ni hiyo public toilet kuangaliana face to face na mlango WA kuingilia kwenye masterbedroom ya mshua.

Kikawaida,
Nyumba ya familia inakosa adabu pale choo Cha wageni kinapoangaliana face to face na mlango WA FATHERHOUSE.

Imagine,
-unapiga shoo, afu unaskia mlango WA pili, mgeni anaharisha
Au
-umemtembelea mtu, unamsubiria sebleni, afu unakaribishwa msalani, unaskia miguno Yuko na mkewe masterbedroom WANAPIGA SHOW.

Kiuhalisia,
Masterbedroom inapaswa kujitenga na vyumba vya kawaida au public toilet.

Masterbedroom haitakiwi kua pamoja na vyumba au korido zenye traffic kubwa ya watu, Kwa sababu ya usiri.
🤝🤝🤝🤝🤝
 
haswaa. master bedroom ya kuheshimiwa.

Hili nalo ni la kulipa umakini .
hasa ambao hawajawah kumiliki nyumba.
ukikosea setup ya Master . bas jua nyumba yako mwenyewe ila itakukera.

Inabid ujipendelee 😁😁😁😁.
 
Sahii kabisa, mgeni au MTU baki akifika kwako, hatakiwi kbs kujua uwa unalala Chumba kipi, ndo maana wengi, masterbedroom huziweka mwishoni kabisa mwa nyumba.

Hata ukipigana na mkeo, hakuna alievyumbani au sebleni ataskia
haswaa. master bedroom ya kuheshimiwa.

Hili nalo ni la kulipa umakini .
hasa ambao hawajawah kumiliki nyumba.
ukikosea setup ya Master . bas jua nyumba yako mwenyewe ila itakukera.

Inabid ujipendelee 😁😁😁😁.
[/QUOT
 
1. Mfumo wa sebule kukaa kati kati na kufanya isiwe na madirisha ya pembeni inafanya mzunguko wa hewa uwe mdogo na pia kutoruhusu mwanga wa kutosha, kipindi cha kiangazi utakuwa huwezi kukaa tena sebleni kutokana na joto

2. Kuna bedrooms mbili ambazo mtu hawezi kutoka nje ya nyumba bila kupitia sebleni japo bedroom moja kati ya hizo ina option nyingine ya kutoka kipitia store>>kitchen (kitu ambacho sio vizuri pia)

3. Mlango wa kuingilia jikoni kukaa kati kati kunazuia nafasi isitumike ipasavyo (mlango siku zote huwa unakaa pembeni ili kuruhusu nafasi ya upande mwingine kutumika bila kuzuiwa na ufunguaji/ufungaji wa mlango)

Nimeelezea hayo machache, wengine wataongezea.

Imekuwa heri upande wako kugundua baadhi ya makosa kabla ya kuanza ujenzi, maana kuna boss mwingine ukimpatia ramani haelewi chochote kwa hivyo yeye akipatiwa tu ramani anaanza ujenzi hapo hapo (atakuja kugundua makosa baada ya nyumba kukamilika)

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
4. Mpishi akitaka kwenda toilet ni lazima apitie sebleni vinginevyo inabidi atoke nje ya nyumba aje kutumia choo cha nje (hiki ambacho kimetengwa kama choo cha master bedroom)

Nakiita master bedroom ili tuelewane lakini hakistahili kuitwa master bedroom kutokana na contents zake

5. Ukiangalia vizuri utagundua kwamba store ni kubwa kuliko hata jiko lenyewe

6. Bedroom ambayo imelengwa itumike kama Master bedroom ina dirisha moja tu tena dirisha lenyewe ni la upana wa futi 4 (hii ramani inaweza ikaua watu kwa suffocation)

7. Vyumba vingi lakini vyote ni single bedrooms (mtu yeyote akitaka kwenda toilet ni lazima atoke nje ya chumba, kwa maana hata self bedroom moja hakuna)

8. Bedrooms zote, milango yake imegeuzwa (ilipaswa ifungukie upande tofauti na huu uliowekwa ili mtu akifungua mlango wakati wa kuingia au kutoka, sehemu kubwa ya chumba iwe imezibwa na mlango)

Hapo jinsi milango ilivyowekwa, hata mtu akifungua mlango wa chumba kwa nyuzi 45 tu basi anaona kila kitu ndani ya chumba lakini kama ingegeuzwa, hata mtu afungue mlango kwa nyuzi 90 bado ataona sehemu ndogo sana ya chumba (ni kama strip tu yenye upana unaolingana na upana wa mlango)

9. Choo cha chumba cha master bedroom ni kidogo kuliko vyoo vyote, ikumbukwe kuwa choo cha master bedroom kinatakiwa kiwe kikubwa kwa kuwa sometimes unakuta partners wanataka wakaoge wote pamoja (hasa mishahara ikiingia, natania), achilia mbali mambo ya kuogeshana kuna vitu kama sehemu ya kupiga mswaki, kubadilishia nguo n.k
 
Ramani ya hovyo sanaa. Vyoo vitatu vyote ni public, na kimoja kuingia hadi utoke nje! Bora bedroom 2 zingekuwa na choo ndani, choo kilichobaki kiwe public. Jiko linalingana ukubwa na store yake? We uliskia wapi? Punguza ukubwa wa store, ongeza jiko. Halafu store ya jiko ina mlango wa kutokea chumbani, wa nini? Punguza dead spaces (lobby, corridor), ongeza usable spaces e.g. dressing room; gross floor area ya nyumba ni kubwa; but very poorly designed floor plan!
 
4. Mpishi akitaka kwenda toilet ni lazima apitie sebleni vinginevyo inabidi atoke nje ya nyumba aje kutumia choo cha nje (hiki ambacho kimetengwa kama choo cha master bedroom)

Nakiita master bedroom ili tuelewane lakini hakistahili kuitwa master bedroom kutokana na contents zake

5. Ukiangalia vizuri utagundua kwamba store ni kubwa kuliko hata jiko lenyewe

6. Bedroom ambayo imelengwa itumike kama Master bedroom ina dirisha moja tu tena dirisha lenyewe ni la upana wa futi 4 (hii ramani inaweza ikaua watu kwa suffocation)

7. Vyumba vingi lakini vyote ni single bedrooms (mtu yeyote akitaka kwenda toilet ni lazima atoke nje ya chumba, kwa maana hata self bedroom moja hakuna)

8. Bedrooms zote, milango yake imegeuzwa (ilipaswa ifungukie upande tofauti na huu uliowekwa ili mtu akifungua mlango wakati wa kuingia au kutoka, sehemu kubwa ya chumba iwe imezibwa na mlango)

Hapo jinsi milango ilivyowekwa, hata mtu akifungua mlango wa chumba kwa nyuzi 45 tu basi anaona kila kitu ndani ya chumba lakini kama ingegeuzwa, hata mtu afungue mlango kwa nyuzi 90 bado ataona sehemu ndogo sana ya chumba (ni kama strip tu yenye upana unaolingana na upana wa mlango)
Kiukweli Hii ramani ya mtoa mada, ina makosa mengi mno, haijazingatia kabisa kanuni za ujenzi.

Kafanya jambo la busara sana kuilta jf, kabla ya kuzamisha pesa, kutoa nyumba kituko
 
Back
Top Bottom