Kule Ujerumani alipewa test ya kula tu akafeli! Alizoea chipsi dume za bongo kafika kapewa menu hata nusu hakumaliza wazungu wakaona kumchezesha mtu na njaa hata km ana kipaji ni dhambi na non professional akarudishwa temeke kwetu!
Pale ujeruman alikwenda kwa majaribio FC cologne na 1998 bado wachezaji weusi hawakuwa wengi.
Alifanya majaribio lakini walipendekeza arudi atafute ftness.
Sielewi nini kilitokea kwakua kipindi anarudi apa nyumbani kulikua na maandalizi ya Simba na Yanga na akaiwahi iyo mechi iliyo chezwa Mwanza.
Alifanikiwa kufunga goli moja katika ushindi wa Yanga wa 2- 0 dhidi ya Simba.
Goli la pili alifunga Bakari Malima ambaye licha ya kucheza vizuri siku iyo pia alifanikiwa ku mdhibiti vizuri Dua Saidi ambaye alikua akiwafunga Yanga karibia mechi mbili mfululizo.
Katika Mechi ile ya Mwanza Malima alipelekwa acheze beki wa pembeni pembeni kutoka nafasi ya beki wa kati aliyo izoea ili ahakikishe Dua Saidi aleti madhara maana alikua aki isumbua sana Yanga na kufanya mashabiki wakose raha timu izo ziki kutana.
Bahati mbaya Dua Said akumaliza mechi baada ya kugongana na Bakari Malima wakati mechi ikiwa inaendelea.
Dua alikimbizwa Bugando kwa matibabu na alizinduka kutoka kwenye kupoteza fahamu usiku wa manane.
Kwasasa jamaa ni marafiki sana Kati ya Dua na Malima.
Lunyamila kwasasa naona anafanya shughulizake pale Airport kule Cargo marakwa mara uwa namuona kule.