Edibily Lunyamila - Moja ya wachezaji bora Nchi iliwahi Pata. Yupo wapi?

Atakuwa anajuta sana kuzaliwa mapema kwa sasa angekuwa na utajiri mzuri tu

mbona sunday manara kacheza zamani ila alifika mbali?

mbona nonda shaaban kacheza zamani ila alifika mbali?


ukweli ni kwamba Lunyamila alikuwa mchezaji wa show off, kwa jila lingine chenga twawala ila hakuwa mtu wa direct football kama Samatta ama Nonda shaaban.

ndio maana hakuifikisha yanga wala simba hata robo fainali tu ya caf champions league
 
Unaambiwa wakati Nonda Shaban yupo Ligi Kuu ya Ufaransa alihojiwa na Mtangazaji Mtanzania, Nonda alimuuliza Mtangazaji huyo kuwa Lunyamila yuko wapi kipindi hicho? Mtangazaji akamjibu amestaafu kucheza mpira. Nonda alishangaa sana, akamwambia Mtangazaji kuwa alipokuwa anacheza Yanga alitamani sana afikie kiwango alichokuwa nacho Lunyamila.
 
"mpira una level ni kama ilivyo utajiri, Kuna tajiri wa mkoa, taifa na dunia" 🤝
 
Akisimulia zuberi mkalaboko pale abood fm miaka ya 2020
UZee huu hapa
 
Mariga hakufika final na Intermilan ?
 
Hiyo mipira ya miaka hiyo ilikuwa ya wazawa watupu mnajilinganisha tiimu zenu wenyewe hlf mnajisifia. mkienda kimataifa mnakula chuma 3 bila mnarudi nyumbani mnaanza kubishana mambo ya simba na yanga sijui lunyalunya upuuzi mtupu. haya mambo ya kuendekeza uzawa mabaya sana. km alitisha alicheza wapi uko nje?
 
Jembe Ulaya ni Lunyamila
Likud ulikua wapi Lunya akicheza mpira ukiona mtu anamkumbuka James Tungaraza,Godwin Aswile (Mrimba) au Twaha Hamidu na Nyigu mchezaji wa Simba chochote atakachoongea kuhusu kabumbu wewe piga makofi tu pana mtu alikua anaitwa Jumanne Bubu kutoka Tabora kitasa ya Yanga.
 
Ramadhan imetamatika, Bakar Malima, jembe ulaya.
Huyo Lunyamila alikuwa Jembe ulaya akiwa timu gani?
Na maana ya Jembe Ulaya alipewa kama Trekta yaani anazoa kila kilicho mbele yake huyu ndugu yangu Likud anataka atubishie ambao tumeuishi mpira wa zamani..
 
Kipindi kile vilabu vingi barani Afrika vilikuwa kiboko sio kama hivi vilabu vya sasa na ndio maana hata unaona hivi vilabu vya Tanzania eti vinatamba leo na hawa wachezaji wa kuokoteza.

Tofauti na zamani ambapo wachezaji wazuri wa kiafrika walikuwa wakibaki hapa hapa na kuchezea vilabu vya hapa lakini leo hii wachezaji wabovu tu ndio wanabaki kuchezea vilabu vya Afrika huku wazuri wakipaa zao Ulaya.
 
Alihojiwa na BBC swahili wakati Monaco imetoka kucheza Fainali ya Champions League ndo akasema hivyo, inasikitisha sana wachezaji wetu aaliokua na uwezo kupotea kwenye ramani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…