Ni maneno ambayo nayakumbuka katika mafundisho yangu ya dini, "njoo kwangu, japo dhambi zako niwe nyekundu kama damu, zitasafishwa ziwe nyeupe kama theruji"
Naona vyama vya siasa vimeliona hilo na kulifanyia kazi barabara - Lowasa akiwa CCM alikashifiwa na kusemwa kwa kila baya na wapinzani, hasa Chadema. Alipohamia Chadema dhambi zake nyekundu kama damu zikasafishwa kuwa nyeupe kama theruruji. Ila sasa kule CCM alikoondoka ikawa tatizo, weupe wa matendo yake kama theruji ukawa dhambi nyekundu kama damu - kwa kuwa tu kahamia Chadema. Kuna wakati hata akaambiwa anaropoka!
Sasa Lowasa karudi tena CCM, na ghafla dhambi zake nyekundu kama damu zimekuwa nyeupe kama theruji! Tunasubiri kusikia Chadema waanze kutueleza dhambi za LOwasa zilivyo nyekundu kama damu
Sasa kwa sisi wenye akili tusio na vyama vya siasa yote haya yanatuambia nini? Yanatuambia jambo moja la msingi - wanasiasa wote ni wanafiki tu hawana lolote la ukweli ndani yao. Sisi tuendelee na maisha yetu na kutunza familia zetu. Usikubali kugilibiwa na wanasiasa. Watakulisha upepo tu. Usikubali wanasiasa wakugombanishe na ngugu jamaa na rafiki zako.