Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Na wafanyakazi wa serikali Lowassa ndie alikuwa anawapa mishahara? Maana hadi Leo hawajawahi kuongezewa mishahara tangu Lowassa asepe


Yaan umeniwahi haswa................ na huyo huyo Lowasa ndio aliyekuwa akitoa mafao ya wastaafu maana nao hali yao tete kabisa hali si hali na huyo huyo Lowasa ndio aliyekuwa anapandisha madaraja ya Serikali. Next time utulie ndio uanzishe thiredi hapa maana unadhani kuanzia thread ni rahisi
 

Sasa si ndio maana ya maoni; sikuwa nafanya academic research; lakini ndani yake utaona madai yangu ya objectivity.
 
Yaani, hadi sasa kweli kabisa huoni jinsi gani CHADEMA iliathirika? au hutaki kuona?
 
MWEMBESI ONE Hoja yangu ni rahisi sana. Kuna baadhi ya wana-CHADEMA tena wengine ni viongozi wa ngazi ya Kamati Kuu waliwaaminisha watanzania kwamba Lowassa ndiyo alama ya ufisadi na ndiyo ufisadi wenyewe...

Of course. Japo mimi si mwana-CDM, lakini nimeegemea upande wa upinzani. Nilikwazika kuona CDM wanampokea Lowasa na kumfanya mgombea wao wa uraisi. Nilikwazika zaidi kumuona Slaa akjiengua. Hilo lilikuwa kosa lliliofanywa na viongozi wa CDM, labda na washirika wao katika UKAWA.
Pamoja na kukwazika huko, bado nilichagua upinzani kwa sababu naona ccm kama chama kimechoka kupindukia; na kinaumwa kifafa
 

Very good counter attack arguments....

Hata hivyo, alichokiandika MwanaKijiji hakiwezi kuwa ni "facts" bali yatabaki kuwa ni "maoni" yake tu....

Hii ni kwa sababu na kama ulivyosema, inategemea sana unayatazama mambo haya katika engo gani kwa kuzingatia siasa zetu za Kiafrika na hususani za Bongo yetu hii....

Na kwa mtazamo wangu, issue ya Mbowe kujiuzulu eti tu kwa kuwa alifanya kosa hili la kumpokea EL kwa mazingira na siasa zetu hizi za Kibongo, binafsi sikubaliani nalo 100%....

Bado naona kabisa kuwa, kwa mazingira tuliyo nayo ingalau kwa kipindi hiki, Freeman Aikael Mbowe ndiye Mwenyekiti anayestahili kuendelea kuongoza harakati za mapambano hayo kwa CHADEMA....

Nakuhakikishia kuwa, likifanyika kosa la Mbowe kutangaza kuwa anaachia ngazi kwa sababu hii iliyotajwa na Mzee MwanaKijiji, ndiyo itakuwa mwisho wa CHADEMA na hakuna jambo muhimu lenye kuashiria kuua rasmi upinzani kabla 2020 wanalosubiri CCM kwa hamu kutokea upesi na kwa haraka isipokuwa mambo matatu haya yafuatayo:

1. Tundu Lissu kupotezwa kabisa ktk siasa za Tanzania aidha iwe kwa KIFO rasmi cha roho na mwili na cha aina yoyote ile ama asije kabisa Tanzania awe mkimbizi wa kisiasa huko huko aliko...

2. Freeman Aikael Mbowe haendelei kuwa M/kiti na Mbunge wa CHADEMA iwe kwa mbinu yoyote ama hata kwa KIFO cha mwili cha kawaida ama hata kisicho cha kawaida.....!!

3. Maalim Seif Sharrif Hamad na CUF ya Zanzibar wanapotezwa kisiasa kabisa iwe kwa KIFO cha kawaida ama hata kwa njia zozote zile. Rejea marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa juzi kati. Lengo ni hili hili.......

• Si ajabu maandiko haya ya kina Mzee Mwanakijiji yaliyoandikwa kwa mpangilio wa dizaini ya "Kimalaika wa nuru" kumbe ndani yake ni " utekelezaji wa kiapo cha ushetani na mkakati wa kufuta upinzani kabla ya 2020" mtupu.....

Soma tu ndani between lines utaligundua hili mara moja na utadhani kuwa ni full chembechembe za "nia njema", kumbe it's part of the strategic plans to lead the opposition to the road heading to hell before 2020 general Election...!!

Kama wanabisha, wanaopewa ushauri huu wenye "nia njema", wajaribu kuutekeleza waone impact yake....

In my opinion, acha Lowassa aende zake. Na nakubaliana kabisa na Mh. Freeman Mbowe, kuwa haya maisha yawe ktk nyanja ya kisiasa ama dini nk hayako "constant" kwamba ikiwa hivi basi inakuwa vilevile.....

It's like a Train Safari to Kigoma whereby on the way there will be get off and get in passengers....!!

Wanaoshuka hawawezi kuzuia Gari Moshi kuendelea na safari hadi mwisho wa Reli Kigoma....


Na haiwezekani kumshusha abiria kwa nguvu njiani mahali ambapo siyo Kituo chake cha kushukia....

Kumlazimisha Mbowe ajiuzuru kwa sbb ya EL, ni kumlazimisha abiria mwenye tiketi ya hadi mwisho wa safari - KIGOMA achukie Tabora junction na kumhadaa kuwa hapa ndo Kigoma .....!!
 

Ulikubali kucompromise principles zako ili tu upinzani uende Ikulu. Kwamba, haikujalisha yote uliyosimamia kabla na kiu yako ya mabadiliko ikakufanya ufumbe macho usione kilichokuwa nikitoka mbele yako. My friend haukuwa peke yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…