Hii ni baadhi ya maandiko yangu ya zamani
Niliwahi kuandika humu siku moja kuwa Lowassa wala wapambe wake wasitegemee fursa yoyote tena ndani ya Chadema baada ya uchaguzi mkuu 2015.
Katika hali ya kawaida kibinadamu haiwezekani Mgombea wa nafasi ya urais kama alivyo Lowassa umfungie kwenye kitanzi cha Ujumbe wa Kamati Kuu tu hali ya kuwa ana ndoto za kushiriki tena uchaguzi wa 2020.
Nilikuwa namwambia mtu mmoja Lowassa hawezi kudumu Chadema chini ya uongozi wa Mbowe huyu anayeota urais 2020 na ambaye ameshapanga safu yake makao makuu ya Chama na kwasasa yuko busy kujenga mtandao wa ushindi ndani ya Chama.
Mathalani katika uchaguzi Mdogo wa marudio wa kata 43 uliofanyika mwezi uliopita. Lowassa alipangiwa kampeni Kata ya Murieti wakati Mbowe alipangiwa ziara ya mikutano ya kampeni kwenye Kata zote 43 ili ajitangaze. Isitoshe hakuna rafiki yoyote wa Lowassa akina Guninita, Mgeja, Mahanga n.k aliyepangiwa kufanya siasa kwenye kata yoyote. Kwa kifupi John Mrema (Mkurugenzi wa Itikadi, Mambo ya nje na Uenezi) na Reginald Munis (Mkuu wa Idara ya mambo ya Uchaguzi, Oganaizesheni na Wanachama ) wanayomaagizo ya kumdhibiti Lowassa na watu wake kuelekea 2020.
Katika mazingira kama hayo siku sio nyingi ndani ya mwaka huu utasikia nao wakirudi Nyumbani . Wataitwa wasaliti, wamenunuliwa n.k lakini ukweli ni kuwa hawathaminiwi na wanadhibitiwa.
Alichokifanya Lowassa leo kwa mtazamo wangu ni mwanzo wa siasa zake mpya kuelekea 2020 na safari yake ya matumaini.
Benson Mramba
Jan 09, 2018
Sent using
Jamii Forums mobile app