Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Amemkimbia kamanda Tundu Lissu. Tuseme ukweli jamani, Lissu na Lowasa ni nani angechaguliwa kupeperusha bendera ya CDM? Mzee mjanja anajua kusoma alama za nyakati.
TUNAENDA NA TUNDU LISSU
 
Wakati tulipoasi Chadema ile dakika mlipomuasi Dr Slaa sababu ya huyu jamaa tulitukanwa sana. Naomba niseme kwa nia njema na ya dhati kabisa. Tuombane radhi maisha yasogee otherwise hatuisaidii Tanzania. Zile hatua za 2015 yalikuwa makosa ya karne, kubalini tujipange upya wakuu. Hakuna haja ya kushupaza shingo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo mkuu utarudi CDM au bado utabaki katikat. ..
 
1551453623684.png
 
Wanasiasa wanatufanya sisi matahira kabisa.....amini amini usiamini wanaCCM wataanza kumpamba tena na wanaCHD watageuza kibao

Ujinga ujinga ujinga
 
Draft imebadilika sasa….Hii ina maana gani sasa? ina maana bado TISS wanaendesha siasa za Tanzania kwa ufanisi mkubwa, wakichanganya vitisho, fedha na ahadi kubwa kubwa kwa wanasiasa wetu, Na sasa ni clear fact kwamba kama unaikosoa serikali na haikuchukulii hatua kali (kukupoteza ama gun down) wewe bado si mpinzani. Nyalandu,zitto, alivyokuwa mtatiro ni mifano dhabiti. 2019 imeingia, sasa tutaona mengi sana lakini yasioshangaza. Mpaka pale wananchi wa kawaida tutakavyoamka na kufanya maamuzi yetu wenyewe nje ya Politican Games. computer games 😱🙄😳😡😛XXX. POLITICIANS GAME OVER
1551454230285.png
 
Dr. Slaa sasa upo tayari kufanya kazi na choo, wakati ule uliikimbia ukasema ilikiwa sebureni lakini harufu ikakutoa nduki, sasa imerejea chumbani kabisa...tunasubiri ufafanuzi wako
Mpaka sasa mnajifanya vipofu? Kuna tukio la kichama la Dr Slaa kuhamia CCM? Bado mnahangaika na spinning? Msipokubali hizi blunders na kutubu mtafikia status ya NCCR very soon. Ibadilini Chadema for good, acheni uongo uongo. Chadema inahitaji mabadiliko makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bavichaa haaaahaaaahaaa leo mmeachwa makalio waziii...alipohamia chadema wwnyew mlimpokea kwa mliyoyaita mafuriko leo imekuwa hana impact.. ..haaaahaa impact my foot.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni baadhi ya maandiko yangu ya zamani

Niliwahi kuandika humu siku moja kuwa Lowassa wala wapambe wake wasitegemee fursa yoyote tena ndani ya Chadema baada ya uchaguzi mkuu 2015.

Katika hali ya kawaida kibinadamu haiwezekani Mgombea wa nafasi ya urais kama alivyo Lowassa umfungie kwenye kitanzi cha Ujumbe wa Kamati Kuu tu hali ya kuwa ana ndoto za kushiriki tena uchaguzi wa 2020.

Nilikuwa namwambia mtu mmoja Lowassa hawezi kudumu Chadema chini ya uongozi wa Mbowe huyu anayeota urais 2020 na ambaye ameshapanga safu yake makao makuu ya Chama na kwasasa yuko busy kujenga mtandao wa ushindi ndani ya Chama.

Mathalani katika uchaguzi Mdogo wa marudio wa kata 43 uliofanyika mwezi uliopita. Lowassa alipangiwa kampeni Kata ya Murieti wakati Mbowe alipangiwa ziara ya mikutano ya kampeni kwenye Kata zote 43 ili ajitangaze. Isitoshe hakuna rafiki yoyote wa Lowassa akina Guninita, Mgeja, Mahanga n.k aliyepangiwa kufanya siasa kwenye kata yoyote. Kwa kifupi John Mrema (Mkurugenzi wa Itikadi, Mambo ya nje na Uenezi) na Reginald Munis (Mkuu wa Idara ya mambo ya Uchaguzi, Oganaizesheni na Wanachama ) wanayomaagizo ya kumdhibiti Lowassa na watu wake kuelekea 2020.

Katika mazingira kama hayo siku sio nyingi ndani ya mwaka huu utasikia nao wakirudi Nyumbani . Wataitwa wasaliti, wamenunuliwa n.k lakini ukweli ni kuwa hawathaminiwi na wanadhibitiwa.

Alichokifanya Lowassa leo kwa mtazamo wangu ni mwanzo wa siasa zake mpya kuelekea 2020 na safari yake ya matumaini.

Benson Mramba
Jan 09, 2018

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa heri Ruge, karibu Tena Mzee Ngoyai

Kata mti panda mti


Lowassa 'ali rejea' CCM Siku Rais alipokunywa chai Na Rostam Azizi Leo ilikuwa Ni kutangaza kurudi
 
Mzee kakumbuka Pensheni yake , Upinzani Tanzania ni mgumu sana !!

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom