Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Hapana. Huwezi kuwa na moyo mgumu kiasi hicho.

Huwezi kuona mkakati na maana ya tendo hilo kwa wakati huo na kuweka 'exception'?

Mkuu Lowassa hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya cdm sio wakati huo, au wakati huu na hatokaa awe na msaada wowote.
 
Hao wote uliowataja hapo ni wakristo wa kuzaliwa ndani ya ukristo ilo sina shaka nalo
Lakini kuhusu kuhama chama kutoka chama A kwenda chama B
Katika sihasa ilo sio la kulisemea humu kwa mapovu kabisaaa
Kwanza tambua hao jamaa awajazaliwa chadema
Wameshahama vyama kibao huko nyuma labda wewe kwa ushamba wako au udogo wako unawaona kama vile wamezaliwa hapo chadema
Wanasiasa wana mambo mengi sana ikiwemo maslahi,falsafa,itikadi na misimamo ikitokea kugongana hama mawazo alafu suluhu hakuna mtu anaondoka mchana kweupe na wewe anakuacha mdomo wazi
Ukipenda sana watu kupitiliza utakuja kufa kama mwenzako kwa presha ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee aliona hapati yale mahaba aliyokuwa anaoneshwa mwanzo yamehamia kwa Lisu ameona bora achomoke.
 
Mh Lowassa amerudi nyumbani.full stop.
MAENDELEO HAYANA CHAMA

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Mkuu Lowassa hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya cdm sio wakati huo, au wakati huu na hatokaa awe na msaada wowote.
Chochote kinachoweza kuwaondoa CCM ni msaada, hata kama sio malaika.

Kwa wakati huo, dalili zilionyesha kulikuwepo na matumaini ya Lowassa kusaidia kuwaondoa CCM. Na kwa maoni yangu uwezekano huo ulikuwepo sana, lakini kampeni alizofanya (muonekano wa kuwa kama mgonjwa), hazikusaidia.

Angekuwa ni Lowassa mwenye uhai kama yule wa mwanzoni mwa utawala wa Kikwete kabla ya Richmond, CCM ingeondoka hata kama wangelazimisha kuiba kura.

Na hapa siwezi kamwe kukubishia kuhusu lebo ya "Fisadi" anayobeba ambayo ilimnata barabara; hasa wakati wa Richmond, ambayo kihalisi haikuwa yake, ilikuwa ya Kikwete!

Simtakasi kwa lolote, kwa sababu najua hili ni kundi la wapigaji wakubwa, na kuwa kwake ndani ya CHADEMA kusingewaongezea au kuwapunguzia CHADEMA nao kuwa na mwelekeo huo.

Sasa hapa sijui kama utanielewa ninachokieleza hapa, lakini basi ngoja nimalizie hivyo.
Tumefikia hatua Tanzania , bora ya kumweka yeyote madarakani badala ya CCM, hata kama hatujui huyo anayeingia atafanya nini.
 
Tundu Lissu ndo mtu pekee mwenye msimamo dhabiti Lema baada ya kutoka jela ameufyata Lissu pekee ndo Nina Imani nae
 
Chochote kinachoweza kuwaondoa CCM ni msaada, hata kama sio malaika.

Kwa wakati huo, dalili zilionyesha kulikuwepo na matumaini ya Lowassa kusaidia kuwaondoa CCM. Na kwa maoni yangu uwezekano huo ulikuwepo sana, lakini kampeni alizofanya (muonekano wa kuwa kama mgonjwa), hazikusaidia.

Angekuwa ni Lowassa mwenye uhai kama yule wa mwanzoni mwa utawala wa Kikwete kabla ya Richmond, CCM ingeondoka hata kama wangelazimisha kuiba kura.

Na hapa siwezi kamwe kukubishia kuhusu lebo ya "Fisadi" anayobeba ambayo ilimnata barabara; hasa wakati wa Richmond, ambayo kihalisi haikuwa yake, ilikuwa ya Kikwete!

Simtakasi kwa lolote, kwa sababu najua hili ni kundi la wapigaji wakubwa, na kuwa kwake ndani ya CHADEMA kusingewaongezea au kuwapunguzia CHADEMA nao kuwa na mwelekeo huo.

Sasa hapa sijui kama utanielewa ninachokieleza hapa, lakini basi ngoja nimalizie hivyo.
Tumefikia hatua Tanzania , bora ya kumweka yeyote madarakani badala ya CCM, hata kama hatujui huyo anayeingia atafanya nini.

Nimependa mchango wako maana una hoja za msingi hata kama sizikubali. Sasa tuje kwenye mtazamo wangu kuhusu huyo Lowassa. Hivi Lowassa anakubalika kwa nyota au uliwahi kumuona akihutubia ukasikia falsafa zake? Lowassa nimjuaye mimi ni mtu ambaye sifa zake zinahubiriwa na wapambe na sio yeye. Hata cdm walimchukua kwa sifa za kusikia sio kwa uwezo halisi waliojiridhisha nao. Kikubwa ambacho sina shaka nacho, uwezo wake wa kipesa ambao vyanzo vyake havifahamiki ndio vilivyompa sifa zinazohubiriwa lakini sio uwezo wa kisiasa wa dhahiri.

Viongozi wa cdm nitaendelea kuwalaumu na hata kuwadharau kwakuwa cdm hizo kura milioni sita wangezipata hata kama wangenisimamisha mimi kwani ilikuwa inakubalika. Baada ya uchaguzi wa 2010-2015, cdm walianzisha operation mbalimbali nchi nzima za kupata wanachama na kupandisha hamasa kwa wananchi, na wao ndio chama kilichofanya mikutano mingi au wajibu wa chama cha siasa kuliko vyama vyote. Hata hamasa ya watu kujiandikisha na kitambulisho cha kura kuitwa kichinjio ni kwakuwa watu walijua Lowassa ndio atakuwa mgombea wa ccm ili wamchinje. Viongozi wa cdm bila kujali ukweli huu wakaingia tamaa ya pesa na kumchukua mtu ambaye hakuwa na uwezo halisi zaidi ya sifa za propaganda pekee. Hata huko ccm ambako Lowassa alikuwa anaonekana tishio ni lini ulimuona akikijenga zaidi ya kugawa pesa chafu chini ya meza na watu kumsifia? Ni lini toka Aachie uwaziri mkuu uliwahi kumuona akiongea hata dakika 10 ukavutiwa na speech yake?

Hata kama ni kutaka kuitoa ccm na kushirikiana na shetani ndio hiyo kumsimamisha mtu anaongea dakika chini ya 3 kwa kusema kipaombele changu ni "Elimu, elimu, elimu, au Lowassa mabadiliko, mabadiliko Lowassa" Mkuu hata uandike kitabu kuhusu Lowassa, nitafurahia uandishi wako lakini sio msaada wa Lowassa ndani ya cdm. Mbowe na genge lake wanapaswa kutuomba radhi watu tuliopigania mageuzi ya kweli na kisha kutuletea mtu aliyetaka urais badala ya mabadiliko.
 
Back
Top Bottom