Nimependa mchango wako maana una hoja za msingi hata kama sizikubali. Sasa tuje kwenye mtazamo wangu kuhusu huyo Lowassa. Hivi Lowassa anakubalika kwa nyota au uliwahi kumuona akihutubia ukasikia falsafa zake? Lowassa nimjuaye mimi ni mtu ambaye sifa zake zinahubiriwa na wapambe na sio yeye. Hata cdm walimchukua kwa sifa za kusikia sio kwa uwezo halisi waliojiridhisha nao. Kikubwa ambacho sina shaka nacho, uwezo wake wa kipesa ambao vyanzo vyake havifahamiki ndio vilivyompa sifa zinazohubiriwa lakini sio uwezo wa kisiasa wa dhahiri.
Viongozi wa cdm nitaendelea kuwalaumu na hata kuwadharau kwakuwa cdm hizo kura milioni sita wangezipata hata kama wangenisimamisha mimi kwani ilikuwa inakubalika. Baada ya uchaguzi wa 2010-2015, cdm walianzisha operation mbalimbali nchi nzima za kupata wanachama na kupandisha hamasa kwa wananchi, na wao ndio chama kilichofanya mikutano mingi au wajibu wa chama cha siasa kuliko vyama vyote. Hata hamasa ya watu kujiandikisha na kitambulisho cha kura kuitwa kichinjio ni kwakuwa watu walijua Lowassa ndio atakuwa mgombea wa ccm ili wamchinje. Viongozi wa cdm bila kujali ukweli huu wakaingia tamaa ya pesa na kumchukua mtu ambaye hakuwa na uwezo halisi zaidi ya sifa za propaganda pekee. Hata huko ccm ambako Lowassa alikuwa anaonekana tishio ni lini ulimuona akikijenga zaidi ya kugawa pesa chafu chini ya meza na watu kumsifia? Ni lini toka Aachie uwaziri mkuu uliwahi kumuona akiongea hata dakika 10 ukavutiwa na speech yake?
Hata kama ni kutaka kuitoa ccm na kushirikiana na shetani ndio hiyo kumsimamisha mtu anaongea dakika chini ya 3 kwa kusema kipaombele changu ni "Elimu, elimu, elimu, au Lowassa mabadiliko, mabadiliko Lowassa" Mkuu hata uandike kitabu kuhusu Lowassa, nitafurahia uandishi wako lakini sio msaada wa Lowassa ndani ya cdm. Mbowe na genge lake wanapaswa kutuomba radhi watu tuliopigania mageuzi ya kweli na kisha kutuletea mtu aliyetaka urais badala ya mabadiliko.
Ngoja ni'quote' yote, kwa sababu naona tunakubaliana karibu kila sehemu, ila katika sehemu ndogo tu.
Tunaweza tukawa tunatofautiana katika haya yafuatayo:
1. Mimi naamini kwamba Lowassa angesimamishwa na CCM angeshinda uchaguzi ule. kwa asilimia kubwa kuliko aliyopata Magufuli. Nakubaliana nawe kwamba ushindi huo usingekuwa kwa sababu ya 'fikra' na uwezo alionao katika kuongoza kama ulivyoeleza hapo juu. Hili ninakubaliana nawe kabisa, na nashukuru umeliandika vizuri zaidi kuliko nilivyojaribu kulielezea mimi.
Na pengine utaniuliza, ushindi huo angeupata vipi. Bahati nzuri sana ni kuwa hili nalo umelielezea kwa ufasaha kabisa, "sifa za propaganda", na wapambe wanaomzunguka. Ni makundi yale yale waliyoyatengeneza na Kikwete ndio ilikuwa ngazi yao wote wawili, na sio uwezo wao katika kujenga hoja au kuweka mikakati.
2. Sikubaliani na wewe kwamba kuingia kwa Lowassa CHADEMA ndio sababu iliyowanyima ushindi; na kwamba hizo milioni sita zingepatikana bila ya kuwepo Lowassa.
Unasema kuwa kura nyingi zaidi ya hizo milioni sita zingepatikana kama Lowassa asingeingia CHADEMA; na ukatoa ushahidi wa 'kichinjio'. Sikubaliani na hili na huo ushahidi hauna nguvu katika kulinda hoja unayoiwasilisha.
Kama tunakubaliana kwamba kulikuwa na makundi ya 'propaganda' ya kuwezesha ushindi wa hawa watu, halafu tusikubaliane kwamba makundi hayo yasingewezesha kupata hizo kura milioni sita, hapa ni lazima tutafute nguzo nyingine ya kuegemea.
3. Ni kweli CHADEMA walipokea hela za Lowassa? Hili sina ushahidi nalo, lakini itanibidi niliweke kuwa moja ya eneo nisilokubaliana na wewe, na kuendelea kusimamia ile 'dhana' yangu kwamba CHADEMA iliwabidi wamtumie 'paka' mradi awaondolee 'panya' waTanzania, na mengine yafuate mbele ya safari
Kwa hiyo, katika kuhitimisha, ninakubaliana nawe kwamba Lowassa asingekuwa na tofauti yoyote na Kikwete katika utawala wake ndani ya CHADEMA; lakini angekuwa amesaidia kubadilisha siasa za Tanzania, na hasa hasa ndani ya CCM.