Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mzee kaondoka na ramani ya ufipa, lazima watafutane. Mtahangaika sana na mzee huwaga hajibu kitu atapiga kimya tu. Tuliwaambia mbn hata gwanda havai Mara ooh Mara ooh, sasa kiko wapi
Aisee

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Wazima jamani ,poleni kwa msiba wa mpendwa wetu na ndugu yetu ,na mtanzania wenzetu kaka Ruge M.
Niende moja kwa moja. Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu ,Daktari alihama chama sababu ya Mzee kuhamia CDM ,sasa nimekaa nimetafakari ,sasa je Daktari atakuwa tayari ku reverse kile alichosema na kuwasimanga CDM baada ya kumpokea mzee???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu hafifu Lowasa, Sumaye, Slaa, Lipumba, Zito ni wana usalama wakongwe wa Taifa la Tanzania ambao kazi yao kubwa kbs ni kuvivuruga vyama vya siasa visichukue dola kwa namna yoyote ile.
Kuja kwa Lowasa CHADEMA kuondoka kwa Slaa ni watu kazini kubadilishana vijiti ili kazi iende kama inavyotakiwa. Hizi ni mbinu tu za kuviparanganyisha vyama vya upinzani Nchini ili vikose nguvu ya pamoja.
Baada ya uchaguzi mkuu na matokeo kutangazwa watu walitaka kuingia barabarani wakijua kbs wameibiwa kura lakini Lowasa aliwaambia tulieni na wakatulia, hapo alikuwa anatekeleza majukumu yake nasio ya kichama.
Uwepo wa Lowasa na Sumaye ndani ya CHADEMA kulikidhoofisha sana chama kwa hoja zao kuwa chama kisifanye siasa za Kiharakati, hii yote ni mipango.
Inchi imetulia habari ya uchaguzi ishaisha chadema kimevunjwa vunjwa mikono na miguu kwa kunyimwa kufanya siasa hadi kipindi cha kampeni Wazee wanajirudisha kambini taratibu kupokea vyeti vya siri vya heshima.
Sisemi sana huenda akili yangu ni mbovu ila ukichunguza sana kesi ya mh Mbowe unaweza pata kuwa mahabusu au mfungwa mtarajiwa ni yeye mtu mmoja mwingine ni bosheni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee kaondoka na ramani ya ufipa, lazima watafutane. Mtahangaika sana na mzee huwaga hajibu kitu atapiga kimya tu. Tuliwaambia mbn hata gwanda havai Mara ooh Mara ooh, sasa kiko wapi
Weeee ufipa hakuna ramani
 
Hili swali hata mimi linanipa wakati mgumu sana.

Wanasiasa wote wanafik, wapo kwa maslahi yao binafsi na si maslahi ya wananchi kama tunavyojitahidi kuamini.

Watanzania, tusiuane na kujiumiza kwa kushawishiwa na viongozi wa siasa au eti kwa mapenzi ya chama. Hili ni fundisho kubwa sana.
Lowasa anafamilia yake.

Lowasa ana maisha yake binafsi kama wewe ulivyo na maisha yako nje ya hii ID ya FaizaFoxy.

Na sio Lowasa tu. Binadamu yeyote ana maisha binafsi kabla ya wengine.
 
Hii ni faida zaidi kwa upinzani kama wataamua kutulia nakujipanga vizuri.Kwasababu hali ya kisiasa ya huyo mzee lilikua robo tatu ccm na robo upinzani kwaiyo kuondoka kwake kutaifanya chadema kupumua zaidi nakujipanga na uko ccm mzee kaenda kuungana ile robo tatu yake aliyokua kaiacha nakwavile ile robo tatu yake iliyobaki ccm ilikua imepooza itafufuka sasa.Kwaiyo tutegemee ccm kua naushindani mkubwa sana wa ndani kwa ndani kwasababu kundi hili sioni kama ni kundi lakukaa kimya nakusubiri mwenyekiti apange nakuamua.ile robo aliyokua nayo mzee cdm ilishindwa kufurukuta kwasababu walikua ugenini kwaiyo kurudi kwa mzee ccm kunawapa nguvu zaidi yakufufuka.Ngoja tuone maana muda ni mwalim mzuri.Mim binafsi credit naitupa Upinzani.
 
Amefanya jambo la heri nakumbuka sana usemi wa mange kimambi ya kwamba

Lowassa ni zigo la mavi chadema toweni huu mzigo"si maneno yangu hayo ni kimambi on air

Lakini mbowe alikuwa mbishi kweli mpaka kimambi akawa anamtumia direct sms mpaka nakutaka kumtukana lakini mbowe alibeba tu huo mzigo aisee zile million 400 alizotia mfukoni ziko wapi leo mbowe mbowe eeeeeh haya ngoja tuone

Kingine nimemkubali sana lowassa maana amecheza ka messi vile yani wakati wa msiba wa boss ruge unatrend yeye ndiyo kang'atuka hahaha dah najikuta najicheka mwenyewe

Kingine alichokosea ni kwamba kawahi sana angesepa mwakani mwezi kama huu alafu tuone upinzani utakuwa na hali gani!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
mbowe
1. alikuwa anaona aibu kumfukuza kwa sababu kapiga pesa za lowass
2. alitaka lowass abaki cdm ili azidi kupiga pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamluki walioenda kule wengine wamerudi hii inaitwa MISSION ACCOMPLISHED waliobaki waua Upi zani tena 2020. Tetesi za mdada kuolewa pia zipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa atatusaidia kupambana na Lissu 2020.Ana uzoefu sana
 
Wimbo ulianza kwa chadema, hakuna kupinga. Kila pembe ilikuwa ni "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" alipokosa kuteuliwa kuwania urais wa tiketi CCM akajitoa CCM na kuhamia chadema, akapewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chadema, ghafla chorus ya "Lowassa fisadi, Lowassa fisadi" ikawa inaimbwa na wana CCM.

Sasa karudi CCM nani ataiimba chorus hiyo?

Siasa ni mchezo mbaya sana.

Ameenda kushiriki matamu ya vote 20!
 
Back
Top Bottom