Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mzee kaondoka na ramani ya ufipa, lazima watafutane. Mtahangaika sana na mzee huwaga hajibu kitu atapiga kimya tu. Tuliwaambia mbn hata gwanda havai Mara ooh Mara ooh, sasa kiko wapi
Aisee

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Wazima jamani ,poleni kwa msiba wa mpendwa wetu na ndugu yetu ,na mtanzania wenzetu kaka Ruge M.
Niende moja kwa moja. Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu ,Daktari alihama chama sababu ya Mzee kuhamia CDM ,sasa nimekaa nimetafakari ,sasa je Daktari atakuwa tayari ku reverse kile alichosema na kuwasimanga CDM baada ya kumpokea mzee???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu hafifu Lowasa, Sumaye, Slaa, Lipumba, Zito ni wana usalama wakongwe wa Taifa la Tanzania ambao kazi yao kubwa kbs ni kuvivuruga vyama vya siasa visichukue dola kwa namna yoyote ile.
Kuja kwa Lowasa CHADEMA kuondoka kwa Slaa ni watu kazini kubadilishana vijiti ili kazi iende kama inavyotakiwa. Hizi ni mbinu tu za kuviparanganyisha vyama vya upinzani Nchini ili vikose nguvu ya pamoja.
Baada ya uchaguzi mkuu na matokeo kutangazwa watu walitaka kuingia barabarani wakijua kbs wameibiwa kura lakini Lowasa aliwaambia tulieni na wakatulia, hapo alikuwa anatekeleza majukumu yake nasio ya kichama.
Uwepo wa Lowasa na Sumaye ndani ya CHADEMA kulikidhoofisha sana chama kwa hoja zao kuwa chama kisifanye siasa za Kiharakati, hii yote ni mipango.
Inchi imetulia habari ya uchaguzi ishaisha chadema kimevunjwa vunjwa mikono na miguu kwa kunyimwa kufanya siasa hadi kipindi cha kampeni Wazee wanajirudisha kambini taratibu kupokea vyeti vya siri vya heshima.
Sisemi sana huenda akili yangu ni mbovu ila ukichunguza sana kesi ya mh Mbowe unaweza pata kuwa mahabusu au mfungwa mtarajiwa ni yeye mtu mmoja mwingine ni bosheni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee kaondoka na ramani ya ufipa, lazima watafutane. Mtahangaika sana na mzee huwaga hajibu kitu atapiga kimya tu. Tuliwaambia mbn hata gwanda havai Mara ooh Mara ooh, sasa kiko wapi
Weeee ufipa hakuna ramani
 
Lowasa anafamilia yake.

Lowasa ana maisha yake binafsi kama wewe ulivyo na maisha yako nje ya hii ID ya FaizaFoxy.

Na sio Lowasa tu. Binadamu yeyote ana maisha binafsi kabla ya wengine.
 
Hii ni faida zaidi kwa upinzani kama wataamua kutulia nakujipanga vizuri.Kwasababu hali ya kisiasa ya huyo mzee lilikua robo tatu ccm na robo upinzani kwaiyo kuondoka kwake kutaifanya chadema kupumua zaidi nakujipanga na uko ccm mzee kaenda kuungana ile robo tatu yake aliyokua kaiacha nakwavile ile robo tatu yake iliyobaki ccm ilikua imepooza itafufuka sasa.Kwaiyo tutegemee ccm kua naushindani mkubwa sana wa ndani kwa ndani kwasababu kundi hili sioni kama ni kundi lakukaa kimya nakusubiri mwenyekiti apange nakuamua.ile robo aliyokua nayo mzee cdm ilishindwa kufurukuta kwasababu walikua ugenini kwaiyo kurudi kwa mzee ccm kunawapa nguvu zaidi yakufufuka.Ngoja tuone maana muda ni mwalim mzuri.Mim binafsi credit naitupa Upinzani.
 
mbowe
1. alikuwa anaona aibu kumfukuza kwa sababu kapiga pesa za lowass
2. alitaka lowass abaki cdm ili azidi kupiga pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamluki walioenda kule wengine wamerudi hii inaitwa MISSION ACCOMPLISHED waliobaki waua Upi zani tena 2020. Tetesi za mdada kuolewa pia zipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa atatusaidia kupambana na Lissu 2020.Ana uzoefu sana
 

Ameenda kushiriki matamu ya vote 20!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…