Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
Lowassa siyo Waziri Mkuu Mstaafu,sema ni Waziri Mkuu wa zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
daah niliemfata kanikimbia

dakta slaa alimkimbia kafatwa huko huko.

Sasa mimi na slaa tupo kwa njia panda.
 
Wana nd
tulikuwa tukifunga na kuomba fisadi kuu liondoke ajiunge na alikozaliwa. Mungu katujalia ameondoka kajiunga na RA kubwa lao. Sasa ni wakati wa kumweleza Sumaye na wengine waondoke na Freeman Mbowe muuza chama. Zitto arudi cdm aongeze nguvu upinzani. Lisu tayari kashapata njia nyeupe kumkabili JP. Mbowe umefanya mengi tunakushru sana kwa ili la lowasa kwa kweli ulituumiza sana. Hata Dr. SLAA ANAWEZA KURUDI SASA na John kapata raha kwani sera ya ufisadi inarudi Mrsa ni
 
Sky, mimi sioni tatizo kwa mzee Lowasa kurudi kwao. Kwa namna siasa zilivyo kwa sasa lazima huyu mzee angerudi . Huku Kenya walishazoea hali hii wanasaisa wa huku wanahama kila siku. Tatizo la huko nyumbani ni kuwa chuki zimezidi ndio maana mtu akihama watu wanashangaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana interest nyingi CCM, mategemeo ya kuwa mtawala yalimhakikishia usalama wa biashara zake. Kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa biashara zake haziko salama.
 
Mpangawangu umenena. Hakika Lowassa hajakurupuka kufikia uamuzi huu na hakutaka pia kuutumi uamuzi wake kuumiza upinzani. Nadhani tafsiri ya hili alilolifanya ni kustaafu siasa. Na bila shaka hii ni kazi aliyopewa Rostam Aziz alipokwenda Ikulu. Kama ilivyokuwa kwa Dr. Slaa sidhani kama atapata kejeli zozote kutoka cdm.
 
Back
Top Bottom