Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Lowassa atufunze sie Vijana tupende na tushike Itikadi ya Vyama sio Mtu, poleni wote mliohamaVyama vyenu kwa sababu ya Lowassa
 
Shukrani kubwa sana kwa mzee Lowasa.

Ulichotufanyia kama ukawa ni mambo makubwa sana, Umetuongezea wabunge na madiwani wa kutosha sana bila kusahau Halmashauri nyingi ambazo chadema au CUF wanaziongoza.

Nakutakia mafanikio mema uko uendako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
 
Nimependa hiyo aliposema, nanukuu, "amerudi nyumbani"...sikuwahi kumsikia akiita Chadema nyumbani. Nadhani kwa kauli hiyo na ile ya wana CCM waliomwimbia Kikwete kwamba wana imani na Lowassa akiwemo Waziri Mkuu Majaliwa, Guninita, Sophia Simba n.k. inajibu maswali kadhaa.
 
Reactions: SMU
USED FROM KINONDONI.
 
King maker RA ndani ya nyumba, kuna kitu kizito bila shaka kinaendelea woga umetanda lazima wahuni watafutwe wapambane na mhuni mwenzao maana hasomeki na inaonyesha kama anacheza karata zake vizuri hivi kupitia vijana wake.. Ngoja tuone mchezo sasa..
 
Safi sana. Huyu mzee alitunyima pumzi kwa hakika. Leo nakula maji hadi asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…