Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Watu wa Mungu habari zenu..

Tetesi za ndani za CDM ni maumivu makali baada ya Mh Lowassa kurudi nyumbani kumenoga..!! Yaani ni sawa kuvunjika kwa uti wa mgongo, haiwezi tena kujitutumua hata kidogo kisiasa..!! Poleeeeni..!

CCM haishindwi chochote huwa nasema hivi kila mara.. Sasa mmeona na kudhibitisha..! Chezea kitu kingine sio CCM..!! CHADEMA leo bado wako ktk maruweruwe hawajui nini kimetokea, hawaamini bado..!! Siasa mchezo mchafu sana..!! 😜😂😂
Hapana. Lowasa alipata support wakati wa uchaguzi tu. Baada ya hapo, he is a liability. Alikuwa anavumiliwa tu ndani ya chama. Na yeye anajua hivyo.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums
Bado Mbowe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali nalo jiuliza ni je wale walio Hama nae wakati akitoka ccm kwenda cdm nao wanarudi ccm au ?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]





siasa bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ilikua ni lowasa kuhamia cdm hii ya kurudi sio habari mbaya zaidi imeshindwa ku outweigh ishu ya Ruge,poor timing kwa wanamkakati wa kuunga mkono juhudi za rais
 
Mamvi ni asset.Uwezo. wake wa kujenga hoja ni zaidi ya Lissu
 
Hapana. Lowasa alipata support wakati wa uchaguzi tu. Baada ya hapo, he is a liability. Alikuwa anavumiliwa tu ndani ya chama. Na yeye anajua hivyo.


Nadhani Mh. JPM ameshtukia kuhusu possibility ya Lowassa kuungana na Membe upinzani ingekuwa hatariiiiiiii sana kwa CCM, hivyo akamuwahi kumrudisha home kw gharama yoyote ile..!!
 
Mbowe aliiua cdm hasilia ameua misingi ya chama kwa kumleta lowasa na alitoa fedha nyingi sasa chama kimekufa ata gerezani uko asitoke tena maana dhamira yetu wanacdm inatusuta,mbowe hajiuzulu kwa kushindwa kusimamia chama apo ndo naanza kumuelewa zitto,slaa yani hata bora lipumba sio mbowe ,damu za wana cdm waliokufa kukipigania hiki cham zitamtesa mbowe ,

@ mbowe out
MBOWE out
MBOWE out

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very well comrade lowassa. Niliwaonya chadema. Wakati wa uchaguzi.. lakin hawakusikia.
Mbowe aliuza gem.. na picha ilikuwa ikionekana waz kuwa kaja kufanya nn.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lowassa kwenda Chadema HAKUWA na agenda yoyote zaidi ya kutapatapa baada ya kuondolewa jina lake kwenye kinyang'anyiro cha CCM. Alikuwa anabahatisha bahati yake upinzani baada ya milango ya CCM kufungwa. Kwa sasa ameona umri umeenda na hakuna uwezekano wa kufanikiwa ndiyo maana anarudi CCM ambako nako hatakuwa active!
 
Watu wa Mungu habari zenu..

Tetesi za ndani za CDM ni maumivu makali baada ya Mh Lowassa kurudi nyumbani kumenoga..!! Yaani ni sawa kuvunjika kwa uti wa mgongo, haiwezi tena kujitutumua hata kidogo kisiasa..!! Poleeeeni..!

CCM haishindwi chochote huwa nasema hivi kila mara.. Sasa mmeona na kudhibitisha..! Chezea kitu kingine sio CCM..!! CHADEMA leo bado wako ktk maruweruwe hawajui nini kimetokea, hawaamini bado..!! Siasa mchezo mchafu sana..!! [emoji12][emoji23][emoji23]
Ushalipwa bk7? Waisha home basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom