Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Mzee kura yangu bwna inaniuma saana. [emoji51][emoji51][emoji51]
FB_IMG_1551461754491.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee alishapima upepo akaona 2020 ndani ya ukawa hataweza kupeperusha bendera ya urais, hizi zinaitwa hesabu za haraka haraka
 
Uyu mzee mnamwonea kwanza Mkwe wake anayemuoa binti yake alifungwa bila dhamana unafikiri uyu mzee anaelewekaje kwenye familia? Lakini pia kazi ilomleta CHADEMA imekwisha alikuja na watu kaondoka mwenyewe.
Ninalowaasa wapinzani chondechonde msimtukane acha ccm wale matapishi yao maana walimtukana vya kutosha.
Nadhani Mh. JPM ameshtukia kuhusu possibility ya Lowassa kuungana na Membe upinzani ingekuwa hatariiiiiiii sana kwa CCM, hivyo akamuwahi kumrudisha home kw gharama yoyote ile..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Kasoma Alama Za Nyakati Kaona Hana Exposure Tena Ikabidi Arudi Kujilia Zake Pensheni Zake Huko Alikotoka
 
Maalim kichwa ngumu, Juma duni MTU makini sana lkn nae kaingizwa cha kike
 
Hapana. Lowasa alipata support wakati wa uchaguzi tu. Baada ya hapo, he is a liability. Alikuwa anavumiliwa tu ndani ya chama. Na yeye anajua hivyo.
Hiyo inaitwa sizitaki mbichi hizi , afadhali Mh Lowassa umerudi CCM umeachana na lichama lisilo na shukrani na limejaa mitusi midomoni
 
Yule maza hawezi kukubali arudi kupigwa mabomu tena, sasa hivi ni mwendo wa vyuku tu....bandika bandua - Hayo maji ya washawasha nani anayataka tena!!
 
Wako wapi wale waliokuja wakimkebehi Dr.Slaa na wale want rais wa moyoni mwao chadema Keisha kazi hamuaminiki Tena endeleeni kujipendekeza kwa wazungu mtaingia ikulu

Taarifa mbaya sana kwa Dr slaa hizi sijui atahama ccm,ahamie Act alisema hawezi kaa chama kimoja na Lowasa
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k

Habari zaidi...

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.

Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.

Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.

Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.

Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.

Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.

Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.



View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums


Huyu mamvi nilimtetea sana hadi nikapigwa ngumi nikidhani syo mwizi, leo ndo nimeamini kuwa lowasa ni mwizi mkubwa na amerudi kuratibu wizi wa fedha na kura.
Is a bull shit.
 
Back
Top Bottom