MICHUTZ
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 271
- 531
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwani lipumba alimkataa lowassa at the first place?? au badaye?Niliisubiri hii Siku kwa hamu kuwaona kina maalim seifu na mbowe wakiumbuka. Lipumba roho ilimsuta aliona mbali. Hence proved prof ni prof tu
Nadhani Mh. JPM ameshtukia kuhusu possibility ya Lowassa kuungana na Membe upinzani ingekuwa hatariiiiiiii sana kwa CCM, hivyo akamuwahi kumrudisha home kw gharama yoyote ile..!!
Wewe mzima?Sasa Lowassa amerudi CCM, chama cha muajiri wako. Tunaomba tamko lako Mh. balozi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo inaitwa sizitaki mbichi hizi , afadhali Mh Lowassa umerudi CCM umeachana na lichama lisilo na shukrani na limejaa mitusi midomoniHapana. Lowasa alipata support wakati wa uchaguzi tu. Baada ya hapo, he is a liability. Alikuwa anavumiliwa tu ndani ya chama. Na yeye anajua hivyo.
Wako wapi wale waliokuja wakimkebehi Dr.Slaa na wale want rais wa moyoni mwao chadema Keisha kazi hamuaminiki Tena endeleeni kujipendekeza kwa wazungu mtaingia ikulu
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.
Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.
Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rais Magufuli, Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Humphrey Polepole n.k
Habari zaidi...
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, nchini Tanzania. Lowassa alikuwa mgombea wa kinyang’anyiro cha urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA katika Uchaguzi mkuu 2015.
Kurejea kwa Lowassa kulikuwa kukitabiriwa na baadhi ya watu, lakini mara kadhaa Lowassa alikanusha kuwa anampango wa kurudi katika chama hicho.
Vyanzo vya habari vinasema hatua hiyo imewashitua watu wengi, kwa sababu ya kile ambacho kilisababisha yeye kuhama chama hicho.
Lowassa baada ya kuitumikia CCM kwa kipindi kirefu alikihama chama cha hicho kufuatia mvutano uliotokea baada ya kutoidhinishwa na chama hicho kuwa mgombea wa urais.
Sherehe za mapokezi yake wakati akirejea rasmi Ijumaa zilifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyoko Lumumba Dar es Salaam na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho John Magufuli.
Lowassa mara kadhaa amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli, Ikulu ya Tanzania.
Kumekuwa na wimbi la wanachama wa upinzani kuingia CCM tangu Magufuli achaguliwe 2015, kitu ambacho kimekuwa kikizungumziwa katika duru za siasa kwamba kinadhoofisha upinzani.
View attachment 1035375
View attachment 1035459
View attachment 1035448
Unaweza soma pia:
Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums
Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums
Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums