Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.

Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.

Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.

Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.

Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,

Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?

Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.

Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.

Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.

Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.

Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.

Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.

Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.

Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .

Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.

Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.

Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.

Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.
 
Cheers Makamanda, Yeah guys today am happy....!!

Daaah we mzee ulijua kutununisha Makamanda, ulijua tuzip midomo na mikono kama wafungwa kwenye gereza letu wenyewe. Hakika tunakushukuru Mungu kwa kutuondolea mtu huyu kwa hiyari yake mwenyewe..!!

Uamuzi alioufanya mzee huyu unafaida kubwa kwa Chadema kuliko kwa ccm. Mzee ndani ya chama alikuwa mwenyewe na Mbowe tu. Kina Mnyika walikuwa wakimuangalia wanaishiwa morali ya kupaza sauti. Lissu ndo kabisaa... hataki hata kumsikia mzee huyu. Wapo viongozi wengi tu ambao walikuwapo Cdm kwa kusukumwa tu kwasababu kwa namna yoyote wasingeweza kwenda ccm. Sasa kuondoka mzee huyu kutawarudisha makamanda hawa kwenye mstari.

Hii inamaana gani.., Mzee ameondoka Mwenyekiti wake akiwa Mahabusu kwa Miezi mitatu..!! Mwanasheria mkuu wa chama ambacho yeye alikuwa mjumbe wa cc akiwa Ubelgiji akiuguza madonda ya kunusurika kuuwawa kwa risasi kedekede, Wabunge kadhaa wakiwa wametapakaa mahabusu mbalimbali kwa kesi hizi na zile.... What a selfish man I ever seen...!!

Ma Comrade Commenders all over the world tembeeni kifua mbele.. Now Cdm asili is back. Mbowe wewe ndiwe Mbowe na juu ya mwamba huu imejengwa na kusimikwa Cdm.. siyo siri ulituumiza makamanda wengi kwa kumpokea bwana huyu..!! Ila tusemeje sasa...

MAJUTO NI MJUKUU... TOKA JELA COMMANDER CDM IKO MLANGONI INAKUSUBIRI TUNAJUA KUWA HURUDII MAKOSA KAMA HAYA BALI UTAYAFANYA TOFALI LA KUJENGA NGUZO IMARA KWENYE GHOROFA HILI LA CHADEMA

Makamanda wote mliopo boda tuonane kesho Valentine tugonge vyombo kusindikizia furaha hii..!! Makamanda Dar semeni tuonane wapi Jumapili... Mimi mgeni wenu tafadhali..!!

BAAAAAAAACK TANGANYIKA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nani asiyejua yule ni Kada mtiifu wa CCM? Cheyo , Mrema wote wapo kwa kazi maalum.
 
Waliomdhihaki lowasa karudi kwao sijui itakuaje,hii ni taarifa mbaya kwa bashite,msukuma, kibajaji,lusinde,na maccm waliomdhihaki lowasa sijui wataangaliana usoni,vipi kuhusu Dr slaa nadhani itabidi aamie chauma au updp maana alimkimbia lowasa chadema akarudi ccm.
 
Una theory nzuri pia. Lakin kwangu mm nilimuona kama asset kwa ccm. Even if alidefect lakin bado ccm walikuwa na access nae.
Kwa upnde mwingine inaweza kuwa kweli ulichsema.. lakin mm naangalia kiundan zaid..

Sent using Jamii Forums mobile app
Mawasilino na CCM yalianza baada ya uchaguzi na yeye kugundua kuwa siasa za upinzani si lelemama hivyo akakata tamaa. Mtu aliyezoea kuwekwa viti vya mbele mbele na kusifiwa hawezi kuhimili shuruba za upinzani!
 
Ilikuwa ni swala la muda tu kabla hili halijatimia, ni wakat wa upinzani kunitafakari na kufukuza vibaraka wote nje ya chama. Waanze upya, Lissu na Zitto ni hazina kubwa iliyobakia upinzani zitumiwe vyema.
 
Makamanda au nyumbu kwa jina lingine,huwa hawawazi nje ya box hata utikise kama vichwa vyao.
Maneno ya kujifariji hayo, CCM imezaliwa lini ? Unafikiri jana ? CCM imezaliwa mwaka 1977 , usifikiri imezaliwa sawa na chadema , hata mtei muasisi wa chadema alikua CCM , kama ulikua hujui ndio hivo.
 
Niliisubiri hii Siku kwa hamu kuwaona kina maalim seifu na mbowe wakiumbuka. Lipumba roho ilimsuta aliona mbali. Hence proved prof ni prof tu
Roho ilimsuta kumkaribisha Lowassa kwenye vyombo vya habari kuwa ni jembe?

Prof uchwara kama yule aliyeshindwa hata kusimamia familia yake unampaje hadhi hiyo?

Lipumba anatumika na ccm muda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…