Baada ya kula na kushiba, ndipo usingizi ulipoanza kunishika. Kweli ni sawa kwa jinsi ambavyo waungwana wanasema "et, shibe ni mtoto wa malevya na njaa ni mtoto wa malegeza!" Kwa kweli inastaajabisha mno, katika kuamini jambo hili, hata hivyo nimeshiba kweli kweli. Nikiwa nimeamka tayari kwa kuelekea kitandani.... Mara anakuja Asia, ambaye ni dada yangu, huku akiniita "Billieeee!!! Bibi anakuita, Fanya haraka ujeee...". "Nakujaaa..." Nikamuitikia.
"Naam Bibi, nimekuja tayari." Nikamuitikia huku nikipapasa kutafuta mahala pa kuketi kwenye mkeka. "jamani wajukuu zangu, kwanza ninayofuraha kubwa kuwaiteni ninyi mahala hapa, kwani nimeona ni vema kuwaeleza jambo la msingi na lenye umuhimu mkubwa kwenu" alianza kuzungumza kwa kuanza na maneno hayo. Akaendelea huku akisema "kwa maneno machache sana, napenda niwashirikishe jambo lifuatalo: Ni kwamba... Ni jambo la hekima kubaki katika usalama wa watu walio salama, chini ya uangalizi wa Baba anayejali, anayependa na anayejua kutunza, badala ya kwenda kutafuta raha katika mahala pa mbali.... Na kwa wakati mmoja wafurahieni wale wote waliowarudia ninyi kwa hiari yao wenyewe kwa lengo la kutimiliza malengo ya pamoja yaliyo na tija kwenu ninyi na kwa wenzi wenu." Baada ya kusema maneno hayo machache sana, akainuka kisha akautaaga akisema "Chilo mwaka!" Kwa pamoja tukamjibu tukisema, "Chilo mwaka nagwe!" huku nasi tukielekea kwenda kulala kila mtu chumbani kwake. Kesho yake asubuhi ikawa ndio siku ambayo niliweza kufahamu maana ya maneno ya bibi, aliyotueleza usiku wa jana.
Karibu sana mzee Lowassa, CCM na Serikali ilikuhitaji na inakuhitaji kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa lengo la kuwahudumia watanzania.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!