Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Leo nitakesha kwenye bar kwa furaha ya Lowassa kuondoka cdm. Alaaniwe Mbowe na genge lake kupokea hela ya Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
Heeee kumbe kweli Mh aliuza chama kwa Lowasa?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Mbona hakuna anaye twambia kutoka Chadema Polepole kampa shilling ngapi??
 
Imenisikitisha sana, ila hili litakuwa somo kwa upinzani. Next time watakuwa waangalifu zaidi. Unawezaje kumchukua mtu wa kuja na moja kwa moja unampa uongozi!
 
Wale waliodeki barabara, wale walio lala chini malaika (former fisadi) apite wana hali gani huko sasa!?!?
Hahhahahahaaa siasa mchezo mzuri sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Roho ilimsuta kumkaribisha Lowassa kwenye vyombo vya habari kuwa ni jembe?

Prof uchwara kama yule aliyeshindwa hata kusimamia familia yake unampaje hadhi hiyo?

Lipumba anatumika na ccm muda wote

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kujiongopea, endelea kuzungusha mikono mpaka wote muishie ccm ndio tuone. Hao mnaowaita ccm in wapinzani mpaka a kesho na wale wanaowaita wenzao wamenunuliwa ndio wakwanza kuunga juhudi
 
Kila anaehamia ccm tulikuwa tunaambiwa amenunulia hata uzushi wa kuporomoka kwa uchumi tunaambiwa sababu ya kununua wapinzani,hata hesabu zilizokosekana kwenye vitabu vya CAG tunaambiwa zimetumika kununua wapinzani.
Hata yeye mwenyewe Lowassa aliwahi kusema mbunge wa monduli amekopeshwa mkopo wa mil 600 hapa ndipo pa kuelezwa Lowassa amenunuliwa kwa bei gani.
Mimi pasi na shaka naona amejiridhisha na kasi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano,ameona kule badala watu kujikita na kujenga chama imara,watu wamejikita kwenye uwana harakati usio na faida na kujitafutia kesi za lazima.
Uchaguzi mkuu 2020 upo karibu mgonjwa ameanza kujitangaza ,lakini chama kimeshindwa kumkemea Mgonjwa, asijitangaze mgombea uraisi ili hali mchakato bado na yeye mgombea wa 2015 yupo na bado anakubalika na wananchi walio wengi ameamua .Bora mtaji wake arudi nao ccm awaachie saccos yao na baada ya kutumia pesa zake nyingi 2015 mgonjwa amekosa busara na kujitangaza hadharani bila ya kushauriana na wenzake.
Poleni makamanda ndio siasa!
 
Kumbuka kauli ya Chakubanga pole pole kuhusu kuongeza dirisha la usajili hadi December kwa dhana kwamba fisadi lowassa alikuwa tayari kusajili. Bila ya shaka hakukubali bei aliyopewa hivyo negotiations ziliendelea hadi hivi karibuni na bei aliyoitaka dhalimu na dikteta kakubali kuilipa bila pingamizi lolote.

Lowasa ni mtu mzima sana hajarudi ccm bure bure kuna sababu muda utaongea .
 
Jakaya kikwete: Lowassa Karibu Nyumbani,,, Bashe apanick ajibu, Mariah Sarungi awachekaaa kwa kejeli

Baada ya jakaya kuandika ujumbe wa kumkaribisha Edward Lowasa CCM na kumsifu kwamba amechukua maamuzi ya busara,

Bashe amejibu chini kwamba Kikwete ndo alimbebesha mzigo na kumsingizia baadhi ya mambo,


 
Leo ndio nimeamini kuwa shida kubwa iliyoko ndani ya CCM ni wizi wa kimfumo.
Si ni huyu Lowasa aliye sababisha mpaka zika anzishwa mahakama za mafisadi ?
Na si ni huko huko CCM ndio walipo akina Tibaijuka wa Escrow, Change au jina jingine nyoka wa makengeza, William mwana Ngeleja , au mahakama ya mafisadi ilikuwa kwa Abinda Singh, na Rugemalira.
Ama kweli CCM sasa leo nimeamini kuwa mchawi anaye iroga Tanzania ili isipate maendeleo ni Chama cha mafisadi CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kabla ya kuja lowasa na sumayi chama kilikuwa hakipigi kazi mbona kilikuwa makini sana kwa hivyo kuondoka kwao Hakuna hasara yoyote ile .
 
Hii kesi kufutwa wakati wowote ule, sidhani hata kama wiki mbili zitafika, au wameshatolewa rumande kimya kimya na kesi kufutwa.
 
Lowasa,Magufuli na "upotevu" wa trillion zetu ndio CCM hiyo, chama cha MAFISADI PAPA
 
Jiwe katuaribia mchongo aise sisi makachero wa ccm tulikuwa tumepandikiza mzee hapo kwa lengo maalumu kuwa 2020 agombee huko chadema then dakika za mwisho (siku tatu kabla ya uchaguzi kufanyika) ajitoe na aseme kutokana na utendaji mahiri wa jiwe na mambo makubwa aliyoyafanya ameona ni bora asitishe kugombea na kumuunga mkono jiwe

Bt kamrudisha kundini mapema hili apate sifa katika kipindi hiki kigumu ambacho shilingi inazidi kuporomoka

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…