Kila anaehamia ccm tulikuwa tunaambiwa amenunulia hata uzushi wa kuporomoka kwa uchumi tunaambiwa sababu ya kununua wapinzani,hata hesabu zilizokosekana kwenye vitabu vya CAG tunaambiwa zimetumika kununua wapinzani.
Hata yeye mwenyewe Lowassa aliwahi kusema mbunge wa monduli amekopeshwa mkopo wa mil 600 hapa ndipo pa kuelezwa Lowassa amenunuliwa kwa bei gani.
Mimi pasi na shaka naona amejiridhisha na kasi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano,ameona kule badala watu kujikita na kujenga chama imara,watu wamejikita kwenye uwana harakati usio na faida na kujitafutia kesi za lazima.
Uchaguzi mkuu 2020 upo karibu mgonjwa ameanza kujitangaza ,lakini chama kimeshindwa kumkemea Mgonjwa, asijitangaze mgombea uraisi ili hali mchakato bado na yeye mgombea wa 2015 yupo na bado anakubalika na wananchi walio wengi ameamua .Bora mtaji wake arudi nao ccm awaachie saccos yao na baada ya kutumia pesa zake nyingi 2015 mgonjwa amekosa busara na kujitangaza hadharani bila ya kushauriana na wenzake.
Poleni makamanda ndio siasa!