Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

51674682_121807855560142_8471271059886238859_n.jpg
51674682_121807855560142_8471271059886238859_n.jpg
 
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza mda si mrefu Sumaye nae ataelekea CCM kutokana na mbinyo wanaokutana nao wanalazimika kurudi CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee kakumbuka Pensheni yake , Upinzani Tanzania ni mgumu sana !!

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Ni sawa,ni haki yake!

Hii inanifanya nizidi kupenda opposition!

Tunaopenda opposition ni watu fulani hivi very tough,tunavumilia magumu yote,tuna vitu fulani hivi vya kipekee unlike others.

Mambo kama haya yananifanya nizidi kujivunia opposition no matter what!

Yes bro.
I do agree....this is OPPOSITION BRAIN.......very tough brain, vey intelligent and unchallenged!!! Look at Tundu Lissu, look at Mbowe, look at Godbless Lema, look at Rev. Msigwa, look at Sugu, look at Halima Mdee, look at Ester Bulaya, look at Esther Matiko, look at John Heche, look at Zitto Kabwe and the like....it's a tough brain in another dimension...!!!

Ndiyo maana Jakaya Kiwete wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 alipokuwa Jimbo la Singida Mashariki aliwaambia wafuasi wa CCM wahakikishe Tundu Lissu harudi Bungeni maana huyo Tundu Lissu MMOJA ni sawa na WABUNGE KUMI wa CCM...Tough Brain!!!!!!.Siajabu waliamua kumpiga risasi ili kumnyamazisha.....lakini Mungu alikataa na ataendelea kukataa mpaka WAHUSIKA WATUBU DHAMBI HII.......muda bado utasema.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k



View attachment 1035375View attachment 1035381

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

FISADI KARUDI KUNDINI, sasa tunasubiri kina SLAA Na LIPUMBA wataendelea kushikamana na TEAM POLONIUM ama watachutama?
 
Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.

Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.

Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.

Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.

Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,

Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?

Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.

Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.

Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.

Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.

Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.

Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.

Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.

Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .

Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.

Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.

Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.

Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wamepoteza maisha Kwa sababu ya huyu Mzee, malipo ni hapahapa duniani

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
Chadema inamalizwa na wanachadema wenyewe!!! Angalieni hata comments zao baada ya tukio hili!!! Naomba muweke kumbukumbu hii, bila kutubu makosa ya 2015 na kuwajibika tusitarajie mabadiliko ya kisiasa. Chadema inaenda kuwa NCCR mpya, mark my word!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom