Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k



View attachment 1035375View attachment 1035381

Kwa kuwa amerejea alikotoka, hiyo ni haki yake kikatiba. Watakaopongeza watampongeza na watakaolaani watamlaanI
Waliomsafisha wataanza tena kumchafua na waliomchafua watamsafisha upya. Ndio siasa zetu zilivyo.
 
Yoyote anaye support CCM mie huwa nashangaa sana hivi hawaoni suffering of Tanzanian people?..very selfish people ...kuweka matumbo Yao mbele mxiewww

Becky

Ndio maana matukio kama haya yananifanya nizidi kujivunia opposition!

Watu wa opposition ni watu fulani very intelligent,righteous,tough na hatukatagi tamaa!

These are the virtues I'm ready to die for!

My heart goes to all men and women who left all the luxuries of this world CCM's government can offer and decided to die for the noble cause of democracy of this country through opposition!

These are the toughest people in Tanzania....I"m with 'em till the end!
 
Nadhani ameambiwa sharti la mkwewe kutoka sero basi arudi ccm!! Na fisadi imebidi achutame.
Sasa ni wakati wa Mbowe kuachia uenyekiti ili chadema iongozwe na vijana wasio mamluki ama sivyo aking’ang’ania kuongoza chadema itakufa!! Yeye ndio aliyekiuza chadema kwa Lowassa! Lazima Mbowe awajibike kwa hili.
 
Dr. Slaa sasa upo tayari kufanya kazi na choo, wakati ule uliikimbia ukasema ilikiwa sebureni lakini harufu ikakutoa nduki, sasa imerejea chumbani kabisa...tunasubiri ufafanuzi wako
Wanasiasa wanajuana wenyewe....hivi zile kauli za kina msukuma na nape hazikumbuki
 
Walaaaaa

Mzee hata hujui analysis yoyote about opposition...

Maalim na Lowassa hawana intersection wewe!

Lowassa amerudi humo,ile mamba haijafa,itamgeuza Jiwe kitoweo,subirini!
Hahaaa 2020 hiyooo! Anaenda kujikatia kipande chake alichokibakisha awali! Kumbuka alikuwa na ccm yake ndani ya ccm! Mchezo alioutumia wa kuondoka na sehemu ya jeshi na kwenda kuliunga na jeshi jipya ili kupata jeshi kubwa na imara inaweza kuendelea kumweka kwenye ramani ya siasa ila kuhusu madaraka asahau!! This time anaweza kuondoka na kijipande kidogo tu kutoka chadema ambacho hakitamsaidia kama kile alichokibandua kutoka ccm 2015!! Pia labda anaogopa kuwekwa jela nna umri wake ule!!
 
Wakati tulipoasi Chadema ile dakika mlipomuasi Dr Slaa sababu ya huyu jamaa tulitukanwa sana. Naomba niseme kwa nia njema na ya dhati kabisa. Tuombane radhi maisha yasogee otherwise hatuisaidii Tanzania. Zile hatua za 2015 yalikuwa makosa ya karne, kubalini tujipange upya wakuu. Hakuna haja ya kushupaza shingo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dr. Slaa na mamvi wote walikuwa kitu kimoja, ulikuwa ni mpango uliopangwa na ukapangika, Mamvi alikataliwa na wazee wa kitengo ila kikwazo kilibaki kwa wafuasi wake ndani ya ccm na namna ya kupoza machungu ya kukata jina lake ilibidi atafutwe mshenga ambae ni Much. Gwajima amfungishe ndoa kwa Chadema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom