Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Amerejea Rasmi CCM Leo.

Amepokelewa Lumumba Makao Makuu Madogo Ya Chama Cha Mapinduzi Na Katibu Mkuu Dr Bashiru Ally.

Aidha, katika mapokezi hayo walikuwepo Rostam Aziz, Mzee Phillip Mangula, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim n.k



View attachment 1035375View attachment 1035381

Unaweza soma pia:

Edward Lowassa na Frederick Sumaye mbioni kurejea CCM - JamiiForums

Edward Lowassa: Wanaodhani nitarudi CCM wanapiga porojo na kuota ndoto - JamiiForums

Lowassa hana namna zaidi ya kuipigia magoti CCM, Mkwewe Sioi Sumari mpaka sasa yupo lockup - JamiiForums

Nani kamsafisha lile dubwasha lake la RICHMOND?
 
Slaa sasa hivi ana njaa ya kufa mtu, itabidi avumilie tu

Sent from my Iphone using Tapatalk
 
naona kama vita ya 2015 bado mbichi....mzee kahisi tishio la jasusi kaona na yeye aunde kambi yake yenye nguvu...hiyo ndio siasa...sasa...kumbuka rostam na apson ni team lowassa na wameshafika kwa mzee....nadhani hapa kuna makubaliano...
Daaa! wanataka kumdhibiti Membe wa Mtama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowasa kaathiri sana siasa za Chadema haswa kuhusu ufisadi, ukumbuke hii miaka 3 CDM imemtetea sana Lowasa na Sumaye kuwa siyo Mafisadi ili hali CCM ilikuwa ikijinadi kuwa mafisadi wamekimbilia CDM,
Nasubiri kumwona Polepole na siasa zake kuhusu Lowasa

Sent using Jamii Forums mobile app
msimamo wa chadema kuhusu lowasa haujabadilika "KAMA FISADI MPEKEKENI MAHAKAMANI!
Poole pole anasemaje kwanza vp nae..
naona this is beyond your brain
 
Kwa heri Ruge, karibu Tena Mzee Ngoyai

Kata mti panda mti


Lowassa 'ali rejea' CCM Siku Rais alipokunywa chai Na Rostam Azizi Leo ilikuwa Ni kutangaza kurudi
hili nalo neno mkuu
 
Aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania ndugu Edward Lowasa amerejea tena katika chama chake cha ccm baada ya kuhamia chadema.

Makorokocho
 
Naona kajifunza kitu kwa Rostam,Rostam alitinga ikulu na kaka yake akafutiwa kesi ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha,akaachiwa!Hivi karibuni tutegemee Mkwe wa Lowassa kufutiwa kesi na DPP!
 
Hajui hata tarehe ya kufanya tukio.
Wiki hii ni wiki ya Ruge .angeisogeza mbele kidogo kupata headlines za kufunika dola.
Nadhani amefanya hili ili tukio lake lisibambe sana anajua jinsi raia watakavyo maindi
 
Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.

Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.

Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.

Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.

Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,

Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?

Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.

Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.

Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.

Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.

Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.

Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.

Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.

Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .

Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.

Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.

Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.

Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1551454946936.png
 
Back
Top Bottom