Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

CDM haiwezi kuendelea na viongozi Hawa hawa waliompokea na kumsifu Lowassa. Ili chama kiwe na heshima mbele ya Jamii, lazima viongozi waliopo watoke waingie wengine. Nazungumzia ngazi za juu. Mwenyekiti, Makamu wake, Katibu Mkuu nk
 
Najaribu kuwaza tu,huenda Lowassa kurejea CCM kuna uhusiano na mkwe wake kuwa lupango kwa kesi ya uhujumu uchumi!
Lowassa huenda kajifunza jambo toka kwa Rostam ambapo Rostam alipotinga tu ikulu tukaona maamuzi ya DPP kufuta mashtaka ya utakatishaji fedha na akabaki na mashitaka aliyoambiwa alipe faini!!!

Wenye kuona mbali,muda utaongea!
 
Nimestaajabu tu hapa mm ..sijui tumemkosea nn Mungu
Hakuna cha kumukosea mungu, hili ni moja ya matukio muhimu kwa wanachama na wapenzi wa siasa za upinzani kwanza kuwatafakari viongozi wao waliowaweka madarakani na pili kujitafakari na wao wenyewe Kama je hivi vyama vina viongozi sahihi? Je vina wapenzi na wanachama sahihi? Kwa sababu ukitaka kutafuta mahali palipokosewa, utabaini kuwa viongozi walikaribisha lakini pia wanachama na wapenzi wakashangiria sana kwa huo ukaribisho.
 
Hahhahahahahahaa, sasa wale kina jingalao waliokuwa wakisema Lowassa ni fisadi sijui watakuwa wameficha wapi sura zao. Bashite nae sijui atakimbilia wapi
 
Sasa nadhani rafiki yangu nayemuheshimu Dr Slaa atarudi CHADEMA,maana asiyempenda kaja.
Ndio shida ya kuhama au kuhamia chama kwa kwa kutizama mtu na sio imani katika misingi na itikadi. Dr Slaa atapata tabu sana katika hili....bila shaka na wengine wengi huku jamvini ambao ujio wa EL uliwafanya wa switch kwenda ccm....tusubiri waanze kula matapishi yao....both sides, of course!
 
Hata Mbowe nae ni suala la muda tu. Hasa kama atapokonywa uenyekiti nadhani baada ya masaa 72 atakuwa tayari ashapewa kadi ya CCM na uwaziri wa TAMISEMI kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhama kwa Mjumbe wa Kamati Mkuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa na kuamua kurejea CCM hivi kweli anamkimbia Tundu Lissu katika kinyang'anyiro cha Urais 2020?
IMG_20190301_184529_074.jpeg
IMG_20190301_180705_353.jpeg
 
Kwahiyo wewe una amini Lowassa alitoa hela kuingia CHADEMA?

Really?

Kiasi gani labda?
Dr slaa ndo alikua hot kwa kipindi kile ni kama sasa ilivyo kua juu tundu lisu,,,,,

ed low akapenyeza rupia,, eti mara akawa mgombea urais wa ukawa,,,,
Ukawa ikaanza kufa kuanzia hapo,,,,

Siasa uchwara,, propaganda uzushi na uwongo zikaanza,,,,
Alafu ndo kama kuna mtu alikufa au ali alijeruhiwa kwa ajili ya lowasa basi imekula kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom