Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Njia nyeupe kwa Lissu 2020 Mungu mbariki lowasa kwa kumuachia njia kamanda Lissu .
 
Wachambuzi wa mpira kina mwalim kashasha na wengine hua mechi ikishinda utasikia "Nililiona tangu mwanzo" Mechi ikifungwa utasikia "tangu mwanzo nilitegemea hivi" na mimi leo naomba kuwa Mwalimu kashasha Hakika hiki nilikitegemea maana Safu ya Ulinzi na mabeki hawakua na ushiriano kabisa.

Kwako.mwl kashasha
 
Hivi Mbowe kashapata dhamana au? Mi nasubiri kusikia Mbowe anajiunga CCM nione nani mbishi by nature
 
Wako wapi wale waliokuja wakimkebehi Dr.Slaa na wale want rais wa moyoni mwao chadema Keisha kazi hamuaminiki Tena endeleeni kujipendekeza kwa wazungu mtaingia ikulu
 
Uamuzi wa EL kurejea CCM haushangazi. EL hakuwahi kuwa na chembe ya mabadiliko ya kweli. Yeye alichokuwa anatafuta ni urais. Akina Mbowe na wenzake hilo walilifahamu vizuri sana. Kilichofanyika wakati huo - uchaguzi mkuu wa 2015 - ilikuwa mkakati wa siasa za uchaguzi ambapo maadui wawili waliungana ili kuona kama wangemwangamiza aliyekuwa adui wao wote. Na walipata kura za kutosha lakini urais wa Tz hautegemei mgombea kapata kura ngapi, unaamuliwa na politiburo ya CCM (inayojumuisha vitengo kadhaa ikiwa ni pamoja na NECcm). Pengine hilo ndo fundisho ambalo Mzee EL atakuwa amejifunza uzeeni. Karibu tena zizini mzee EL, sasa wewe sio fisadi tena! Tutakusanya majina yote uliyoitwa na CCM wenzako wakati uko uahamishoni tuyabandike hapa ili uyatunze kama trophy yako ya kisiasa.
 
Nitashituka siku nitakaposikia watu kama Lissu, Lema, Seif na wapinzani wengine ambao ni wapinzani wa kweli wamejiunga na CCM,hawa akina Lowassa ambao wanahama vyama kama wanyama wanaohama kwa kufuata msimu wanarudi nyumbani kwao.
 
1551455141431.png
 
Hiki ni kipindi cha kua na akiba ya maneno, wana chedama inabidi muonyeshe demokrasia mnayoipigania sio muda wa kumkashifu, kumbeza, kumtukana wala kumdhalilisha mzee wa watu.
kwa mazingira ya sasa kuunga mkono juhudi ni jambo la kawaida.

Maendeleo hayana chama
 
Back
Top Bottom