Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

naona kama vita ya 2015 bado mbichi....mzee kahisi tishio la jasusi kaona na yeye aunde kambi yake yenye nguvu...hiyo ndio siasa...sasa...kumbuka rostam na apson ni team lowassa na wameshafika kwa mzee....nadhani hapa kuna makubaliano...
Dah hawa jamaa kuna kitu kikubwa wanataka kutupiga tena,ameenda kuungana na Rostam,chenge,tubaijuka &Co. Ma mastermind sa hivi itakuwa kimyakimya na jiwe alivyo mkali kufunika tutalizwa...
 
Tusitegemee chadema mpya kutoka kwa viongozi hawa wa sasa ambao walikula matapishi yao. Tusijipe moyo kuwa sasa tunaenda kuwa na chadema imara wakayi hawa ndio viongozi wasio na msimamo.
Kiongozi pekee sasa hivi chadema ni John Mnyika, alionyesha wazi kwa boy language kuwa hakuunga mkonobkupokelewa kwa lowasa na alikuwa kama amekizilia chama.
Huyu ndiye apewe uenyekiti na apewe rungu kabisa kinyoosha watu.
 
Mpinzani pekee kwa Magufuli alikuwa Lowasa na sio Lissu wala Zitto wanaojibaraguza mitandaoni. Lowasa hayupo sana mitandaoni ila field yupo vizuri sana kuliko Lissu na Zitto.

2015, Lowasa alionyesha nguvu ya upinzani dhidi ya Ccm, mtanange ulikuwa mkubwa kweli na haikushabgaza yeye kupata kura nyingi ila wabunge na madiwani wachache kulinganisha na asilimia ya kura alizopata.

Lowasa kurudi Ccm ni pigo kubwa kwa upinzani haswa Chadema na neema kubwa kwa Ccm.

Kwa sasa upinzani una option chache mno, Lissu ambaye uwezo wa kuzunguka nchi nzima hatokuwa nao 2020 na hata akiwa nao bado watanzania hawajamuelewa.

Zitto, huyu ana umaarufu mkubwa sana mitandaoni ila field ukiondoa Kigoma mjini hana impact yoyote. Akisema asimame na Magufuli ni kipigo cha mbwa mwizi.

Mbowe?
Sumaye?

Ila kiuhalisia Lawama zote anastahili kuzibeba Mbowe kwa tamaa zake na kama ana busara lazima akampigie magoti Dr Slaa.

Njia ya Ikulu tayari imesafishwa na Lowasa Leo.View attachment 1035464

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajitahidi Sana !! Kazana
Hivi kama njia ni nyeupe kwanini tume ya uchaguzi isiwe huru ?!. Lowassa ameondoka (fine). Lakini upinzani umo mioyoni mwa WaTz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nchi hii hakuna upinzani kabisa kama lowasa ataitwa tena fisadi itabidi mbowe nae aunganishwe kwenye iyo list maana nae ilisemekana kakatiwa dili na fisadi lowasa akamsafisha kwamba sio fisadi
 
Wakuu Mimi niko nawaza tu kwamba itakuwaje mzee mbowe akipata taarifa za mzee lowassa kurudi ccm.

Mzee mbowe ndie alikuwa wa kwanza kumkaribisha mzee lowassa cdm tena kwa shangwe na vigere gere.

Sasa hivi mzee wetu mbowe yuko gerezani na sijajua kama huko gerezani huwa wanapewa nafasi ya angalau kusikiliza redio / kuangalia TV.

Sasa hapa nilipo namuhurumia sana mzee mbowe pindi atakapotoka gerezani na kukuta mgeni wake katoroka nyumbani bila hata ya kuaga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jihurumie mwenyewe, na mawazo yanayokusumbua wala hayawasumbui wale unaofikiria.
Kwani kuna lipi la ajabu Lowassa kurudi CCM. Pambaneni na hali yenu.
 
Niseme tu ukweli.nimeishiwa nguvu.
Ile kauli ccm itatawala milele.uenda ikawa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo ndio siasa.Watu walipoteza pesa,kazi , biashara nk mchezo wa ngumi roundi ya kwanza ilikuwa 2015 tukutane 2020 usichoke karibu kwenye ulingo wa ngumi za siasa round ya pili 2020 kati ya CCM na Upinzani Usivue gloves tukutane 2020 round ya pili
 
Mashabiki wa wanasiasa mnapata taabu sana
Sasa hivi upepo umegeuka wale waliokuwa wanamsema vibaya kazi kwao sasa kumsifia
 
Back
Top Bottom