Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

LOWASA KURUDI CCM
Lowasa kurudi ccm ni ushahidi kuwa ana uchu wa madaraka. Aliondoka ccm kwa kuwa hakupata fursa ya kugombea urais akiwa ccm na alipoona kuna uwezekano wa kugombea kupitia UKAWA, akafanya uamuzi wa kwenda ukawa ili apate fursa hiyo.
Lowassa alitarajia kuwa atapewa nafasi ya kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema lakini siku za karibuni upepo ndani ya Chadema umemgeukia Tundu Lissu kuwa ndiye kipenzi cha wengi kugombea urais wa Tanzania. Baada ya Lowassa kuona hakuna uwezekano wa yeye kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema ameamua kurudi ccm.
Sio kuwa Lowassa akiwa ccm ana uwezekano wa kugombea urais mwaka 2020 lakini kule ccm kuna maslahi na vyeo. Huenda pia Lowassa anawaza miaka saba ijayo wakati JPM anamaliza muda wake. Huenda akajaribu tena karata zake za kugombea urais kwa kupitia ccm
Kuhama kwa Lowassa ni pigo kwa upinzani kwa vile kuna baadhi ya wana Chadema walijiunga na Chadema kwa sababu ya Lowassa lakini pia inaweza kuwa fursa ya Chadema kujipanga upya. Shutuma kuwa Chadema wanapokea mafisadi sasa zitaondoka.
Ni fursa pia kwa chadema maana kama kuna weaknesses zo zote za kurekebisha basi Chadema wasisite. Kwa mfano wahahakikishe mchakato wao wa kuchagua mgombea urais uwe wa wazi kwa kutumia vigezo vinavyojulikana na kukubalika na uwe wa kidemokrasia.

SWISSME
 
  • Thanks
Reactions: BAK
<blockquote class="twitter-tweet" data-lang="en"><p lang="in" dir="ltr">Lowasa karudi CCM. Karibu tena nyumbani Mheshimiwa. CCM hoyeee! Magufuli hoyee,,,,,,,,</p>&mdash; Reginald Mengi (@regmengi) <a href="">March 1, 2019</a></blockquote>
<script async src="https://platform.twitter.com/widgets.js" charset="utf-8"></script>
 
Huyu propesa ni malaya wa kisiasa mwingine hana tofauti na mafisadi ndani ya ccm au fisadi lowassa na sumaye. Mtu alijiuzulu halafu anatumia nguvu ya dola kutaka kupora CUF!

Niliisubiri hii Siku kwa hamu kuwaona kina maalim seifu na mbowe wakiumbuka. Lipumba roho ilimsuta aliona mbali. Hence proved prof ni prof tu
 
Chademma sasa wakubali tu yaishe maana hakuna namna. Magufuli ni mwanasayansi, na anafanya mambo yake kisayansi na chadema wanamalizwa kisayansi. so
 
Tafakari tu kwa mapana.
Lowassa kaona (visualize) nini kwa haraka japo wachunguzi wa mambo walishaona akianza kurejea?

Nafahamu Lowassa ni mmoja wa mashabiki wa wa Ruge. Nilitarajia awe busy at least kwa siku mbili hizi kumuaga mpendwa huyu.

"Deads tells no tale" LISSU
 
Nyie mchukueni fisadi wenu muanze kumsafisha ,sasa kale ka form four failure ka msukuma sijui katakuwa kanamwangaliaje kwa jinsi kalivyomchafua .
 
LOWASA KURUDI CCM
Lowasa kurudi ccm ni ushahidi kuwa ana uchu wa madaraka. Aliondoka ccm kwa kuwa hakupata fursa ya kugombea urais akiwa ccm na alipoona kuna uwezekano wa kugombea kupitia UKAWA, akafanya uamuzi wa kwenda ukawa ili apate fursa hiyo.
Lowassa alitarajia kuwa atapewa nafasi ya kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema lakini siku za karibuni upepo ndani ya Chadema umemgeukia Tundu Lissu kuwa ndiye kipenzi cha wengi kugombea urais wa Tanzania. Baada ya Lowassa kuona hakuna uwezekano wa yeye kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema ameamua kurudi ccm.
Sio kuwa Lowassa akiwa ccm ana uwezekano wa kugombea urais mwaka 2020 lakini kule ccm kuna maslahi na vyeo. Huenda pia Lowassa anawaza miaka saba ijayo wakati JPM anamaliza muda wake. Huenda akajaribu tena karata zake za kugombea urais kwa kupitia ccm
Kuhama kwa Lowassa ni pigo kwa upinzani kwa vile kuna baadhi ya wana Chadema walijiunga na Chadema kwa sababu ya Lowassa lakini pia inaweza kuwa fursa ya Chadema kujipanga upya. Shutuma kuwa Chadema wanapokea mafisadi sasa zitaondoka.
Ni fursa pia kwa chadema maana kama kuna weaknesses zo zote za kurekebisha basi Chadema wasisite. Kwa mfano wahahakikishe mchakato wao wa kuchagua mgombea urais uwe wa wazi kwa kutumia vigezo vinavyojulikana na kukubalika na uwe wa kidemokrasia.

SWISSME
 
Lowassa kwenda Chadema HAKUWA na agenda yoyote zaidi ya kutapatapa baada ya kuondolewa jina lake kwenye kinyang'anyiro cha CCM. Alikuwa anabahatisha bahati yake upinzani baada ya milango ya CCM kufungwa. Kwa sasa ameona umri umeenda na hakuna uwezekano wa kufanikiwa ndiyo maana anarudi CCM ambako nako hatakuwa active!
Una theory nzuri pia. Lakin kwangu mm nilimuona kama asset kwa ccm. Even if alidefect lakin bado ccm walikuwa na access nae.
Kwa upnde mwingine inaweza kuwa kweli ulichsema.. lakin mm naangalia kiundan zaid..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
EL hawezi kuwa eti uti wa mgongoo...kha!!

Yeye ndiyo kabebwa na CDM tena awashukuru sana kumsaidia kipindi hicho ambacho alikuwa anaumwa ila CDM haikujali ikawa bega kwa bega na yeye.
 
Back
Top Bottom