Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Wazima jamani ,poleni kwa msiba wa mpendwa wetu na ndugu yetu ,na mtanzania wenzetu kaka Ruge M.
Niende moja kwa moja. Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu ,Daktari alihama chama sababu ya Mzee kuhamia CDM ,sasa nimekaa nimetafakari ,sasa je Daktari atakuwa tayari ku reverse kile alichosema na kuwasimanga CDM baada ya kumpokea mzee???

Sent using Jamii Forums mobile app

Akafanye nini chadema? While ccm ndio nyumbani kwake
 
Ni muda mzuri kwa upinzani kustaw sasa EL alikuwa akiwatesa sana na kuua vipaj kama wakina Mnyika sasa tutegemee kuona wakina Mnyika wale wa zamani hakika patakuwa patamu sasa.
 
Ilikuwa ni swala la muda tu kabla hili halijatimia, ni wakat wa upinzani kunitafakari na kufukuza vibaraka wote nje ya chama. Waanze upya, Lissu na Zitto ni hazina kubwa iliyobakia upinzani zitumiwe vyema.
You'll be shocked, Zitto? Endeleeni kuwaamini wanasiasa...
 
LOWASA KURUDI CCM
Lowasa kurudi ccm ni ushahidi kuwa ana uchu wa madaraka. Aliondoka ccm kwa kuwa hakupata fursa ya kugombea urais akiwa ccm na alipoona kuna uwezekano wa kugombea kupitia UKAWA, akafanya uamuzi wa kwenda ukawa ili apate fursa hiyo.
Lowassa alitarajia kuwa atapewa nafasi ya kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema lakini siku za karibuni upepo ndani ya Chadema umemgeukia Tundu Lissu kuwa ndiye kipenzi cha wengi kugombea urais wa Tanzania. Baada ya Lowassa kuona hakuna uwezekano wa yeye kugombea tena urais kwa tiketi ya Chadema ameamua kurudi ccm.
Sio kuwa Lowassa akiwa ccm ana uwezekano wa kugombea urais mwaka 2020 lakini kule ccm kuna maslahi na vyeo. Huenda pia Lowassa anawaza miaka saba ijayo wakati JPM anamaliza muda wake. Huenda akajaribu tena karata zake za kugombea urais kwa kupitia ccm
Kuhama kwa Lowassa ni pigo kwa upinzani kwa vile kuna baadhi ya wana Chadema walijiunga na Chadema kwa sababu ya Lowassa lakini pia inaweza kuwa fursa ya Chadema kujipanga upya. Shutuma kuwa Chadema wanapokea mafisadi sasa zitaondoka.
Ni fursa pia kwa chadema maana kama kuna weaknesses zo zote za kurekebisha basi Chadema wasisite. Kwa mfano wahahakikishe mchakato wao wa kuchagua mgombea urais uwe wa wazi kwa kutumia vigezo vinavyojulikana na kukubalika na uwe wa kidemokrasia.

SWISSME
Nidhani hakuna sababu ya huyu Jamaa kuongelewa sana. Itoshe fanyeni kama hakikutokea kitu chochote.
Tafuteni habari ingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana nd
tulikuwa tukifunga na kuomba fisadi kuu liondoke ajiunge na alikozaliwa. Mungu katujalia ameondoka kajiunga na RA kubwa lao. Sasa ni wakati wa kumweleza Sumaye na wengine waondoke na Freeman Mbowe muuza chama. Zitto arudi cdm aongeze nguvu upinzani. Lisu tayari kashapata njia nyeupe kumkabili JP. Mbowe umefanya mengi tunakushru sana kwa ili la lowasa kwa kweli ulituumiza sana. Hata Dr. SLAA ANAWEZA KURUDI SASA na John kapata raha kwani sera ya ufisadi inarudi Mrsa ni
Slaa hawezi kurudi kutokan na kiapo kikali na cha kikatili cha ubalozi, kuwa Balozi katika nchi yoyote ni sawa na kusaini mkataba wa kuzimu.
 
Sio vyema kumsema vibaya EL. Kwa wengi wenu ni Baba au Babu. Hivyo kusema lolote kinyume naye ni dhambi mbele za Mungu. Anajua yeye anachokifanya ila kwa kweli namhurumia. Kuliko nirudi ccm hiyo iliyonitukana hivyo, ningelijinyamazia tu ningojee mauti yangu.
 
Fisadi gamba laamua kurudi kwa magamba wenzie ili nalo likaibe tena maana mlango wa hazina uko wazi kabisa. Kwa wanasiasa Malaya/changudoa kama hawa wanaojali matumbo yao Watanzania tutayasubiri sana maendeleo ya kweli.
Kaona sasa kuiba haz8na ni rahisi zaidi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom