Mwenye ID ya Dr.Slaa tafadhali amtag,tumwite hapa tumuulize maswali
Tuliambiwa na CCM ya akina Nape,kwamba Lowassa,Rostam na Chenge ni wezi na mafisadi wakubwa,
Upinzani nao wakaukomalia wimbo wa ufisadi na ukawapa mafanikio makubwa!
Siku alipohamia Upinzani (mzee Lowassa),upepo wa matusi ulivuma zaidi kutoka CCM kwenda kwa mzee Lowassa,kwamba kutokana na usafi na umahiri wa Mh.Rais,Dr. JPM,katika kupambana na ufisadi,hakika Lowassa hawezi kukaa meza moja na Mh.(kwa sababu anachukia sana ufisadi na mafisadi).
Mimi niliwahi kufikiri kwamba wakati wowote baada ya kufunguliwa kwa ile mahakama yetu maalum,ya MAFISADI kutokana na kasi ya Mh.JPM katika swala zima la kupambana na UFISADI pamoja ana RUSHWA,nilitegemea kuona siku moja MAFISADI papa kama walivyokuwa wanashambuliwa na UPINZANI PAMOJA NA CCM kwa nyakati tofauti,wakiwa katika vyama tofauti,basi ilikuwa sawasawa kabisa kufunguliwa angalau mashtaka tu wajibu tuhuma zilizokuwa zimetapakaa kila mahali!
Tunaoweza kufikiria angalau kidogo,tunajiuliza maswali,je,kitendo cha Lowassa kurejea CCM,akiwa na rafiki yake,(ROSTAM)kitarahisisha kushughulikiwa kwa tuhuma zinazowakabili?
Je,Mh.Rais JPM,ameona bora aungane nao tu na kuwasamehe kwa makosa yao?
Je,Rugemarila,na Seth wataachiwa kwa mtirirko huu wa kusawazisha mambo?
Je,wazee wetu,kama Dr.Slaa wataamua sasa kuachana na siasa jumla jumla,kutokana na tabia mbaya za Upinzani na CCM kuwakumbatia watuhumiwa hawa?????
Wasalaam,"KARIBU SANA MZEE LOWASSA,TUSHIRIKIANE KUIJENGA NCHI!!"