Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Btw najua unaelewa vyema lakini unafanya spinning tu kwa wenye akili ndogo. Hivi unalinganisha kumpokea adui wa chama kwa miaka zaidi ya kumi akiitwa fisadi kuu na kumpa kijiti agombee urais na mgombea ubunge muadilifu kama Dr Slaa?
Naomba nikuulize swali moja tu, je unataka kusema Dr. Slaa hakuhusika kabisa katika ujio wa Lowassa Chadema?

MTAZAMO je, unakumbuka hii?

 
Huyu propesa ni malaya wa kisiasa mwingine hana tofauti na mafisadi ndani ya ccm au fisadi lowassa na sumaye. Mtu alijiuzulu halafu anatumia nguvu ya dola kutaka kupora CUF!


Malaya ni ww lakin lowasa kutusaidia kuthibitisha ukweli wa prof lipumba na dk slaa .
Lipumba ndio kazuia cuf kuuzwa
 
Mwenye ID ya Dr.Slaa tafadhali amtag,tumwite hapa tumuulize maswali
Tuliambiwa na CCM ya akina Nape,kwamba Lowassa,Rostam na Chenge ni wezi na mafisadi wakubwa,
Upinzani nao wakaukomalia wimbo wa ufisadi na ukawapa mafanikio makubwa!

Siku alipohamia Upinzani (mzee Lowassa),upepo wa matusi ulivuma zaidi kutoka CCM kwenda kwa mzee Lowassa,kwamba kutokana na usafi na umahiri wa Mh.Rais,Dr. JPM,katika kupambana na ufisadi,hakika Lowassa hawezi kukaa meza moja na Mh.(kwa sababu anachukia sana ufisadi na mafisadi).

Mimi niliwahi kufikiri kwamba wakati wowote baada ya kufunguliwa kwa ile mahakama yetu maalum,ya MAFISADI kutokana na kasi ya Mh.JPM katika swala zima la kupambana na UFISADI pamoja ana RUSHWA,nilitegemea kuona siku moja MAFISADI papa kama walivyokuwa wanashambuliwa na UPINZANI PAMOJA NA CCM kwa nyakati tofauti,wakiwa katika vyama tofauti,basi ilikuwa sawasawa kabisa kufunguliwa angalau mashtaka tu wajibu tuhuma zilizokuwa zimetapakaa kila mahali!

Tunaoweza kufikiria angalau kidogo,tunajiuliza maswali,je,kitendo cha Lowassa kurejea CCM,akiwa na rafiki yake,(ROSTAM)kitarahisisha kushughulikiwa kwa tuhuma zinazowakabili?

Je,Mh.Rais JPM,ameona bora aungane nao tu na kuwasamehe kwa makosa yao?
Je,Rugemarila,na Seth wataachiwa kwa mtirirko huu wa kusawazisha mambo?
Je,wazee wetu,kama Dr.Slaa wataamua sasa kuachana na siasa jumla jumla,kutokana na tabia mbaya za Upinzani na CCM kuwakumbatia watuhumiwa hawa?????

Wasalaam,"KARIBU SANA MZEE LOWASSA,TUSHIRIKIANE KUIJENGA NCHI!!"
 
Siasa bhna ni mchezo mchafu kwelvyama pinzan vnaamin Chama tawala ni mafisad na leo wanarduko huko haya maswala ya siasa jaman yataguweka pabaya bure tuchunge midomo yetu
 
Mimi Nafikiri CHADEMA wawe makini sana ktk kujibu suala hili la Lowasa. Ikiwezekana wampongeze kwa yale +ve aliyowaachia basi, mengine yaendelee. Hakuna namna. Then wahakikishe wajao wasipewe nafasi TENA pale ILI wenye moyo waendelee Kwao. Sisi tusio na vyama Tuendelee kuwaweka sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof huyu wa kusaliti upinzani at prime time. Na kulindwa na wasiojulikana Hadi Kigali. Karudi na mission ya kutengua uamuzi wake. Lkn hapo hapo kutwa Yuko na msajili wa vyama wanapanga njama za uporaji wa fedha. Na wale polisi waliomlinda siku aliyovamia buguruni. Leo hii amekuwa jabali. Hesabu zinaonesha Lipumba sasa anataka kutoswa rasmi. Hii ndio hesabu Kama ambavyo Dr Slaa amedhibitiwa. CCM haijawahi kumuacha mtu salama kea naslahi yake. Mtego umewanasa wote. Slaa na Lipumba. Wenye vyama vyao CUF na CDM hawana Cha kujutia
 
Hivi ni kwa vipi yule aliyeitwa fisadi no 1 nchini siku ya kurejea kwake CCM apokelewe kwa nderemo kubwa na Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu wake??
 
Mtajiuliza maswali mengi majibu wala hamtoyapata aliingia usiku chadema watu wasimuone ametoka mchana kweupe watu wanamuona!
 
Hivi ni kwa vipi yule aliyeitwa fisadi no 1 nchini siku ya kurejea kwake CCM apokelewe kwa nderemo kubwa na Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu wake??
Kwa sababu keshasafishwa na Chadema kuwa sio fisadi bali ni mzalendo wa kweli ha ha ha
 
Kama hilo uliliona mkuu nakupa big up. Lakini bado hatuko salama tumeonesha Chadema tunakumbatia ufisadi ukiwa tu na maslahi.
Damage 2020 huyu jamaa ataongea sana atataja hata kwa exagration kuwa ndani ya CDM kuna uozo ikiwemo hati miliki ya vyeo kama mwenyekiti, Ukanda , Ruzuku nk
Kwa ma Ccm mapokezi yao ni yale ya "The spy is Back" atakaa tu akila popcorn movie ikiendelea
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.

Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.

Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.

Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.

Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof hakuangalia faida,aliangalia maslahi yake binafsi. Wakati anagombea yeye alipata Mbunge mmoja tu Bara. Kaja Lowassa Cuf ilipata Wabunge zaidi. Halafu anapora ruzuku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya lowassa kukiacha njia panda chama hicho, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuondoka kwa mwanachama wake, Edward Lowassa na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutakuwa na madhara yoyote.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 1, 2019 na Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha upinzani Tanzania, Dk Vicent Mashinji muda mfupi baada ya Lowassa ambaye ni waziri mkuu wa zamani kutangaza uamuzi huo.

“Tunamtakia maisha mema huko aendapo yeye ni mtu mzima anajua anachokifanya,” amesema Dk Mashinji.
 
Back
Top Bottom