Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Baada ya mzee Lowasa kurudi nyumbani sasa wapenda mabadiriko tunataka radical politics, kale kazee kalikosema muache siasa za uanaharakati aliwapoteza, Jiwe linahitaji radical politics za jino kwa jino, Mbowe amuondowe sasa Katibu mkuu, na ajihudhuru uenyekiti apewe Lisu na Mbowe arudi kwenye ukatibu mkuu, Mashinji ni mzigo aondolewe haraka, ni Lisu pekee mwenye sifa za kuliongoza jahazi la chadema kwa sasa kuelekea uchaguzi mkuu. Mwisho samahani kwa uandishi mbovu device yangu ina matatizo nimeshindwa kuweka paragraph

Sent using Jamii Forums mobile app
Matola, ninaunga mono hoja.
Masahihisho kidogo: haya maneno niliyopigia rangi nyekundu ni baadhi ya maneno ya msingi katika kuzungumzia siasa. Sio wewe pekee, nimeshaona wana-JF wengine wanakosea tahajia zake sahihi. 'Mabadiriko' liandikwe na kutamkika 'mabadiliko' na 'ajihudhuru' liandikwe na kutamkika 'ajiuzulu'.
 
Mtajiuliza maswali mengi majibu wala hamtoyapata aliingia usiku chadema watu wasimuone ametoka mchana kweupe watu wanamuona!

Kuondoka kwa Lowasa Chadema ni sawa na mtu aliyemaliza mkopo wa benki, what a relief! Siku si nyingi Kitilya,Sioi na Shose watakuwa huru. Mimi binafsi nimefurahi na nimefarijika sana huyu mzee kuondoka Chadema.
 
Longo longo unazo wewe unayelazimisha vitu pasi kufikiri,kumbuka msiba kuna leo mpaka j3 kama Mh Rais aliweza kutoa hadi ndege ibebe maiti unadhani hii haitoshi kueleza kuwa ameguswa?....ninyi ndo mnapenda kujuza vitu vidogo viwe vikubwa ona aibu
Acha longolongo wewe.
Unataka kuniambia pale Lumumba kwenye kumpokea Lowasa hakukuwa na Wawakilishi wa Rais au Mwenyekiti wa CCM(T)?
I'll never buy that cheap and non-sense!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Magufuli na Polepole.

Hawa watu wawili walitushambulia sana eti mafisadi yamewakimbia na yamehamia Chadema. Sisi kweli kama Chadema tulibanwa sana kuhusu Lowassa ila tulijikongoja tuu. Kiuhalisia mwaka 2015 tulipoteza uhalisia wetu kichama ingawa Lowassa kweli alikuwa mtu wa watu. Tulilazimika kuwafanya wengine kukaa kimya maana kama chama tuliua agenda zetu kuu. Hatimaye sasa tutapumua.

Nimeshangazwa sana na mapokezi ya kifalme aliyopewa Lowassa huku serikali kuu zaidi ya nusu wakihamia Lumumba kwenda kumpokea mkubwa yule. Ni kwa mara ya kwanza kuona mtu akipokewa na viongozi wote wakuu wa chama na serikali. Mtu ambaye watu hao hao walidai kawakimbia! Leo wao ndiyo waliomkimbilia! Mbaya zaidi Magufuli anampokea Lowassa huku akiwa kasimamiwa na zee la mipango aka Rostam Aziz. Dah kweli dunia ina mambo.

Lowassa najua amerudi CCM ili kulinda fursa zake kibiashara pamoja na hatima yake ya uzeeni. Ni hayo tu.

Nasubiri kuona sasa mapovu ya kina Polepole na Bashiru baada ya madon kujihakikishia kuwa sasa wamemzunguka mkubwa wao. Acha kabisa siasa hizi za kibongo. Pia nasubiri neno la Slaa (Najua hatosema chochote maana anatumikia)
 
Najua, ila ni nani mpaka rais aende nyumbani kwake?

Wewe inaelekea ubongo wako ni wa rangi ya kijani.....!!! Kwani Rais alipoingia Tweeter na ku-tweet alikwa ana maanisha nini? Rais yeyote makini na mwenye hekima anahusika na kifo cha Mtanzania awaye yote......!!Unakumbuka ile siku Rais alipowalazimisha Ruge na Makonda kupatana kule Tanga??Alikwa akiwapatanisha Ruge kama nani na Makonda?? Try to think big.
 
Kuna Kipindi nilikuwa najiuliza ni Lini Lowassa atarudi Ccm au kustaafu Siasa Kabisa..
Sababu uchaguzi wa 2015 ulipoisha nilikuwa sioni Jipya kutoka kwake .

Asante Yametimia
 
Back
Top Bottom