Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Kwamba Mbowe kumpokea lowassa na lowassa kuondoka ndio ajiuzulu uenyekiti ? Kisa wewe hukupenda basi ndio unataka awajibishwe,ebu niambie unatumia kigezo ghani kujua kwamba jiwe sio fisadi ?
Labda hujaelewa...koza Hilo liliuuzia upinzani kanyaboya na kuwafanya wapoteze uchafuzi.
 
Kwamba RA anaweza kutinga ilkula na ndugu yake akatoka selo.....kunaonesha udhaifu mkubwa sana kwenye utawala wa sheria katika nchi yetu na kwa kweli Jiwe mwenyewe. Kunasema mengi sana kuhusu matumizi mabaya ya madaraka na mfumo wetu wa mahakama. Kesi nyingi dhidi ya upinzani, ni wazi zaidi sasa zina mikono ya wanasiasa.
Kumbuka faini aliyolipa taslimu...kurudi kwa Lowassa je?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Swali langu kwa mwanakijiji ni hili, kama ndoto ya Lowassa kugombea urais 2020 itahuishwa na RA, wewe utasimama upande gani? Unaweza vilevile kumjibia Dr. Slaa kama ukipenda.
Yaani Bado hujui ninaposimama linapokuja suala la Lowassa na Urais?
 
Chonde chonde CHADEMA msidanganyike mkabadili uongonzi katikati ya vita haijawahi kutokea ndiyo maana akina mzee Mandela waliweka demokrasia walipokamata nchi siyo walipokuwa vitani
Yaani umesahau kabisa kuwa walishafanyan hivyo...
 
Jamaa huyu ni mnafiki mkubwa. Anadhani Watanzania wote ni wapumbavu.

Porojo za Mzee Mwanakijiji, tueleze watu hawa ni lini walijiunga na ccm!? Liundi, Jaji Augustino Ramadhani, Robert Mboma, Omar Mahita, Alfred Tibaigana na ukumbuke hawa nafasi zao kiutumishi hazikuwaruhusu kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Rais jana tu amewakumbusha Watanzania siyo mabwege.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother najua watu ambao hamkupenda yale maamuzi mnafikiri huu ndio wakati muufaka kuonyesha hayakuwa sahihi,lakin unajua kampen za arumeru lowassa alikuwa target kwa sababu na yeye alishiriki zile kampen moja kwa moja,japokuwa hakuna aliyenionyesha ni kwa jinsi ghani chadema waliathirika na uchaguzi wa 2015 kwa kumuweka lowassa kama mgombea

Hata ukila chakula chenye sumu utashiba, tatizo sio kushiba bali ni matokeo ya hiyo sumu uliyokula. Kweli matokeo ya 2015 yalikuwa mazuri, je baada ya hayo matokeo mchango wa huyo Lowassa ulikuwa upi? Kama Lowassa aliweza kuleta kura 6,000 mbona hakwenda TLP, UDP nk waliokuwa na uhaba wa kura? 2010-2015 cdm ndio chama kilichofanya mikutano mingi nchini kuliko vyama vyote kwa pamoja, hivyo hizo kura 6m zilitokana na juhudi hizo na sio ujio wa Lowassa.
 
Now you are talking. Tupo tulioumizwa sana na uamuzi ule.

Rudini kazini sasa....

Aliyewasababishia maumivu ameshaondoka na kurudi kwao....

Maisha ni kuumia, kumiizwa na kuumiza wengine....

What is important, is forgiveness....

Kila binadamu anafanya makosa. Wewe unafanya. Mimi hufanya. Kila mtu hufanya.....

Lililo muhimu ni kugundua makosa yako. Unarekebisha na unasonga mbele....

Narudia tena. Aliyewafanya muumie, hayupo ndani ya nyumba. Come back home, safari ya Kigoma inaendelea...
 
Kumkaribisha fisadi lowassa ilikuwa ni kosa kubwa sana lakini bado chadema inapinga kwa nguvu zote ufisadi nchini na uthibitisho wa hili ni kuibua na kupinga uchotwaji kienyeji wa $464 millions kununua ndege, zaidi ya billion 50 kujenga chato airport na ukwapuzi wa trillion 2.4 pale hazina. Chadema pia ilimtetea sana CAG Assad dhidi ya udhalilishwaji wake uliofanywa na kikaragosi cha dikteta, Ndugai.

Hivyo utaona pamoja na kosa kubwa la kumpokea fisadi bado wanapinga ufisadi kwa nguvu zote.

Ukiipima kupitia CHADEMA utakuwa unakosea sana. CHADEMA ipime dhidi ya mitazamo ya wananchi inayotokana na pia uchochezi toka kwa wapinzani wa CHADEMA.

Ndani ya CHADEMA bado tunaamini kwamba tunapambana na ufisadi, lakini ni kweli kwamb watu wengi sana wanatumia kupokelewa kwa Lowassa kama ni kukengeuka kwa CHADEMA kwenye mapambano dhidi ya Upinzani.
 
Hata ukila chakula chenye sumu utashiba, tatizo sio kushiba bali ni matokeo ya hiyo sumu uliyokula. Kweli matokeo ya 2015 yalikuwa mazuri, je baada ya hayo matokeo mchango wa huyo Lowassa ulikuwa upi? Kama Lowassa aliweza kuleta kura 6,000 mbona hakwenda TLP, UDP nk waliokuwa na uhaba wa kura? 2010-2015 cdm ndio chama kilichofanya mikutano mingi nchini kuliko vyama vyote kwa pamoja, hivyo hizo kura 6m zilitokana na juhudi hizo na sio ujio wa Lowassa.
Labda kama ukiniambia ww ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema unaweza ukawa nauhakika kwamba lowassa ajawa na mchango wowote kwenye chama baada ya uchaguzi.kwamba alipokuwa chadema hata Rais mwenyewe alikuwa bado anamuogopa hapo siwez kukaataa ndio maana hata juz chama na serikali nzima imempokea kwa kurudi kwake.mimi mwenyewe nimefurahi lowasa kurudi CCM na wala haijaniumiza kabisa kwa sababu inatoa mwanya zaid ya kina LISSU na wengine kutumia fursa.lakin sibez hata kidogo maamuz ya chama kumchukua lowasa
 
Ulikubali kucompromise principles zako ili tu upinzani uende Ikulu. Kwamba, haikujalisha yote uliyosimamia kabla na kiu yako ya mabadiliko ikakufanya ufumbe macho usione kilichokuwa nikitoka mbele yako. My friend haukuwa peke yako.
Ha ha haaa! Not quite. Sikuamiini kama upinzani unaweza kuingia ikulu. Binafsi nilifikiria zaidi kuongeza idadi ya wabunge na madiwani wa upinzani ili kupunguza nguvu za chama tawala.
Ila kwa utawala wa ngosha, hali itakuwa mbaya sana 2020. Anatumia nguvu za kupindukia;na vitisho juu. Mh! Siwezi kuwa shabiki wake hata kidogo.
Kuna hoja yako moja umesema uncle anasukuma gari kwa mikono yake; badala ya kuliwasha. Hoja hiyo imenifanya nicheke sana. Jamaa ana hulka ya kutumia mabavu.
 
Rudini kazini sasa....

Aliyewasababishia maumivu ameshaondoka na kurudi kwao....

Maisha ni kuumia, kumiizwa na kuumiza wengine....

What is important, is forgiveness....

Kila binadamu anafanya makosa. Wewe unafanya. Mimi hufanya. Kila mtu hufanya.....

Lililo muhimu ni kugundua makosa yako. Unarekebisha na unasonga mbele....

Narudia tena. Aliyewafanya muumie, hayupo ndani ya nyumba. Come back home, safari ya Kigoma inaendelea...
Treni ilitekwa ikaelekezwa Mpanda, bado zinatakiwa juhudi kuirudisha kwenye reli ya kuelekea Kigoma ili tuweze kufika Kigoma.
 
Treni ilitekwa ikaelekezwa Mpanda, bado zinatakiwa juhudi kuirudisha kwenye reli ya kuelekea Kigoma ili tuweze kufika Kigoma.

Haa haaa😀😀😀😀😀haa....

Mtekaji ameshavalishwa "ushanga mwekundu" shingoni na pingu mikononi na miguuni....!!

Hofu ya nini tena?

Japo treni ya kuelekea Kigoma ilitekwa na kuelekezwa Mpanda, lakini mtekaji amekuwa arrested na Treni iko njia moja kurudi Tabora, then ielekee west Kigoma....


Ingieni twendeni!!
 
Fisadi akikaa na mafisadi wenzie unategemea nini? Na huyu ndiye alikuwa kinara kwenye ufisadi wa EPA na Richmond/Dowans. Karudi tena kwenye driver’s seat na mlango wa hazina umeachwa wazi ng’waaaaa shuhudia wizi na ufisadi wa kutisha toka sasa hadi October 2020.

Ila Rostam sijui ametengenezwa na nani. Nguvu yake si ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom