TANZIA Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia

Pole sana kwa Mama Regina, Fred "Cadet", Pamela na familia yote.

Tukiwa shule, Mzee Lowassa akiwa AICC nafikiri bado, kama mzazi wa mwanafunzi mwenzetu , alikuwa anakuja sana shule kufuatilia mambo ya elimu ya watoto, kuongea na walimu. Ni kati ya wazazi niliokuwa nawaona sana wakija shule kufuatilia mambo ya elimu.

Alivyokuja kuingia kwenye siasa na kusisitiza mambo ya elimu nilikumbuka sana na kuona huyu mtu ameishi haya maneno, si mambo aliyoanza kuyasema baada ya kuingia kwenye siasa.

RIP Mzee Edward Ngoyai Lowassa.
 
"Roho ya umauti inaiandama namba mbili kati ya zile awamu SITA"nabii rollinga.alitabiri hivyo!

Pia alitabiri waziri mkuu maarufu sana ataondoka mwaka huu!!

Sisi tunafuatilia unabii tu mkuu!!
Sasa mtu alikuwa mgonjwa wa muda mrefu kapelekwa nje kutibiwa imeshindikana akarudishwa Muhimbili kuvuta vuta siku halafu mtu akisema fulani atafariki ndani ya mwaka huu huo sio utabiri maana tayari anajua ni mgonjwa mahututi.
 
Rais Samia Suluhu ametangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa.

Aidha, bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo Februari 10, 2024.
Angekuwa ana act mapema hivi kwa mambo makubwa ya nchi pia ingependeza.

Umeme kaona tuzoee
Maji mvua zjnanyesha ila hayatok tuzoee
Miradi ya Taifa ni ipi na imefika hatua gani

Nasikia Wizara za Somalia hazina fedha kabisa (hazina hakuna kitu).
 
RIP Kiongozi...

Idea yako ya kuanzisha shule za sekondari kila kata imeendelea kudumu...

Ila zimechakaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…