financial services
JF-Expert Member
- May 17, 2017
- 17,776
- 42,402
R.I.P
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huoni namba 3 hajaweka R.I.P?Hiyo namba 3 lini tena?
Marehemu hasemwi vibaya mkuu [emoji1787][emoji1787]Moja ya mijizi iliyo wafanya watanzania wabaki maskini
Hakuianzisha yeye. Ilianza zama za Mkapa, sema 2006 shule (kata) nyingi zikawa zinajikongoja ndiyo akashupalia zaidi. Ndiyo maana shule kongwe za kata zilifunguliwa 2004, 2005 nyingi 2006.RIP Kiongozi...
Idea yako ya kuanzisha shule za sekondari kila kata imeendelea kudumu...
Ila zimechakaa sana.
Taifa liko gizani hatuna umeme kauchuna! Kaibukia kwingine kana kwamba suala la umeme halimhusu!Angekuwa ana act mapema hivi kwa mambo makubwa ya nchi pia ingependeza.
Umeme kaona tuzoee
Maji mvua zjnanyesha ila hayatok tuzoee
Miradi ya Taifa ni ipi na imefika hatua gani
Nasikia Wizara za Somalia hazina fedha kabisa (hazina hakuna kitu).
Kwa Hilo na matumizi ya maji ya ziwa Victoria EN anastahili Maua yake.Pumzika kwa amani mzee wa Elimu, Elimu na tena Elimu.
Una mchango mkubwa kwenye shule za kata
Ila alikua mwizi na fisadi sana wanasema.Ipo siku atasimama mtu na kurejesha heshima ya Taifa hili. Pumzika kwa amani mzee wetu! Mwamba wa siasa umedondoka
Duh 🙄 !Au Mzee alitaka kuchukua Fomu Chawa wa Mama wakamuagizia Juisi ya Baridi?.
May he rest in Eternal Peace, Ameen.
EDWARD NGOYAI LOWASSA AFARIKI DUNIA
Aliyewahi kugombea nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mtoto wake Fredrick Lowassa amethibitisha na Makamu wa Rais, Philip Mpango amelitangazia Taifa.
Pia, Lowassa aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2008 na kuweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kujiuzulu.
WASIFU WA EDWARD NGOYAI LOWASSAEdward Ngoyai Lowassa anatoka katika jamii ya Wafugaji Kaskazini mwa Tanzania. Alizaliwa August 26 mwaka 1953 katika Kijijini cha Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha. Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.
Kitaaluma Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza (1983-1984).
Uzoefu katika siasa
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni.
Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977.
Kabla ya kugombea Ubunge , aliwahi kutumikia Jeshi la Tanzania na hata kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin kuondolewa madarakani.
Baada ya hapo alikuwa Mtumishi wa Umma kwa miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa Mbunge kuwajilisha Vijana na kujiunga rasmi na siasa.
Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la uchaguzi la Monduli.
Alifanyikiwa kwa miaka yote hii Lowassa ameendelea kulishikilia jimbo hilo la uchaguzi hadi alipolazimika kuliachia ili kuwania Urais.
Mwaka 2015 alipowania Urais haikuwa mara yake ya kwanza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani mwaka 1995, alikuwa miongoni mwa watangaza nia 15, hata hivyo nafasi ikachukuliwa na Benjamin William Mkapa.
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake, Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo, badala yake aliunga mkono rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete.
Je Lowassa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia Kiserikali?
Edward Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.
Lakini pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008, alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha hadi sasa.
Katika siasa, Lowassa anafahamika kama mtu wenye misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo ambatana na maamuzi magumu.
Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake wa kukihama chama hicho. Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa chama chake ulivyoendeshwa.
Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha CHADEMA. Kilichukuwa mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda umoja uitwao, UKAWA katika Uchaguzi wa mwaka 2015
Kufuatia uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa chama tawala na sera aliziunga mkono na kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha wakosoaji wake .
Hii ilikuwa mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu.
===========EDWARD NGOYAI LOWASSA HAS PASSED AWAY
Former Prime Minister of Tanzania and presidential candidate for CHADEMA in 2015, Edward Ngoyai Lowassa has passed away after a long illness. His son Fred Lowassa has confirmed.
Lowassa served as the Prime Minister of Tanzania from 2005 to 2008 and set a record as the first Prime Minister to resign voluntarily.
Profile of Edward Ngoyai Lowassa:
Edward Ngoyai Lowassa was born on August 26, 1953, in the village of Ngarashi, Monduli District, Arusha region, Tanzania. He was the third child of Mr. Ngoyayi.
Educational Background:
Lowassa was an educated individual, holding a bachelor's degree from the University of Dar es Salaam and a master's degree from the University of Bath in the UK (1983-1984).
Political Experience:
Lowassa joined the ruling party CCM immediately after completing his university education in 1977. He served in the Tanzanian military and participated in the war between Tanzania and Uganda that led to the removal of Idi Amin from power.
He later became a public servant before being appointed as a Member of Parliament representing youth and officially entering politics. He successfully contested for the Monduli constituency seat and held it until he resigned to run for the presidency.
In 2015, he ran for the presidency under CHADEMA, which was not his first attempt at the presidency. He had previously contested in 1995 but was not successful.
Lowassa held various government positions, including Minister of Water and Livestock Development, Minister of Lands and Human Settlement Development, and others. He served as the Prime Minister of Tanzania from 2005 to February 7, 2008, when he resigned amid corruption allegations related to the Richmond scandal, which he denied.
Known for his strong political stance and decision-making, Lowassa surprised many by leaving CCM due to dissatisfaction with the party's candidate selection process. He joined the opposition party CHADEMA and was part of the coalition UKAWA in the 2015 elections.
His switch in allegiance raised questions about his political principles and loyalty. This was his second attempt at the presidency.
Rest in peace, Edward Lowassa.
Mnasubiri kuona JK anaongea nini !😂 uzur yule bwana hakosagi la kusemaR.i.P Classmate....😪
Hapa ndipo tutauona unafiq grade one wa wanasisasa kwenye msiba wako..😥
Waziri Mkuu Mjiuzuru?Waziri Mkuu Mstaafu?
Hahahahh! Ile zawadi ya gari atarithi nani!?R.i.P mamvi ex Pm wa nchi ya paradise + R.i.P mzee 97 Years old ex namba 1 nchi ya Eden na ahadi
Kwani hakuna?Kumbe 2015 angepita Leo hii tungekuwa nusu mlingoti
Nusu mlingoti ni lazima ingawa siku ni chache.Kumbe 2015 angepita Leo hii tungekuwa nusu mlingoti
Hakustaafu! Alijiuzuru! Waziri mkuu mjiuzuru!Waziri Mkuu Mjiuzuru?