Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

Nisingekuwekea hiyo hyperlink. Tuendelee kujadili hoja nyingine. Hiyo hoja ya kusema Mungu hayupo kwa sababu Biblia ina contradictions imeishajibiwa kwa undani kwenye hiyo article. Leta hoja mpya.
Hujajibu swali langu kwa namna iliyo wazi na ya kueleweka bila utata.

Awali ya yote, unakubali kwamba Biblia ina contradictions?
 
Hujajibu swali langu kwa namna iliyo wazi na ya kueleweka bila utata.

Awali ya yote, unakubali kwamba Biblia ina contradictions?
Duh, Great Thinker anataka majibu ya "ndiyo" au " hapana" kama mahakamani?
Case closed.
 
Kiranga unasema kua mungu hayupo hilo mbona kwanza kabisaa nataka ujuwe kabisaa kua hakuna mtu asie na dini kila mtu ana dini mfano ww dini yako ni uathesist na wengine kwasababu dini ni imani kwa kua unamini hivo basi ndio dini yako homework nataka unidhibitishie uepo wa vitu vifatavyo upepo imani saa mwaka siku maumivu homa baridi isia nguvu kuna vingine vingi tu ila nimeweza kukumbuka hivo.manake unidhibitishie Kama vilishawahi kuonwa nawatu utanisamehe nitapokua nimekosea kuandika au spelling just curious mana naona kama vile vinafana kuepo kwa mungu
 
Hujajibu swali langu kwa namna iliyo wazi na ya kueleweka bila utata.

Awali ya yote, unakubali kwamba Biblia ina contradictions?
Nimeshakuletea majibu marefu kuhusu Biblia isivyo na contradictions based on mafungu uliyoyaweka. Usiwe mbishi wa kitoto hivyo
 
Hakika huko kwenye giza totoro, hivi unawezaje kumthibitisha kwamba kiranga ni binadamu sio roboti.
Usikalili kwamba kila habar ya uwepo wa Mungu ni uongo utakuja kuumia.
huyo haaamini kwamba Mungu yuko jamani mnajisumbua kumwelezea
 
Duh, Great Thinker anataka majibu ya "ndiyo" au " hapana" kama mahakamani?
Case closed.
Kama huwezi kukubali kwamba Biblia ina contradictions, the fact kwamba umeleta hiyo article kwangu haina uzito.

Unaweza kuleta hiyo article halafu ukawa hujakubali kwamba Biblia ina contradictions, kwa sababu hujui kuisoma.

Halafu usi assume kila mtu hapa anaji identify kama "Great Thinker".

To some of us that is an insult.

Acha kuwa simpleton unaye assume assume vitu tu.
 
Nimeshakuletea majibu marefu kuhusu Biblia isivyo na contradictions based on mafungu uliyoyaweka. Usiwe mbishi wa kitoto hivyo
Hayo majibu yako wapi?

Huu ulimwengu wa hypelink, umeshindwa kuweka link? Umeshindwa kuweka post number?

Nitajuaje kwamba umeweka majibu hayo kweli na hii habari hujatunga tu?

Utajuaje hayo majibu yanaridhisha kama hujaweka link au post number tuyahakiki?

Utajuaje kwamba majibu hayo yanaweza kuonekana sawa kwako, lakini yakakosolewa na watu wengine?

Weka link hapa, weka post number, acha uzembe.
 
Kwanza thibitisha Mungu yupo, au kubali huwezi kuthibitisha hilo.

Kisha tutakuja upande wangu.

Usitake nijibu swali lako, kabla hujajibu langu nililouliza awali.
Huwezi kudhibitisha kuwa Mungu hayupo kwa maana kisichokuwepo hakiwezi kudhibitika. Wewe kwa ujuai wako tudhibitishie kuwa Mungu hayupo.
 
Hayo majibu yako wapi?

Huu ulimwengu wa hypelink, umeshindwa kuweka link? Umeshindwa kuweka post number?

Nitajuaje kwamba umeweka majibu hayo kweli na hii habari hujatunga tu?

Utajuaje hayo majibu yanaridhisha kama hujaweka link au post number tuyahakiki?

Utajuaje kwamba majibu hayo yanaweza kuonekana sawa kwako, lakini yakakosolewa na watu wengine?

Weka link hapa, weka post number, acha uzembe.
Post in thread 'Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi' Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

There you go. Wacha kurukaruka hapa
 
Huwezi kudhibitisha kuwa Mungu hayupo kwa maana kisichokuwepo hakiwezi kudhibitika. Wewe kwa ujuai wako tudhibitishie kuwa Mungu hayupo.
Wewe kwanza jifunze tofauti ya "dhibitisha" na "thibitisha" kabla ya kujifaragua zaidi.
 
Post in thread 'Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi' Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi

There you go. Wacha kurukaruka hapa
Jibu la kwanza tu contradiction, mara Mungu kawambia muitakase Sabato, mara Biblia inasema mjiongeze mnavyofikiri wenyewe.

The whole thing is made up by people, that's why it is full of contradictions.

Mwenzenu mediaman kaleta article imekubali kwamba Biblia ina contradictions.

Namuuliza, unakubali Biblia ina contradictions?

Anajigongagonga kujibu.

Nimeshakueleza ambavyo Biblia haijicontradict au ni lazima jibu litoke kwa mediaman?
Unajua wewe tunachezea watu akili. Umeshakubali na unafahamu kuwa Mungu yupo tatizo unataka tu tukuletee Biblia isiyokuwa na contradictions.
 
Kama huwezi kukubali kwamba Biblia ina contradictions, the fact kwamba umeleta hiyo article kwangu haina uzito.

Unaweza kuleta hiyo article halafu ukawa hujakubali kwamba Biblia ina contradictions, kwa sababu hujui kuisoma.

Halafu usi assume kila mtu hapa anaji identify kama "Great Thinker".

To some of us that is an insult.

Acha kuwa simpleton unaye assume assume vitu tu.
Please, try to read between the lines. Nimekuambia kama ningekuwa sioni contradictions nisingekupa hiyo article. Contradictions zipo na sababu za contradictions zimeelezwa kwa undani sana kwenye article hiyo. In other words, kudai kwamba Mungu hayupo ati kwa sababu Biblia ina contradictions ni kutokuelewa Biblia ni nini na iliandikwaje. Sio kila neno lililoandikwa kwenye Biblia limenenwa na Mungu. Biblia ina maneno ya watu wengi humo. Shetani ana maneno yake humo. Makahaba wamesema yao humo. Wasiomcha Mungu, wachawi, nao pia wamesema maneno yao humo. The Bible is not a pdf doc that was downloaded directly from God in heaven. Please, kama hujaisoma hiyo article, read it carefully na Mungu akusaidie kuelewa.

Mtu anayetaka kuthibitisha kuwa Mungu yupo asubiri siku ya hukumu, inakuja. Atamuona Mungu waziwazi. But it will be too late kuamini wakati huo kuwa Mungu yupo.

JF is also known as the home of great thinkers. Sijaibuni mimi hiyo "slogan"
Na sijasema kila mtu ni Great Thinker. Am not assuming. Nimekutaja wewe binafsi kwa sababu hoja zako zinadhihirisha kuwa level yako ya kufikiri iko juu. Hivyo nimekupa hiyo article uisome ujue na great thinkers wengine wanavyofikiri. Usiegemee upande mmoja tu.
 
Ooh, ni huzuni, ni majonzi, ni maombolezo. Mwenzetu ametutoka akiwa bado kijana. Alikuwa mwema sana, tena mkarimu. Hakupenda ugomvi, fitina wala chuki. Hakuwa mchoyo wala bahili. Wote waliokuwa wakimuomba awakopeshe pesa, walipewa mikopo tena bila masharti. Na wale walioshindwa kurudisha mikopo aliwasamehe bure tu. Akisikia jirani anaumwa, haraka sana alikuwa anaenda kumuona na kumpa pole.

Akiombwa kuchangia sherehe, ujenzi au gharama za misiba, hakusita kutoa mchango. Alikuwa anamiliki nyumba nzuri ya kisasa na magari ya kifahari lakini hakujivuna wala kuwa na kiburi. Unyenyekevu ilikuwa sehemu ya tabia yake. Akialikwa arusini alikuwa anakaa viti vya nyuma. Alikuwa msomi mwenye shahada ya uzamivu. Hata hivyo hakupenda kujikweza wala kuonekana mtu mkubwa. Akisikia ndugu wamefarakana alikuwa wa kwanza kwenda kuwapatanisha. Akisikia mtu amekatishwa tamaa na jambo fulani anamtia moyo kwa maneno mazuri ya faraja. Kinywa chake kilikuwa hakitoi matusi wala maneno ya kashfa au dharau. Alikuwa anampenda sana mke wake. Hakuwahi kumpiga kofi wala ngumi tangu walipooana. Hakika alikuwa mtu mwema sana. Ee Mungu iweke roho yake mahali pema peponi.

Hakukosea aliyesema ‘duniani sisi wanadamu ni wasafiri na wapitaji.’ Magonjwa, ajali, vita nk vinatuondoa duniani hata kabla ya wakati wetu kufika. Hakuna anayeweza kukwepa kifo. Kuna takwimu fulani zinasema kwamba takriban watu 150,000 wanaaga dunia kila siku kwa sababu ya magonjwa tu! Kwa sababu hiyo, misiba imekuwa ikishuhudiwa kila siku pia. Na kila mara wakati wa maziko/mazishi huwa tunawasikia viongozi wa dini au wafiwa wakimuomba Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya mpendwa wao aliyeiaga dunia.

Hapa JF, ‘members’ wanajulikana pia kama ‘Great Thinkers.’ Great Thinker, sio mwepesi wa kuamini au kukubali jambo fulani, bila kulitafakari au kulichunguza kwa makini jambo hilo. Na mimi ni miongoni mwao; nimejaribu kuchunguza Maandiko matakatifu kuhusu sala au maombi hayo tunayomuomba Mungu kwamba awaweke mahali pema peponi wenzetu waliotutoka. Je, Mungu anasikia maombi hayo na kufanya kama tunavyomuomba? Kwa utafiti wangu mdogo, nimegundua Mungu hafanyi kama tunavyomuomba. Mtu akifa, sekunde ile ile roho yake ama inaingia mahali pema peponi au inaingia kuzimu kwenye mateso. Maombi yetu hayawezi kamwe kubadili mahali roho ya mtu inapowekwa. Nimehakikisha hilo kwa kusoma Luka 16:19-31. Kwa sababu hiyo tufanye bidii kuishi maisha mema/matakatifu(Waebrania 12:14) ili siku tukiondoka duniani tuwe na uhakika kwamba Mungu atatuweka mahali pema peponi na kutupatia pumziko na raha ya milele.
Bado unamuomboleza jiwe
 
Please, try to read between the lines. Nimekuambia kama ningekuwa sioni contradictions nisingekupa hiyo article. Contradictions zipo na sababu za contradictions zimeelezwa kwa undani sana kwenye article hiyo. In other words, kudai kwamba Mungu hayupo ati kwa sababu Biblia ina contradictions ni kutokuelewa Biblia ni nini na iliandikwaje. Sio kila neno lililoandikwa kwenye Biblia limenenwa na Mungu. Biblia ina maneno ya watu wengi humo. Shetani ana maneno yake humo. Makahaba wamesema yao humo. Wasiomcha Mungu, wachawi, nao pia wamesema maneno yao humo. The Bible is not a pdf doc that was downloaded directly from God in heaven. Please, kama hujaisoma hiyo article, read it carefully na Mungu akusaidie kuelewa.

Mtu anayetaka kuthibitisha kuwa Mungu yupo asubiri siku ya hukumu, inakuja. Atamuona Mungu waziwazi. But it will be too late kuamini wakati huo kuwa Mungu yupo.

JF is also known as the home of great thinkers. Sijaibuni mimi hiyo "slogan"
Na sijasema kila mtu ni Great Thinker. Am not assuming. Nimekutaja wewe binafsi kwa sababu hoja zako zinadhihirisha kuwa level yako ya kufikiri iko juu. Hivyo nimekupa hiyo article uisome ujue na great thinkers wengine wanavyofikiri. Usiegemee upande mmoja tu.
Mungu wenu alishindwa kufanya kitabu kinachomuelezea kiwe na habari nyoofu isiyo na contradiction?

Kitabu kinaharibika, tafsiri zinaharibika, waandishi wanaharibu habari.

Mungu anaangalia tu? Kalala?

Alishindwa kufanya kitabu cha habari zake kisiwe na contradiction watu tukipime tushangae kwa kuona hiki kitabu hakina contradiction hata moja, mtu akituambia hiki kitabu cha Mungu tuweze kuamini?

Kwa nini kaachia kitabu kinachoeleza habari zake kwa watu kiwe na contradictions?

Kama wandishi wameweza kuandika makosa ambayo yapo mpaka leo kwenye Biblia, tutajuaje habari nzima ya Mungu kuwepo nayo si habari ya kutungwa na watu tu?

Unaelewa kwamba wasomi wa Biblia wanakubali kwamba Biblia imeandikwa na watu tu kusitiri utamaduni wao?

How to Read the Bible​

A Guide to Scripture, Then and Now​

READ AN EXCERPT
Scholars from different fields have joined forces to reexamine every aspect of the Hebrew Bible. Their research, carried out in universities and seminaries in Europe and America, has revolutionized our understanding of almost every chapter and verse. But have they killed the Bible in the process?

In How to Read the Bible, Harvard professor James Kugel leads the reader chapter by chapter through the “quiet revolution” of recent biblical scholarship, showing time and again how radically the interpretations of today’s researchers differ from what people have always thought. The story of Adam and Eve, it turns out, was not originally about the “Fall of Man,” but about the move from a primitive, hunter-gatherer society to a settled, agricultural one. As for the stories of Cain and Abel, Abraham and Sarah, and Jacob and Esau, these narratives were not, at their origin, about individual people at all but, rather, explanations of some feature of Israelite society as it existed centuries after these figures were said to have lived. Dinah was never raped — her story was created by an editor to solve a certain problem in Genesis. In the earliest version of the Exodus story, Moses probably did not divide the Red Sea in half; instead, the Egyptians perished in a storm at sea. Whatever the original Ten Commandments might have been, scholars are quite sure they were different from the ones we have today. What’s more, the people long supposed to have written various books of the Bible were not, in the current consensus, their real authors: David did not write the Psalms, Solomon did not write Proverbs or Ecclesiastes; indeed, there is scarcely a book in the Bible that is not the product of different, anonymous authors and editors working in different periods.

Such findings pose a serious problem for adherents of traditional, Bible-based faiths. Hiding from the discoveries of modern scholars seems dishonest, but accepting them means undermining much of the Bible’s reliability and authority as the word of God. What to do? In his search for a solution, Kugel leads the reader back to a group of ancient biblical interpreters who flourished at the end of the biblical period. Far from naïve, these interpreters consciously set out to depart from the original meaning of the Bible’s various stories, laws, and prophecies — and they, Kugel argues, hold the key to solving the dilemma of reading the Bible today.
How to Read the Bible is, quite simply, the best, most original book about the Bible in decades. It offers an unflinching, insider’s look at the work of today’s scholars, together with a sustained consideration of what the Bible was for most of its history — before the rise of modern scholarship. Readable, clear, often funny but deeply serious in its purpose, this is a book for Christians and Jews, believers and secularists alike. It offers nothing less than a whole new way of thinking about sacred Scripture.
 
Mungu wenu alishindwa kufanya kitabu kinachomuelezea kiwe na habari nyoofu isiyo na contradiction?

Kitabu kinaharibika, tafsiri zinaharibika, waandishi wanaharibu habari.
Hajasema alishindwa. Na kwa kitabu hicho hicho unachokidharau, maelfu kwa maelfu wamemuamini Mungu na kuokolewa kutoka dhambini. Hata wewe utarudi tu kundini. Nakuombea

Unashangaa kitabu kuharibika? Mbona dunia inaharibika. Hata miili yetu wenyewe inachakaa na mwishowe itakuwa mavumbi.
 
Mungu wako alishindwa kuumba dunia isiyoweza kuharibika?

Kama alishindwa, ni kweli ana uwezo wote?

Kama aliweza hakutaka tu, ni kweli ana upendo wote?
 
Kwa nini kaachia kitabu kinachoeleza habari zake kwa watu kiwe na contradictions?
Ndio sababu Mungu ameweka watumishi wa kufundisha na kufafanua hizo contradictions. Ukikaa kwenye kanisa linaloamini wokovu na lenye walimu wazuri wanaofundisha kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu hakuna kitu utashindwa kuelewa katika Biblia.

Waefeso 4:11-14
[11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
[13]hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
[14]ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
 
Back
Top Bottom