EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Mkuu Satoh je unamjua mtu mmoja wa kuitwa DR Ulimboka!!? Huyo Ulimboka yalimpata ya kumpata kipindi cha JK!!
Namkumbuka mzee wa mabwepande.

Lakini enzi ya jiwe hizi mambo Ni Kama zilipigwa muhuri Kaka,au tuseme sisiem Siyo watu wazuri na siyo watu wa kuwaamini.
 
Issue ni pombe au ukweli wa kile alichokisema?

Kama hoja yake ni positive kwanin tuamue kumjaji kwa issue zilizo nje ya alichokisema
 
Mjizo jana alikua na Mkwere pale Bwaga Moyo tamashani Msoga....unategemea nini.
 
Magufuli hakupenda kusifiwa you are getting it wrong, isipilokuwa chawa na kunguni na papasi waliozunguka, yeye alikua focused na kazi zake tu za kuikwamua Tanzania. Sema tu ule usemi wa mzigo mzito mpe Punda wa kinyamwezi.
 
Watu kama wewe kwenye nchi nyingine ni "mboga mchemsho"


Acha kabisa kuvaa uwehu kichwani mwako.
 
Yes jamaa huwa anauma kotekote. Hata simba na yanga huwa anazipopoa zote tu licha ya kuwa yeye ni simba.
Hata mimi nishawahi kumsikia mara kibao tu akiisifu serikali kwa miradi yake hususani swala la mradi wa umeme ambapo na yeye alienda kabisa kule mwl Nyerere. Hata ukienda kwenye clip zake instagram ushahidi upo.

Shida ya ccm wanataka kusifiwa tu, hata ukiona madhaifu wewe sifu na kuabudu. Ukisema ukweli unaouma tu, shida hiyo.
Ni kweli nchi inakopa hovyo hii.
 
Sasa kama si Msimamo wa Taasisi wanahangaika kwanini kumwadhibu Hando?
 
Ni muda muafaka Sasa media industry ikaondoa majitu mahuni, huyu arudi pale Masai pub akapige miziki
Sio Bure Hando alishawahi kukung'ata kisha akaku_dump. Umebaki na makasiriko. Akiondolewa hapo ndio utaajiriwa wewe!?
 
Tunahitaji katiba mpya ambayo italetq usawa ktk taifa letu ccm ni shida
 
Yaani wakuu sijuhi tufanye nini?? serikali ya tanzania ipo juu ya kila kitu ipo juu ya bunge, mahakama,na sasa juu ya wananchiii wanataka waboronge waue nchiiii Sisi tukae kimyaaaa.Hawasomi katiba wanaongoza kwa akili zao tunapoelekea wataharibu wasipende kukurupuka wafate sheria ipo siku kutanuka nakwambia tuna hasira saaana.
 
Ukifikiria Kwa kina, Utagundua jamaa anaitetea taasisi Ili wapate ugali wao wa kila siku.
Tukisema media imuunge mkono Hando inaweza kula kwao Hasa hasara itakua ya Media,

Sometime hii nchi yabidi kua Chawa. Ili maisha yaende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…