EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Lakini haya mengine hatujui kama wanasakamwa na serikali, au wanajipendekeza wenyewe tu kwa self censorship.
 
Kabla ya Magufuli media ganii ilikuwa inaichana serikali ????

Lini Tanzania imewahi kuwa na free press ????
Mkuu,enzi ya kikwete angalau Uhuru ulikuwepo tofauti na alipoingia Magufuli,japo haikuwa kwa % Mia ila angalau wakosoaji hawakupata misukosuko Kama enzi za jiwe na mwendelezo Hadi Sasa enzi ya mama.

Katika Hilo angalau tuseme ukweli. Nakuhakikishia kwa alichosema Hando na Ndugai ingekuwa enzi ya kikwete Wala kusingetokea yaliyotokea.
 
Hahahahahahahaha we jamaa ni hatari
 
Ni kama una bifu na Hando! Punguza chuki
 
Tatizo lilianzia kwa Magufuli hili. Nchi imekuwa ya hovyo Sana.

Hata Mungu anakosolewa sembuse sisiem.
Mkuu,

Haya mambo yalikuwapo tangu enzi za Nyerere.

Watu walifungwa kwa kumkosoa rais. Mpaka vyama vingi vikafutwa.

Kama hujasoma, tafuta hiki kitabu "Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960-1964" cha Paul Bjerk.

Haya hayakuanza na Magufuli.

Magufuli kaja kufanya kijinga tu mpaka kipofu kaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…