EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

Majizo na kampuni yake wanatafuta ugali sasa channel ilishakamata halafu mtu mmoja anahoji mikopo wakati hiyo serikali ndo ina TRA, INA BRELA, TCRA, INATAWALA hapo kama Gerald Hando ajitokeze aombe msamaha hadharani na akae nje ya kituo mwezi 1 atakuwa amejirekebisha
Alitakiwa asome maudhui ya radio na TV yao
 
Yaan unachoongea ,inaonekana hauna ufahamu na uelewa wa philosophy za dunia hii.Kwa ufupi hauna elimu ya kutosha.Unajadili issue sensitive Kama mtoto mdogo w darasa la saba B.Nimeshituka sana kuona material zako zikiwa pointless.Nikwambie Tanzania sio kisiwa.Ipo siku kila kitu kitakuwa sawa.Jaribu kusoma theory za dunia kwenye vitabu usibaki nyuma unaonekana upo empty kabisa.
Kwa hiyo hii comment yako ndio Ina ishara za usomi?
 
TANGAZO la MD wa E-FM la kumchukulia hatua Gerald Hando limetolewa kiwa Chalinze Msoga hii ina maana gani wa
20221231_181825.jpg
dau tuchambue kinagaubaga
 
Kiukweli nimeshangaa sana ni nini kimemtuma Majizzo kuomba msamaha kwenye public? Kuna jambo lolote baya kutoka kwa hando? Maana yeye alisema binafsi hafurahishwi na serikali kukopokopa kama raia wa nchi ana haki ya kuishauri serikali na kutoa dukuduku lake kama katiba inavosema.

Kwani hando kuna sehemu kadanganya? Si kweli tunakopa? Kama hakuna ubaya kukopa kwanini Majizzo anaomba msamaha? Kama taifa tuna safari ndefu sana.

View attachment 2464611
Yaani wote tuungane na msimamo wa serikali kwa lazima hata kama tuna mawazo tofauti?
 
Majizo na kampuni yake wanatafuta ugali sasa channel ilishakamata halafu mtu mmoja anahoji mikopo wakati hiyo serikali ndo ina TRA, INA BRELA, TCRA, INATAWALA hapo kama Gerald Hando ajitokeze aombe msamaha hadharani na akae nje ya kituo mwezi 1 atakuwa amejirekebisha
Alitakiwa asome maudhui ya radio na TV yao
Kuna Kosa gani amefanya?
 
SAKATA la Gerald Hando kuchukuliwa hatua na uongozi wa E-FM kwa kusema hafurahishwi na Serikali inavyokopa kopa unatupa mashaka makubwa sisi wasikilizaji na wadau wa E-FM na kuanza kujiuliza upya kama kweli Majizo ndiye mmiliki halali wa E-FM
View attachment 2464670

View attachment 2464673
Mali ni ya Majizo ila uamuzi wa Majizo ni wa kwake binafsi na hataki matatizo na Mamlaka na wewe tafuta chombo chako cha mawasiliano fanya kama Hando life ni tight mno kwa sasa why uingie matatizo na Mamlaka tena kupitia kwa mtu ambaye hajui umetafutaje hizo Mali kwa jasho kubwa?
 
Wamesema wanazingatia sheria lakini kwenye andiko hilo hawajatuambia huyo Hando amevunja sheria ipi? Haya mambo ya kuiogopa serikali hata mahala ambapo hujavunja sheria ni mambo ya kipumbavu yaliyoanza enzi za Marehemu. Marehemu ametuharibia nchi.
 
Muhimu ujumbe ulishafika, hii serikali inasifa zote za kidikteta, haina tofauti yoyote na ile iliyopita.

Majizzo anaposema wasikilizaji wa EFM wamemlalamikia kwa ile kauli ya Hando ni kama anatuona watanzania wote wajinga, bora angetafuta excuse nyingine..hii aliyoitoa amejitungia tu.
 
Amekiuka maadili ya taaluma, ashughulikiwe vilivyo, suala la umiliki halihusiani.

Ni wakati muafaka kuondoa watu wa hovyo katika tasnia
Maadili gani ya umma aliyokiuka Hando?

Suala la public kujadiliwa public kuna ubaya gani? kwani hiyo mikopo inamuhusu nani mpaka isijadiliwe na umma? na ni nani wanaolipa hiyo mikopo kama sio watz? sasa kwanini walipaji wasiruhusiwe kuijadili hiyo mikopo inayowahusu?

Listen, haya mambo ya kijinga ya kusifia muda wote hufanywa na wapumbavu pekee, lakini werevu watakaa kimya kwa muda fulani, ila iko siku wataongea ukweli, hicho ndicho Hando alichofanya, na kitafanywa na mwingine tena next time, hili sio taifa la wapumbavu kama mnavyotaka liwe.
 
Back
Top Bottom