Egypt: Hii siyo sawa kuwafanyia ndugu zenu. Kuna nini Kinaendelea hapa?

Egypt: Hii siyo sawa kuwafanyia ndugu zenu. Kuna nini Kinaendelea hapa?

Makundi yote ya kigaidi ya Iran, yanachukiwa na nchi zote za kiarabu.

Ukiwakaribisha Hamas, Hezbollah au Houthis, ujue umeingiza ushetani nchini mwao. Wale biashara yao kuu ni ugaidi. Hawawezi kupata pesa ya Iran mpaka wathibitishe wapo kwenye mapigano.
Hongera mhitimu wa Sunday school
 
Kweli kabisa ndio maana katika Salafi tunaitakidi kwamba alqaida, ISS bokoharam, alshabab , hao ikhwaan muslimeen ni katika wapotofu kwani hawafuati mafundisho ya Mtume Mohamad S.A.W na wema waliotangulia katika karne tatu bora .. lakini ukiongea haya maneno wasiojua dini yao na kufuata mihemko watakusema na kutukana mpaka basi
Salaf?ndo wale mapro wa Saudia au????
 
Inachokifanya Egypt ni tahadhari ya athari mbaya zinazoweza kutokea kwa kuchukua watu wengi waliotoka kwenye machafuko ya kivita.
Kumbuka yaliyotokea Lebanon na madhara yake hadi sasa, yaliyotokea Jordan na mataifa mengine mengi ulaya
Kuchukua wakimbizi wengi nchini kwako ni sawa na kuanzisha taifa jingine nchini kwako, na mbaya zaidi wanajihisi ni kwao na wanaurahisi wa kuanzisha vikundi vyao vya kijeshi vinavyoweza kutumiwa na watu wenye nia ovu na nchi yako. Kumbuka tena ya Lebanon utawaelewa wa Misri. Saudia yenyewe ndo haiwataki kabisa maana wanajua utakuwa mlango wa kuingiza machafuko kupitia washirika wa iran haswa Hezbollah na waHouthi wa Yemen.
Geopolitics ni zaidi ya dini hapo Mashariki ya kati.
Hapa Tanzania tunajua jinsi mapori ya Tabora na Kigoma yalivyokuwa hatari, uhalifu wa kutumia silaha ulishamiri sana maeneo hayo iliwemo utekaji wa magari. Mengi yalihusianishwa na wakimbizi wa Kongo na Burundi.
 
Back
Top Bottom